Serikali isiishie tu kukanusha madai ya wapinzani kuwa maisha yao yapo hatarini, bali iwahakikishie usalama wao

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Kumekuwa na madai mengi ya wapinzani kuwa maisha yao yapo hatarini kwa kuwa wanatishiwa maisha na "watu wasiojulikana"

Imefikia hatua ya viongozi wetu wa upinzani, hususani wa Chadema, kuikimbia nchi hii na kwenda kutafuta hifadhi ya kisiasa nje ya nchi.

Miongoni ya viongozi waliopata Hifadhi ya kisiasa nje ya nchi ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ambaye amepata Hifadhi nchini ubelgiji na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbless Lema, aliyepata Hifadhi nchini Canada.

Wakati wote ambao viongozi wa upinzani wanapotoa madai ya kutishiwa maisha yao, msemaji wa Serikali Dkt Mohamed Abbas, amekiwa akikanusha kuwa madai hayo ya wapinzani ni ya uongo na nchi hii ipo salama kabisa kwa mwananchi yeyote kuishi.

Nimuulize maswali machache Dkt Abbas, kama kweli nchi yetu ipo salama kivile kama anvyodai, ni kitu gani kimesababisha wale waliompiga risasi Tundu Lissu, kwa lengo la kummaliza, miaka zaidi ya mitatu ilyopita, hakuna hata mshukiwa mmoja ambapo Jeshi la Polisi limemkamata na kumburuza mbele ya vyombo vya sheria?

Iwapo nchi yetu ipo salama kama msemaji wa serikali Dkt Abbas anavyodai, ni kwanini hadi Leo zaidi ya miaka 4 imepita, Jeshi la Polisi nchini halijamkamata hata mtuhumiwa mmoja, kuhusiana na mauaji ya Mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Alphonce Mawazo, aliyeuawa kinyama kwa kukatwa katwa na mapanga mchana kweupe?

Hivi huyu msemaji wa serikali Dkt Abbas, ni kwanini anapenda.kutupiga bla bla, wakati hali halisi ikionekana wazi kuwa kuwa mpinzani, hususani kuwa kiongozi wa chama cha Chadema nchini, ni sawa sawa na kuonekana kama mhaini nchi hii na umejitumbukiza kwenye tanuru la moto?
 
Mbona wenzao wapo huko "ubeberuni"kitambo?

Au kuna nani mwingine aliyetishiwa uhai?

Uongo utawasaidia nini kwa mfano??🤔🤔
 
Nawe ondoa uzembe wako hapa! Nchi hii siyo ya wanasiasa wa upinzani tu! Wote tunahitaji kuhakikishiwa usalama. Kwa nini unataka atoe uhakika kwa wanasiasa wa upinzani tu? Kama nchi haifai waoneshe mediteraniani wakazame! Kila siku tuwe tunajadili mambo ya upinzani tuuuu!
 
Nawe ondoa uzembe wako hapa! Nchi hii siyo ya wanasiasa wa upinzani tu! Wote tunahitaji kuhakikishiwa usalama. Kwa nini unataka atoe uhakika kwa wanasiasa wa upinzani tu? Kama nchi haifai waoneshe mediteraniani wakazame! Kila siku tuwe tunajadili mambo ya upinzani tuuuu!
Hivi wewe unajua kuwa jukumu namba moja la Jeshi la Polisi ni kulinda usalama wa raia na Mali zao?

Sasa kama Jeshi la Polisi limekuja na msamiati mpya wa "watu wasiojulikana" ili kulinda vibarua vyao ni kwanini IGP Sirro asiwajibike kwa kujiuzulu?
 
Back
Top Bottom