Mwanapropaganda
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 4,235
- 2,505
Sasa hivi suala la mabinti wengi kuzaa limekuwa kama mtindo wa kisasa(fashion).
Katika mambo yanayochangia umaskini na kuzorota kwa maadili kwenye jamii ni hili la watoto wengi kutopata malezi stahiki kutoka kwa wazazi wao.
Nimeona kwa sasa mabinti wadogo wanazaa tu bila utaratibu wala mipango kwa maslahi ya maendeleo ya mtoto siku za mbeleni. Vijana wanaowapa mimba hizo hutokomea na kuacha jukumu lao kuwa kama mzigo wa wenhgine, hivyo watu wengine wanajikuta wakilazimika kuwatunza watoto hao pasipo kitegemea.
Leo ukipita kwenye mitaa na kuona watoto wanaoishi mazingira magumu, wengi wao wametokana na hili ninalosema hapa.
Wito wangu kwa serikali ni kupiga marufuku watu kuzaa kabla ya ndoa na vile vile kuhakikisha hakuna atakayezaa nje ya ndoa ili kuwafanya watoto wapate malezi stahiki, hatua hiyo itapunguza vijana wa mitaani ambao wengi wao huishia kujiingiza kwenye magenge ya uharifu na matumizi ya dawa za kulevya.
Migogoro kwenye ndoa inayosabanishwa na tuhuma za kuzaa nje ya ndoa zinasababisha watoto kukataliwa na hatimaye kuathiriks kisaikolojia.
Serikali itamke wazi kwamba, kuzaa nje/kabla ya ndoa ni jinai, vile vile kuhakikisha watoto wote wanapata huduma za lazima kutoka kwa wazazi wao.