Serikali ingepiga marufuku export ya Mkaa nje..

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,884
Nchi kama India washapiga marufuku siku nyingi ku export mkaa nje ya nchi
Tanzania inaathirika mno kimazingira kwa kutokupiga marufuku kuuza mkaa nje ya nchi
mkaa wa Tanzania ambao nimatokeo ya kuchoma misitu mna miti pori unauzwa
Uarabuni,commoro na UK na Europe kwa ujumla kwa wingi kupitia Kenya na Somalia

Washauri wa Rais na viongozi wengine tuiokoe nchi na uharibifu wa mazingira kwa kuzuia mkaa
kuuzwa nje.

Nchi inayofaidika zaidi na biashara hii ni Kenya ikifuatiwa na Somalia
 
kuna mkaa unavushwa bagamoyo kwenda zanzibar nafikiri huko ndio wanapitishia zaidi kwenda nje lakini hapa ukibeba gunia mbili tatu za matumizi wanakusumbua sana
 
Ni biashara kubwa sana kuliko unavyoweza kudhania..
kuna wasomali mamilionea kwa mkaa wa TZ wanapeleka Europe

Nami ndio nasikia leo. Zile check points zote za maliasili bado watu wanaweza kufanya biashara ya mkaa kuwa kubwa kiasi hiki? Kazi nzuri kuibua hii 'inshu'.

Hebu weka facts zaidi au mfano wa nani na wapi hiyo biashara imeshamiri.
 
kuna mkaa unavushwa bagamoyo kwenda zanzibar nafikiri huko ndio wanapitishia zaidi kwenda nje lakini hapa ukibeba gunia mbili tatu za matumizi wanakusumbua sana

huo unaenda Comoros na Dubai...na kwingine
ni biashara ya mabilioni ya shillingi
 
Nami ndio nasikia leo. Zile check points zote za maliasili bado watu wanaweza kufanya biashara ya mkaa kuwa kubwa kiasi hiki? Kazi nzuri kuibua hii 'inshu'.

Hebu weka facts zaidi au mfano wa nani na wapi hiyo biashara imeshamiri.

Kenya ndo loophole kubwa ya biashara za mbao na mkaa
mradi sio illegal..loopholes ni nyingi sana
vibali vinafojiwa na kuzidishiwa viwango kienyeji
dawa ni kupiga marufuku tu kupeleka mkaa nje hasa Kenya
 
ipige marufuku? hiyo biashara inafanyika kinyemela au imeruhusiwa kabisa? serikali yetu ni ya kijinga kiasi cha kuruhusu mkaa uuzwe nje karne hii kweli?
 
Kenya ndo loophole kubwa ya biashara za mbao na mkaa
mradi sio illegal..loopholes ni nyingi sana
vibali vinafojiwa na kuzidishiwa viwango kienyeji
dawa ni kupiga marufuku tu kupeleka mkaa nje hasa Kenya

Bila shaka Magufuli atapita hapa ID yake sijui ni ipi nimtag. Kwa sasa hakuna kinalofanyika hadi mkulu aliweke kwenye spotlight.

Ilikua hivi hivi kwenye biashara ya Tanzanite, zilikuwa smuggled nchi jiraji na India wakawa wauzaji wakuu.
 
hiyo biashara inafanyika kinyemela au imeruhusiwa kabisa? serikali yetu ni ya kijinga kiasi cha kuruhusu mkaa uuzwe nje kweli?

Lini ulisikia ni marufuku? wao si wanauliza vibali?
Kupeleka Kenya huwa haionekani kama tunapeleka nje
Kenya ndo wanapeleka hadi Europe..
Kuna article nimesoma sehemu ngoja nikipa link ntaweka hapa
 
Kenya mbona nilisikia kusafirisha tu mkaa kutoka kaunti moja kwenda nyingine ni marufuku achilia mbali nje ya nchi? Ulaya wanafanyia nini mkaa anyway, kuchomea nyama?
 
Isee! Sijawahi kufikiri kama Tuna export mkaa nje ya nchi yani kelele zote zinazo pigwa kuhusu mazingira kumbe bado serikali inaruhusu mkaa usafirishwe nje
 
Nchi kama India washapiga marufuku siku nyingi ku export mkaa nje ya nchi
Tanzania inaathirika mno kimazingira kwa kutokupiga marufuku kuuza mkaa nje ya nchi
mkaa wa Tanzania ambao nimatokeo ya kuchoma misitu mna miti pori unauzwa
Uarabuni,commoro na UK na Europe kwa ujumla kwa wingi kupitia Kenya na Somalia

Washauri wa Rais na viongozi wengine tuiokoe nchi na uharibifu wa mazingira kwa kuzuia mkaa
kuuzwa nje.

Nchi inayofaidika zaidi na biashara hii ni Kenya ikifuatiwa na Somalia
Ila watoe vibali kwa mtu yeyote tena bila ushuru au kodi yoyote kwa watu wanaoingiza mkaa ndani ya nchi
 
Kenya mbona nilisikia kusafirisha tu mkaa kutoka kaunti moja kwenda nyingine ni marufuku achilia mbali nje ya nchi? Ulaya wanafanyia nini mkaa anyway, kuchomea nyama?
kuchomea nyama? duh
hebu soma hii ya mkaa wa Nigeria unavyoplekwa Ujerumani ushangae
 
Sio mkaa wote ni zao la misitu asili mfano Njombe kuna miti inalimwa kwa wingi sana inaitwa miwati (milingo) inatumika kuzalisha mkaa, kiwi na lami
 
Back
Top Bottom