Serikali inavyochangia kuua elimu

Serikali inavyochangia kuua elimu

shikulaushinye

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2014
Posts
828
Reaction score
456
Kwa muda mrefu, elimu ya Tanzania imekuwa ikishuka hasa masomo ya sayansi na hisabati. Binafsi nina mtoto anayesoma shule chekechea ktk shule moja hapa Tanzania, huwa ninakaa na mtoto kuangalia maendeleo yake, siku moja katika kukagua daftari za mtoto.

Nilipigwa swali na mtoto, swali lenyewe lilikuwa nimtajie aina za insects, basi nikamtajia akanikumbusha kuwa nimesahau Snake na Frog, yaani nyoka na chura. Nikamwambia hao siyo insects, basi akakataa akanilitea kitabu kweli kitabu mtunzi kaandika snake yaani nyoka na chura wapo katika kundi la insects. ilikuwa kazi sana kumfanya aaache kuamini alichofundishwa na Mwalimu wake kupitia kitabu hiki.

Inashangaza sana hata walimu wana copy na paste bila kungalia kama kitabu kimeandikwa sahihi, hii ina maana hata uwezo wa walimu wetu ni mdogo na ndiyo chanzo cha kukosa wataalamu katika Sayansi na Hisabati.

Watanzania wenzangu, hii elimu huria ni tatizo. Serikali imeachia kila kitu, mbaya zaidi, serikali kupitia wizara wa Elimu na ufundi imekuwa ikitoa baraka kutumika vitabu hivi bila hata kuangalia madhara kwa jamii ya Watanzania.

Kwa lengo la kutoa ujembe na kuikumbusha serikali yetu, kuviangalia vitabu vinavyotumika mashuleni basi nimeweka baadhi ya kurasa za kitabu, mtunzi na jina. Pia nimefanya utafiti mdogo kitabu hiki kinatumiwa na shule nyingi za English medium hapa Tanzania. Hivyo watoto wengi wamemezeshwa sumu kupitia kitabu hiki.

Pili: wale wataalamu wa Elimu tunaomba mtusaidie hivi ni sahihi mtoto wa chekechea/KG umri wa miaka 4-5 kufundishwa mambo mazito kama haya wakati hata kusoma bado wanajifunza? Darasa la kwanza watasoma mambo gani iwapo kg wanasoma mambo kama haya?

Insects.jpg Cover pg.jpg Mtunzi.jpg Table of content.jpg Cover pg.jpg
 
Attachments

  • IMAG1556.jpg
    IMAG1556.jpg
    163.2 KB · Views: 124
Tumekupata hiyo ni BRN unashangaa nn sasa,tupatie mchango wako tuboreshe.
 
Duh kweli mkuu watoto wetu, wadogo zetu wanapewa elimu mbaya sana, yaani nyoka, chura na kenge wote ni insects?
Na kitabu kimeruhusiwa kutumika!!! Serikalini watu wanaangalia matumbo yao tu
 
Mkuu pole sana, inasikitisha kwamba waandishi wa vitabu hivyo nao ni Watanzania waliopewa elimu duni. Inasikitisha pia vitabu havikaguliwi na mamlaka husika. Inasikitisha kwamba mchapishaji nae anachapisha kama zuzu tu.

The whole system is a big joke.
 
Tumekupata hiyo ni BRN unashangaa nn sasa,tupatie mchango wako tuboreshe.

Tunatofautiana kuelewa yawezekana hata hujui nilichoandika kina maana gani, nikibishana na wewe ni sawa na kumpigia gitaa mbuzi.
 
Ndo mnatakiwa Kuwaheshimu walimu kwani nguvu wanayotumia ni tofauti na nguvu ya mtu atumiaye silaha ana uwezo wa kuliangamiza Taifa!!
Walimu waheshimiwe kama kada zingine kwa kupewa stahiki zake!
 
Walimu tunawaheshimi sana, wanadharauliwa na Serikali yoa. Uilwahi kisikia wabunge na mawaziri wakidai malimbikizo ya madai?
 
Iki google ni kama mtunzi ni mganda, inawezekana ni kwa sababu Watanzania hatutungi vitabu.
 
Kwa muda mrefu, elimu ya Tanzania imekuwa ikishuka hasa masomo ya sayansi na hisabati. Binafsi nina mtoto anayesoma shule chekechea ktk shule moja hapa Tanzania, huwa ninakaa na mtoto kuangalia maendeleo yake, siku moja katika kukagua daftari za mtoto.

Nilipigwa swali na mtoto, swali lenyewe lilikuwa nimtajie aina za insects, basi nikamtajia akanikumbusha kuwa nimesahau Snake na Frog, yaani nyoka na chura. Nikamwambia hao siyo insects, basi akakataa akanilitea kitabu kweli kitabu mtunzi kaandika snake yaani nyoka na chura wapo katika kundi la insects. ilikuwa kazi sana kumfanya aaache kuamini alichofundishwa na Mwalimu wake kupitia kitabu hiki.

