rr4
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 3,969
- 5,898
Ni muda mrefu nimewaza sana hii kitu na nikafikia hitimisho kuwa kama Serikali haitaweka mkono wake kwenye sekta hii kikamilifu, hii sekta itaendelea kudidimia kila siku badala ya kuchanua na kuwa mkombozi.
Sekta hii ni muhimu sana katika kuchachua uchumi wa wananchi wa kawaida sana ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi kupata mikopo kwenye mabenki makubwa aidha kwakua hawana dhamana au biashara ni ndogo sana mfano muuza maandazi.
Sekta hii inajitolea sana kukuza uchumi hasa wa akina mama ambao ndio wapambanaji wakubwa hapa nchini na wenye dhamana ya kuhakikisha familia inakula na wakusoma wanasoma.
Tatizo ni kuwa Serikali imeichukulia poa sana hii sekta na kuiacha ipambane yenyewe.
1. Watu wanachukua mikopo na kukimbia tu miji yao.
2. Wengine wanachukua mikopo na kuamua tu wasilipe.
3. Wengine wanachukua mikopo na biashara aidha zinakufa au kuharamishwa tu na Serikali maana sio biashara rasmi mfano wamachinga.
Serikali ingeitambua hii sekta na kuikumbatia vizuri kwa kuhakikisha:
1. Elimu ya mikopo na ujasiriamali inatolewa toka darasa la kwanza mpaka chuo kikuu. Watanzania wengi hawana elimu ya ujasiriamali na mikopo na hawajui namna ya kutumia mikopo, mara nyingi mikopo inawaangusha zaidi kuliko kuwanyanyua na hii ni kutoka na Serikali kufanya uzembe wa kushindwa kutengeneza mtaala wa kuwafundisha raia wake umuhimu wa mikopo katika ujasiriamali.
2. Sheria kali za kuwabana wakopaji zitungwe. Kule Ethiopia, mtu akikopa kwenye Mirofinance akishindwa kurejesha basi anapelekwa na Serikali kufanya kazi mfano za Ujenzi wa barabara au majengo na kipato chake kinakwenda moja kwa moja kwa mdai wake.
3. Serikali iweke miundo mbinu mizuri kwa wafanyabiashara ndogondogo ili wasiwe watu wa kuhama hama.
4. Suala la hati za viwanja lipewe uzito na viwanja vipimwe vyote nchi nzima. Kule Uganda imefikia mahala mtu aanaweza kuwa na hati tatu kwenye kiwanja kimoja. Unakuta ana hati ya eneo nyumba ilipojengwa, hati ya eneo choo kilipojengwa na hati ya eneo jiko lilipojengwa. Hii itasaidia hizi Microfinance Institutions kuweza kuwa na hizi hati kama Collateral. Saa hizi mtu anaweka vimakochi, tz, subwoofer na vi-collateral vingine vilivyochoka.
5. Mtu akishindwa kulipa sheria itungwe achukuliwe kama mhalifu wa jinai na afanye kama namba. 2
Serikali ikishikamana vizuri kwenye hili, kwakweli itaweza kuchachua au kuzimua uchumi wetu huu.