Serikali isigawe bure ARV, inachochea uzinzi

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
32,937
2,000
Kwa kifupi
Kwa vigezo vilevile vilivyotumiwa kutokuruhusu watoto waliodungwa mimba mashuleni kwamba kurudishwa mashuleni kutachochea uzinzi. Kuna haja sasa ya serikali hii ya awamu ya tano kupiga marufuku ugawaji bure wa ARV kwa wagonjwa wa UKIMWI kwa kuwa inachochea uzinzi.

Magufuli atoe tamko kila mtu abaki na mkewe/mumewe, na hakuna kufanya ngono nje ya ndoa. Kwa kuwa vitabu vya dini zote vimekataza uzinzi, hivyo serikali itumie kigezo hicho kwa sababu hakina tofauti kabisa na kigezo ilichotumia kwa wanafunzi wa kike

Nadhani nimeeleweka
 

keithevans2685

Senior Member
Dec 17, 2014
110
225
Mawazo mgando hayo,umeshasoma recent statistics toka ARV zianze kugawiwa!!?Maambukizi yameongezeka!!?

Je kipindi chote ambacho ARV zilikuwa hazitolewi,maambukizi yalikuwa chini kuliko kipindi ambacho ARV zimeanza kutolewa!!?

Unajua kiasi gani,ARV inapunguza maambukizi ya mama kwenda mtoto,Kati ya wanandoa!!?

Unafikiri kuacha kutoa kutapunguza maambukizi kwa study gani,uliuofanya!!?
 

The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,412
2,000
Omba yasikukute.

Utakuwa hauwatendei haki wale waliozaliwa wakiwa tayali wamevipata na sasa hivi wako wengi kuliko walioambukizwa kwa ngono zembe.

Ni haki yao kupata dawa kama wapatavyo Wagonjwa wengine.

Pia dawa hizo ni za hisani kutoka Taasisi za nje.
 

Dahafrazeril

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,501
2,000
Omba yasikukute.

Utakuwa hauwatendei haki wale waliozaliwa wakiwa tayali wamevipata na sasa hivi wako wengi kuliko walioambukizwa kwa ngono zembe.

Ni haki yao kupata dawa kama wapatavyo Wagonjwa wengine.

Pia dawa hizo ni za hisani kutoka Taasisi za nje.
Good Thinking Mkuu!

Licha ya kuzaliwa nao (UKIMWI), pia zipo njia nyingi mno za maambukizi tofauti na Mleta mada alivyo base katika Njia moja tu (Ngono zembe).

Kwa uchache tu ni, kuwekewa damu yenye maambukizi ya UKIMWI katika taasisi za Afya, Ku-share zana zenye ncha kali pamoja na mwathirika nk.....(You can add).

Nadhani tatizo ni Uelewa mdogo juu ya Maambukizi ya Ugonjwa wenyewe na si vinginevyo.
 

silasc

JF-Expert Member
Feb 10, 2013
3,354
2,000
Nimekuelewa mkuu mleta uzi ujumbe uliotaka kufikisha. Aisee!
 

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
134,568
2,000
Nenda huko vijijini ukaone watu walivyo masikini halafu wana UKIMWI. Fikiri kabla ya kutoa post. Siyo wote tuna uwezo wa kula pilau leo!
 

tofali

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
4,013
2,000
Ngoja uupate ndio utajua umuhimu wa hizi dawa....
Usidhani uzinzi pekee ndio utakufanya upate ukimwi..
Unajua PEP?
Sasa subiri dawa ziondolewe halafu kitoto chako cha miaka 3 kibakwe na muathirika...
Unajua wafanya kazi wa afya wanajichoma mara ngp na sindano wanapokuwa wanahudumia waathirika...??
Unajua wanatumia nini kujizuia virusi visianze kuzaliana muda ule alipojichoma.?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom