Serikali inavyo piga marufuku shamrashamra za Pasaka, hawakuona kelele mule Bungeni?

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Wakuu hebu tujadili hili.

Serikali imetoa wito kutoskia shamrashamra za sikukuu ya Pasaka mwaka huu tofauti na miaka mingine kisa bado tupo kwenye maombolezo.

Je, Swali kwa Serikali inamaana hawakuona zile kelele na shamrashamra Bungeni baada ya jina la Philipo Isdor Mpango kupendekezwa na mama Samia?

Yaani wao walisherekea Jina tu, je sisi swala la kidini kwa nini waingilie kati.

Tuchangie mawazo wanandugu
 
Na mi nimeshangaa yani wao wawe huru kusheherekea furaha zao kwa kupata vyeo halafu kupitia hivyo vyeo wakataze waumini wasisheherekee eti kisa msiba wa wiki mbili zilizopita
 
First things first, kwa nini ni lazima tusherehekee pasaka?

Tunasherehekea bwana kusulubiwa ?
 
Na mi nimeshangaa yani wao wawe huru kusheherekea furaha zao kwa kupata vyeo halafu kupitia hivyo vyeo wakataze waumini wasisheherekee eti kisa msiba wa wiki mbili zilizopita
huu ukandamizaji wa kiwango cha lami
 
Wale wajuba wa mbeya waliochinja mbuzi walikua wanatimiza andiko ila mamwela waliowadaka inaonekana walikua wapagani
Yaani serikali inahangaishana na watu kwenye mambo ya imani.
Ndo maana msibani watu hula sasa sijui iliwakamata kwa nini
 
First things first, kwa nini ni lazima tusherehekee pasaka?

Tunasherehekea bwana kusulubiwa ?
Kuwe na hoja yenye mashiko kwenye hili sio zisisheherekewe eti kisa msiba ambao tumeshaanza kusahau
 
First things first, kwa nini ni lazima tusherehekee pasaka?

Tunasherehekea bwana kusulubiwa ?
Ndio, maana bila yeye kukubali kusulibiwa tusingepata wokovu. Kwa hiyo kifo cha Yesu ni furaha kubwa kwa wenye dhambi na waliofungwa na kila aina ya uonevu wa shetani - ni UKOMBOZI!!
 
Wakuu hebu tujadili hili.
Serikali imetoa wito kutoskia shamrashamra za sikuku ya pasaka mwaka huu tofauti na miaka mingine kisa bado tupo kwenye maombolezo.
Je, Swali kwa serikali inamaana hawakuona zile kelele na shamrashamra Bungeni baada ya jina la Philipo Isdor Mpango kupendekezwa na mama Samia?.
Yaani wao walisherekea Jina tu, je sisi swala la kidini kwa nini waingilie kati.

Tuchangie mawazo wanandugu
KIBURI CHA FARAO kina mwisho wake, mapigo 10 tu atakaa chini.
 
Back
Top Bottom