Serikali irahisishe masharti utoaji vibali dawa za asili`

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
Serikali imeshauriwa kurahisisha mazingira ya utoaji wa vibali kwa wagunduzi wa tiba za asili ili kuwepo uwazi katika uuzaji na matumizi yake.
Hayo yalisemwa jana na Danny Kyauka, mgunduzi wa dawa ya asili ya billyd fomula power, anayodai kuwa inatibu ugonjwa wa figo.
Kyauka alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari (Maelezo), jijini Dar es Salaam jana.
Alisema mazingira yaliyopo sasa yanatawaliwa na ukiritimba unaowafanya wagunduzi na waganga wa tiba za asili, kutoa huduma zao kwa njia za kificho.
Kyauka alitoa mfano kuwa, mamlaka husika serikalini, haijampatia kibali kwa ajili ya kuuza dawa hiyo, hivyo kumfanya aendelee kuitumia kwa wateja wake katika mazingira ya kificho.



CHANZO: NIPASHE
 
ndo uganga wa kienyeji huo...selikali inatakiwa kufuta wote lasivyo, si muda mrefu utasikia hao hao wanaopewa vibali wanatafuta kichwa cha wmanasiasa ili wakiuze kwa mgombea...shauri lao...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom