Katika mikutano yote niliyoenda na kuona kwenye TV, nimeshuhudia watu wakivalia sare za vyama vyao kwa maelfu. CCM wametia fora. Hii imenipa imani kuwa serikali inaweza kugawa uniform na kutoa elimu bila ada kama wagomea wengi au wote walivoahidi. Ukichukua hela zilizotumika kujaza viwanja na zile nauli na usumbufu wa kukaa kwenye jua + lunch, hizi pesa zinatosha kulipa madai ya walimu na kumaliza mgogoro wa walimu na serikali.
Sasa nauliza, huwa tunashindwa wapi? Ni nani mchawi wetu? Ewe Mungu ebu tuongoze tumlete mja wako, atakaye weza kutatua matatizo haya ambayo ni matatizo ya kutengezwa na binadamu kwa kukosa maono. Tupe kiongozi mwenye maono.