Serikali pitieni upya Sera ya 'Elimu Bure', ikiwezekana ifutwe kabisa

Alwatan kamba

Member
Nov 16, 2020
70
150
Ingawa ni jambo jema kwa serikali kutoa elimu bure ili kusaidia watoto watokao kaya maskini kupata elimu ya msingi lakini huu mpango unafaa kuangaliwa upya kwa sababu utekelezaji wake una hasara nyingi kuliko faida.

Hasara ya kwanza: Tangu kuanzishwa kwa sera ya elimu bure, serikali imeshindwa kuajiri walimu wa kutosha na hivyo kusababisha uhaba mkubwa wa walimu hususani wa masomo ya sayansi mashuleni na hivyo kupelekea wanafunzi wengi kufeli masomo hayo katika mitihani yao ya kidato cha nne.

Kadhalika, ukosefu wa walimu pia unachangia wanafunzi kukata tamaa ya kusoma baadhi ya masomo hasa ya sayansi na wengine huamua kuacha shule kabisa na kujichanganya mtaani. Hii yote ni kwasababu serikali inatumia gharama kubwa zaidi ya billions 20 kwa mwezi kuhudumia elimu bure na hivyo kupunguza kiwango cha bajeti cha kuajiri walimu wapya kwa mwaka.

Hasara ya pili: Kufuatia mpango wa elimu bure, upatikanaji wa vifaa muhimu vya kufundishia na kujifunzia kama vile vitabu, vifaa vya maabara na kemikali za kufanyia majaribio upatikanaji wake umekuwa sio wa kuridhisha na hivyo kufanya walimu pamoja na wanafunzi kujifunza katika mazingira magumu. Hii inaweza kuwa inachangiwa na ucheleweshaji wa kupeleka pesa za kuhudumia elimu bure katika baadhi ya halmashauri au bajeti kubwa kupelekwa kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya shule na kusahau eneo muhimu la ununuzi wa vifaa vya kielimu.

Hasara ya tatu: Serikali inatumia gharama kubwa kulipia wanafunzi ada ambao saa nyingine huamua kuacha ama kufukuzwa shule na hivyo kufanya serikali kuingia katika gharama zisizokuwa na msingi.

Hasara ya nne: pamoja na serikali kutoa elimu bure bado kuna changamoto ya madawati na hivyo kupelekea wanafunzi kusoma katika mazingira duni ya kukaa chini hasa katika vipindi vya darasani.

Hasara ya tano: Tangu serikali ianze kutoa elimu bila malipo kumekuwepo na ufuatiliaji mdogo wa wazazi kuhusu maendeleo ya watoto wao(wanafunzi). Hali hii inachangia kushusha kiwango cha taaluma mashuleni kwakuwa ufuatilaji wa maendeleo ya wanafunzi kwa asilimia kubwa umekuwa ukifanywa na walimu pekee. Katika hili, wazazi wamejiweka kando kutokana na kwamba hakuna hasara yoyote wanayopata kwakuwa gharama zote zinalipwa na serikali.

Hasara ya sita: Elimu bure imechangia kudumaza ushiriki wa wazazi katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo. Mfano, ushiriki katika ujenzi wa shule, ushiriki katika upanuzi na ujenzi wa madarasa. Linapotokea suala la kuchangia shughuli kama hizo wazazi wamekuwa wagumu wa kuchangia huku wakidai ni elimu bure hivyo hatutakiwi kuchanga chochote.

Kufuatia hasara hizo na zingine ambazo hazijatajwa, napendekeza elimu bure ifutwe badala yake wazazi waendelee kulipa ada na serikali ifanye yafuatato:

1. Serikali itumie bajeti ya kutoa elimu bure kununua na kuhakikisha kuna vifaa vya kutosha vya kielimu mashuleni.

2. Serikali itumie bajeti ya kutoa elimu bure kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa madawati ya kutosha mashuleni ili watoto wasiendelee kukaa chini.

3. Serikali itumie bajeti ya elimu bure kuajiri walimu wa kutosha mashuleni ili kuinua kiwango cha taaluma katika sekta ya elimu.

4. Utekelezaji wa elimu bila malipo uanze baada ya changamoto zote kwenye sekta ya elimu hususani mashuleni kufanyiwa kazi.

5. Hakuna haja ya elimu bure kwakuwa wazazi wanao uwezo wa kusomesha watoto wao lakini hawana uwezo wa kuwaajiri katika ujira wa kudumu. Hivyo ipo haja ya bajeti ya elimu bure kutumika kuangazia kutoa fursa za ajira kwa vijana.