Inashangaza sana hata walimu wana copy na paste bila kungalia kama kitabu kimeandikwa sahihi, hii ina maana hata uwezo wa walimu wetu ni mdogo na ndiyo chanzo cha kukosa wataalamu katika Sayansi na Hisabati.

Watanzania wenzangu, hii elimu huria ni tatizo. Serikali imeachia kila kitu, mbaya zaidi, serikali kupitia wizara wa Elimu na ufundi imekuwa ikitoa baraka kutumika vitabu hivi bila hata kuangalia madhara kwa jamii ya Watanzania.

Kwa lengo la kutoa ujembe na kuikumbusha serikali yetu, kuviangalia vitabu vinavyotumika mashuleni basi nimeweka baadhi ya kurasa za kitabu, mtunzi na jina. Pia nimefanya utafiti mdogo kitabu hiki kinatumiwa na shule nyingi za English medium hapa Tanzania. Hivyo watoto wengi wamemezeshwa sumu kupitia kitabu hiki.

Pili: wale wataalamu wa Elimu tunaomba mtusaidie hivi ni sahihi mtoto wa chekechea/KG umri wa miaka 4-5 kufundishwa mambo mazito kama haya wakati hata kusoma bado wanajifunza? Darasa la kwanza watasoma mambo gani iwapo kg wanasoma mambo kama haya?

View attachment 251686 View attachment 251695 View attachment 251696 View attachment 251697 View attachment 251695

Suala hilo la vitabu vitakavyotumika katika shule za msingi na sekondari nchini sasa limepatiwa tiba na Rais WA Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, ambapo alizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, katika shule ya sekondari ya Majani ya Chai, Dar es salaam, Februari 13, 2015

Ndiyo maana Mhe. Rais katika hotuba yake ya alisema Sera mpya ya 2014 inaelekeza kutumika kwa utaratibu wa kila somo kuwa na kitabu kimoja kwa shule zote badala ya utaratibu wa awali wa kila shule kuwa na kitabu chake.

Rais alisema walimu ni wadau wenye wajibu wa kipekee sana. Jukumu lao la kuwafumbua macho na kuwaongezea upeo wa ufahamu wa vijana wetu pamoja na kuwandaa kuwa raia wema halina mfano wake.

“Halina badala yake. Mnafanya kazi nzuri lakini mnatakiwa kufanya vizuri zaidi leo na siku za usoni. Elimu ni kitu chenye unyumbufu mkubwa na mabadiliko mengi na hasa siku hizi. Lazima muende na wakati.

Ni ninyi waalimu, pengine kuliko watu wengi wengine mtakaoumba Tanzania ya kesho iliyo bora kupitia elimu mnayowapa wanafunzi. Ninyi walimu ndiyo wa kutusaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii na nchi yetu. Nawaomba sana muendelee kujizatiti katika kutambua uzito wa majukumu yenu na kuyatekeleza. Sisi Serikalini tutaendelea kufanya kila lililo katika uwezo wetu kuboresha maslahi yenu na mazingira yenu ya kazi” alisema Mhe. Rais Kikwete.
 
Sidhani kama unaelewa kinachoendele mashuleni na wanachotendewa walimu. Tatizo la serikali yetu ni kuendekeza siasa kwa mambo ya msingi. Kila leo zinazinduliwa sera ambazo hazitekelezeki.
 
Walimu wana kazi ngumu sana, serikali imeacha elimu iwe hulia, kila mwenye ka shule anaweza kutunga kakitabu na akasema hicho ndicho pekee kitumike kwenye shule yake/zake. hivyo kila mzazi atatakiwa kununua hicho kitabu kwa matumizi ya mtoto, pai mwajiliwa ambaye ni mwalimu akiuliza kuhusu kitabu hicho anaweza kupoteza kazi yake. hivyo inabidi akitumie tu kitabu japo anaona mapungufu.
 
Asante mleta mada kwa kuonesha ushahidi. Aliyeandika kitabu hicho sidhani Kama hajui wadudu na sifa zao. Swali tujiulize ilikuwaje ikawa kama ilivyo? Kuna tatizo mahali fulani!!
Kwa mantiki hiyo siwezi kuilaumu serikali, kwa sababu chache tu :je, kitabu hicho kimeidhinishwa na serikali kwamba kitumike kufundishia?
Je, hatufukiri kuwa mwalimu anayetumia kitabu hicho anaweza kuwa amekinunua mtaani kama ambavyo wewe na mimi tunapita mtaani kuwanunulia watoto wetu vitabu ili wajifunze?
Ushauri :walimu wanapaswa kujua kuwa kuna tatizo katika hivi vitabu hivyo wachambue kwanza haya maarifa, yanayofaa ndiyo wawafundishe watoto.
 
Back
Top Bottom