Serikali ingilieni kati, "Mummians" wanamaliza watu Morogoro vijijini

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,673
1,571
Nimetoka rikizo Matombo kata ya kibungo juu kijiji cha Nyingwa. Hali ni mbaya kwa wakazi wa huko na wanahitaji msaada wa haraka kwani wanaangamia.
Kuna watu wanaitwa mummians kwa lugha ya kigeni au nyonya damu kwa kiswahili na wenyeji wanawaita "machinja". Watu hawa hukamata wanakijiji kwa nguvu na kuwanyonya damu yote mpaka kufa. watu hao wanafahamika kijijini lakini hawachukuliwi hatua yoyote kwa nadai ya kwanba wametumwa na serikali kutafuta damu kwa ajili ya hospitali.
Nimekaa wiki mbili takribani watu wawili wamekufa na kijana mmoja kanusurika kufa kutokana na mummians hao.
WITO WANGU;
Serikali iingilie kati kukomesha mauaji haya kwa kuwa ninaamini serikali haijawatuma wala kiwaagiza wauwaji hawa.
Ama itoe tamko la kukubali kuwaagaiza wauwaji hawa.
Nitakuwa tayari kumtaja hata bosi wao anayeongoza genge hili la wauwaji katika wilaya ya Morogoro v.
 
kwani mambo ya nyonya damu yana ukweli wowote au ni hadithi za watoto tu?
 
Kalalambe bado yupo? Mzee Winga naye bado yupo? Hao watu walisakamwa sana kuwa ni chinjachinja kwenye miaka ya 70 hadi 90. Mkuu TAWA vihi hausindile, gwe ntowele au PM tulonge. Ayo munu yowakoma twaga jake nani?
 
Jamani habari hiyo ni kweli ipo. Mimi ninaishi matombo ila wazazi wangu wanaishi eneo linaitwa Lukenge. Habari hii ni ya ukweli kabisa
 
Kalalambe bado yupo? Mzee Winga naye bado yupo? Hao watu walisakamwa sana kuwa ni chinjachinja kwenye miaka ya 70 hadi 90. Mkuu TAWA vihi hausindile, gwe ntowele au PM tulonge. Ayo munu yowakoma twaga jake nani?
Kwa sasa kuna mtu anaitwa KIKWATO mwenyeji wa Lumba mzaliwa wa kienzema, ndiye bosi wa hao watu.
 
Kalalambe bado yupo? Mzee Winga naye bado yupo? Hao watu walisakamwa sana kuwa ni chinjachinja kwenye miaka ya 70 hadi 90. Mkuu TAWA vihi hausindile, gwe ntowele au PM tulonge. Ayo munu yowakoma twaga jake nani?

Dah! Huyo Kalalambe enzi hizo nipo mdogo hadithi zake nilisikia sna.
Alikuwa si mchezo.
 
Sasa nyinyi mnawajua hao watu mnashindwa kuwapiga kibiriti? Haiwezekani kakundi ka wahalifu wa maisha ya binadamu kijiji kizima mshindwe kukadhibiti na kukatokomeza, chukueni mikuki, mishale, nyundo, mapanga, visu, magobole, vibiriti, baruti na mambwa vamieni hayo mapori yote atakayetokea hamumuelewi tumieni vifaa mlivyobeba. Ilishawahi kuzungumzwa vijiji nilivyotokea miaka ya 1999 mbona tulifanya msako wa mapori yote na tulianza kutambua raia wa vijiji vyote vinavyotuzunguka then tukatoa tahadhari kwa kila raia asikanyage porini kwa mwezi mmoja tunafanya operation tokomeza, hatukuwahi kusikia hizo nyimbo tena, kama walikuwepo basi hawakuwahi kusikika tena.
 
Back
Top Bottom