6. Kama kuna umuhimu wa Sera ya elimu bure kuendelea kuwepo basi ihamishiwe katika ngazi ya elimu ya juu(vyuo vikuu) kwakuwa ndiko kwenye gharama kubwa kuliko huku chini ambako mzazi anaweza kupambana kwa biashara ya kuuza ubuyu, karanga au kilimo cha bustani na kumsomesha mwanae.
 
Mapensho star

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
2,692
2,000
Serikali iliiga sera ya chadema kutoa elimu bure kwa kukurupuka kwa hili nakuuunga mkono mana serikali inagharamia elimu ambayo haiwasaidi watoto kujikomboa wanafunz wengi wanaishia kidato cha nne na tano wameishia kusoma mambo mengi lakini hayawezi kuwasaidia
 
TZ-1

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
318
250
Uchambuz wako huo kwangu Mimi nimeona sababu moja na sijui Kama inahusiana na elimu bure
Kuhusu kuajir walmu kutokan na uhaba.
 
MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
1,627

Serikali haihitaji watu Makini.

Serikali inahitaji mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi tu, kutii mamlaka na kulipa kodi.

Si zaidi ya hapo.

Sasa kwa changamoto zote ulizotaja, unaona zinaathiri mambo hayo ?
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
1,909
2,000
Siku zote vya bure vinalemaza na hapa wanatafutwa wapiga kura tu wasiojielewa
Kama hiyo haitoshi mambo ya bure yanajenga akili tegemezi na kuua ari ya kujituma na ubunifu
 
Therapist 2015

JF-Expert Member
Aug 4, 2018
676
1,000
R. P

UCHAMBUZ WAKO NIMEUPITIA
Naunga mkono Sababu moja ambayo sizan Kama inauhusiano wa ajira na Elimu Bure (capitation)

Sasa apo kama ujaelew jua unacho post ume copy au haupo katk hyo field.
Angalau nimeielewa, kwa maoni yangu Elimu bure na ajira kuna uhusiano mkubwa kwasababu ifuatayo,

Elimu bure imeua shule nyingi za private kupelekea shule hizo kukosa wanafunzi , ambapo shule za private , zilikuwa zinaajiri kwa wingi.
 
ruaharuaha

JF-Expert Member
Feb 14, 2018
1,832
2,000
Ingawa ni jambo jema kwa serikali kutoa elimu bure ili kusaidia watoto watokao kaya maskini kupata elimu ya msingi lakini huu mpango unafaa kuangaliwa upya kwa sababu utekelezaji wake una hasara nyingi kuliko faida.

Hasara ya kwanza: Tangu kuanzishwa kwa sera ya elimu bure, serikali imeshindwa kuajiri walimu wa kutosha na hivyo kusababisha uhaba mkubwa wa walimu hususani wa masomo ya sayansi mashuleni na hivyo kupelekea wanafunzi wengi kufeli masomo hayo katika mitihani yao ya kidato cha nne.

Kadhalika, ukosefu wa walimu pia unachangia wanafunzi kukata tamaa ya kusoma baadhi ya masomo hasa ya sayansi na wengine huamua kuacha shule kabisa na kujichanganya mtaani. Hii yote ni kwasababu serikali inatumia gharama kubwa zaidi ya billions 20 kwa mwezi kuhudumia elimu bure na hivyo kupunguza kiwango cha bajeti cha kuajiri walimu wapya kwa mwaka.

Hasara ya pili: Kufuatia mpango wa elimu bure, upatikanaji wa vifaa muhimu vya kufundishia na kujifunzia kama vile vitabu, vifaa vya maabara na kemikali za kufanyia majaribio upatikanaji wake umekuwa sio wa kuridhisha na hivyo kufanya walimu pamoja na wanafunzi kujifunza katika mazingira magumu. Hii inaweza kuwa inachangiwa na ucheleweshaji wa kupeleka pesa za kuhudumia elimu bure katika baadhi ya halmashauri au bajeti kubwa kupelekwa kwenye ujenzi wa miundo mbinu ya shule na kusahau eneo muhimu la ununuzi wa vifaa vya kielimu.

Hasara ya tatu: Serikali inatumia gharama kubwa kulipia wanafunzi ada ambao saa nyingine huamua kuacha ama kufukuzwa shule na hivyo kufanya serikali kuingia katika gharama zisizokuwa na msingi.

