Serikali ishitakiwe kwa upotoshaji huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ishitakiwe kwa upotoshaji huu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ntemi Kazwile, Jan 2, 2012.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna tangazo la dawa mseto, ujumbe unaotolewa kwenye tangazo hili ni kuwa sasa mwanachi anachangia shilingi elufu moja tu kupata dawa hii kwa sababu gharama halisi imelipwa na serikali, ndani ya tangazo hilo hilo kuna ujumbe kuwa tangazo hilo limeletwa kwenu kwa hisani ya watu wa Marekani, badala ya serikali ya Marekani.

  Nina uhakika kuwa matumizi ya neno "watu wa Marekani" ni ya muhimu vinginevyo walipa kodi wa Marekani wangeliishitaki serikali yao lakini linapokuja suala la Tanzania linatumika neno "serikali" kama kwamba serikali haipati pesa kutoka kwa watu wake...

  Tanganzo hili linanikwaza sana mimi kama mlipa kodi kwani ni upotoshaji mkubwa sana kusema kuwa gharama zimelipiwa na serikali kwani hizo ni kodi zetu na tunatakiwa tutajwe kama walipa kodi tunaoiwezesha serikali kulipia gharama hizi, kama ambavyo walipa kodi wa Marekani wanatajwa badala ya serikali ya Marekani..

  Ninaomba kuwasilisha!
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Tupate common definition ya serikali, then kutokea hapo tuta-conclude kama tangazo hilo ni sahihi au vipi!
   
 3. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Mi nilifikiri inakuuma nchi kama Tanzania "kulipiwa" dawa kumbe ni jinsi walivyoandika.......mmh!! ukombozi bado sana
   
Loading...