Hasara ya nne: pamoja na serikali kutoa elimu bure bado kuna changamoto ya madawati na hivyo kupelekea wanafunzi kusoma katika mazingira duni ya kukaa chini hasa katika vipindi vya darasani.

Hasara ya tano: Tangu serikali ianze kutoa elimu bila malipo kumekuwepo na ufuatiliaji mdogo wa wazazi kuhusu maendeleo ya watoto wao(wanafunzi). Hali hii inachangia kushusha kiwango cha taaluma mashuleni kwakuwa ufuatilaji wa maendeleo ya wanafunzi kwa asilimia kubwa umekuwa ukifanywa na walimu pekee. Katika hili, wazazi wamejiweka kando kutokana na kwamba hakuna hasara yoyote wanayopata kwakuwa gharama zote zinalipwa na serikali.

Hasara ya sita: Elimu bure imechangia kudumaza ushiriki wa wazazi katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo. Mfano, ushiriki katika ujenzi wa shule, ushiriki katika upanuzi na ujenzi wa madarasa. Linapotokea suala la kuchangia shughuli kama hizo wazazi wamekuwa wagumu wa kuchangia huku wakidai ni elimu bure hivyo hatutakiwi kuchanga chochote.

Kufuatia hasara hizo na zingine ambazo hazijatajwa, napendekeza elimu bure ifutwe badala yake wazazi waendelee kulipa ada na serikali ifanye yafuatato:

1. Serikali itumie bajeti ya kutoa elimu bure kununua na kuhakikisha kuna vifaa vya kutosha vya kielimu mashuleni.

2. Serikali itumie bajeti ya kutoa elimu bure kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa madawati ya kutosha mashuleni ili watoto wasiendelee kukaa chini.

3. Serikali itumie bajeti ya elimu bure kuajiri walimu wa kutosha mashuleni ili kuinua kiwango cha taaluma katika sekta ya elimu.

4. Utekelezaji wa elimu bila malipo uanze baada ya changamoto zote kwenye sekta ya elimu hususani mashuleni kufanyiwa kazi.

5. Hakuna haja ya elimu bure kwakuwa wazazi wanao uwezo wa kusomesha watoto wao lakini hawana uwezo wa kuwaajiri katika ujira wa kudumu. Hivyo ipo haja ya bajeti ya elimu bure kutumika kuangazia kutoa fursa za ajira kwa vijana.

6. Kama kuna umuhimu wa Sera ya elimu bure kuendelea kuwepo basi ihamishiwe katika ngazi ya elimu ya juu(vyuo vikuu) kwakuwa ndiko kwenye gharama kubwa kuliko huku chini ambako mzazi anaweza kupambana kwa biashara ya kuuza ubuyu, karanga au kilimo cha bustani na kumsomesha mwanae.

Hizo changamoto zinaweza kutatuliwa. Ikumbukwe ni miaka mitano tu toka elomu bure ianze lazima kuwe na changamoto baadaye kutakuwa na maboresho.

Serikali ijitahidi kuongeza wigo, namba za walipa kodi na vyanzo vipya mbalimbali vya mapato. Sekta za madini, utalii wa ndani na nje, (ufugaji, kilimo, fisheries hapa inabidi kutafuta zaidi masoko ya nje).

TRA ijipange zaidi kuwasaidia, kuwaelimisha na kushirikiana wafanyabiashara na kuhamashisha wananchi kufanya biashara na kupunguza vitendo vya uonevu, kupanga kodi ambazo ziko fair, zinazoenda na hali halisi ya biashara husika. Ili pesa zitakazopatikana zitumike kujenga shule, vifaa, kununua madawati na kuajiri walimu.

Hii (Elimu bure) ni sera nzuri, itabaki kuwa nzuri. Changamoto siku zote zipo inabidi kukabiliana nazo head on, kutafuta ufumbuzi, kuongeza kasi ya maboresho.

Hivi vyote vitategemea mapato ya serikali.

Kuhusu watoto kuacha shule, ufuatiliaji wa wazazi, elimu itolewe kwa wazazi kuwakumbusha majukumu yao kwa watoto wao.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,558
2,000
Uzeni ndege muingize hela kwenye elimu, maana ndege ndio zinakula hela nyingi kwani ni biashara yenye hasara. Kila siku rais anasema nchi hii ni tajiri, ww ni nani wa kuanza kuisemea serikali? Kama mambo ni magumu tokeni mseme mmekwama, na mtuambie ni kipi kimewafanya mkwame wakati mlikuwa na sifa zilizopitiliza. Sasa hivi tunakusanya zaidi ya 1.5t, elimu bure inawashindaje kwa mfano?
 
Drifter

JF-Expert Member
Jan 4, 2010
2,594
2,000
Prioritisation! Vipaumbele!

Serikali hii imejitwisha mizigo mizito sana. Kufanya miradi mikubwa kama Stieglers Gorge HP, SGR na kununua ndege kwa cash - kwa pesa za ndani - HALAFU utoe elimu bure hadi sekondari -KWA MPIGO ni mzigo ambao uchumi tulio nao hauwezi kuhimili. Kudai nchi ni tajiri; ina hela nyingi sana zilizokuwa zinaishia kwa mafisadi ni KUJIDANGANYA. Sio kihivyo.

Hapo ndipo umuhimu wa kushirikisha taasisi zote muhimu unapoonekana. Wizara ya ya Uchumi na Fedha/Tume ya Pipango, Benki Kuu, Bunge na Kamati zake n.k. vyote vilipaswa kutumika (properly engaged) kubainisha yanayowezekana (feasible) ili kutekeleza sera na ahadi kulingana na uharaka wa mahitaji na rasilimali (fedha/wataalamu) zilizopo. Kudharau mfumo ni kuingia gizani na kujiletea maumivu yasiyo na sababu.
 
Alwatan kamba

Member
Nov 16, 2020
70
150
Uchambuz wako huo kwangu Mimi nimeona sababu moja na sijui Kama inahusiana na elimu bure
Kuhusu kuajir walmu kutokan na uhaba.
Mbona nimefafanua mkuu au hiki kipengele hapa chini hujakisoma?

Hii yote ni kwasababu serikali inatumia gharama kubwa zaidi ya billions 20 kwa mwezi kuhudumia elimu bure na hivyo kupunguza kiwango cha bajeti cha kuajiri walimu wapya kwa mwaka.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,558
2,000
Prioritisation! Vipaumbele!

Serikali hii imejitwisha mizigo mizito sana. Kufanya miradi mikubwa kama Stieglers Gorge HP, SGR na kununua ndege kwa cash - kwa pesa za ndani - HALAFU utoe elimu bure hadi sekondari -KWA MPIGO ni mzigo ambao uchumi tulio nao hauwezi kuhimili. Kudai nchi ni tajiri; ina hela nyingi sana zilizokuwa zinaishia kwa mafisadi ni KUJIDANGANYA. Sio kihivyo.

Hapo ndipo umuhimu wa kushirikisha taasisi zote muhimu unapoonekana. Wizara ya ya Uchumi na Fedha/Tume ya Pipango, Benki Kuu, Bunge na Kamati zake n.k. vyote vilipaswa kutumika (properly engaged) kubainisha yanayowezekana (feasible) ili kutekeleza sera na ahadi kulingana na uharaka wa mahitaji na rasilimali (fedha/wataalamu) zilizopo. Kudharau mfumo ni kuingia gizani na kujiletea maumivu yasiyo na sababu.

Kila mara humu ndani nasema serikali hii haina uwezo wa kujenga miradi miwili ya zaidi ya 15t kwa wakati mmoja, kisha ikafanikiwa kuimaliza ndani ya miaka 10. Kwa bahati mbaya tuna bunge linalosimamiwa na serikali na sio kinyume chake. Kwa sasa serikali imekwama ndio maana zinaanza kutoka amri za kupanick kuhusu makusanyo ya pesa.

Ameachwa mtu mmoja kuamua bila kuwa na uwezekano wowote wa kumdhibiti. Hakukuwa na umuhimu wowote wa kununua ndege kubwa tena kwa cash. Kama ilitakiwa tununue ndege, basi ilitakiwa ziwe ni ndege ndogo ndogo za humu ndani tu, tena kwa mkopo. Pia hakukuwa na sababu ya kuweka $6.5b kwenye mradi wa SG. Wangalau tungeweka $2 kwenye umeme wa gas, kisha tuongeze kadiri muda unavyokwenda. Kwenye mradi wa SGR, tayari JK aliacha akiwa ameshakubaliana na wachina wajenge hiyo reli. Kwasasa tumekwama tumeishia kurudi hukohuko kwa wachina!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom