Mimi kama Mtanzania nasikitishwa na viongozi wetu wa serikali na watunga sheria kwa ujumla.
Kodi za Magari ambazo Watanzania wengi wanalipa wanapotoa magari nje si za msingi na hazijafikiriwa kitaalamu. Kwa sasa kuna watu wanalipa kodi zaidi ya 50% ya gharama ya gari. Hizi hapa ni faida za gari kuingia Tanzania kwenye uchumi wetu.
1. Mafuta: Gari itaweka mafuta ili kutembea na kwenye mafuta kuna kodi, kunampa biashara gas station ambayo inatoa ajira na kulipa kodi, ujenzi wa gas station unasaidia kampuni za cement kama twiga, magari ya kubeba mafuta yanapata kazi, bank zinapata pesa kutokana na mikopo na biashara na zinaajiri, tanesco inapata pesa za umeme wa kusukuma mafuta n.k.
2. Maisha: Magari yanaraishisha maisha na kufanya shughuli ziweze kufanyika kwa haraka zaidi. Inaongeza "Productivity", magari yanasaidia kwenye maafa, kusafirisha abiria kama taxi, kwenye sehemu za mbali kama vijijini, kufanya biashara kama za utalii, ulizi, kubeba wagojwa.
3. Vipuli: Magari yana kaa zaidi ya miaka kumi kwa muda huo yatanunuliwa vipuli vya utengenezaji, maduka ya vipuli yatalipa kodi na kuajiri, vijana watapata kazi za ufundi, serikali itapata kodi ya uingizaji wa vipuli, viwanda vitatengenezwa n.k hii ni kwenye vipuli tu.
4.Matari: Magari yanahitaji matairi hivyo maduka ya matairi yatauza na kulipa kodi, vijana watapata kazi kwenye kampuni hizi, mabaki ya matairi yatatumika kwenye shughuli nyingine na serikali itafaidika.
5. Utengenezaji: Kampuni za utengenezaji kama kupiga rangi zinafanya biashara na kulipa kodi, zitaajiri, zitaagiza au kununua rangi na kulipia kodi n.k
Hizi ni faidi chache tu za kuingiza gari. sasa je serikali ikipunguza kodi na iwe kama nchi nyingine 8%-10% watapata hasara gari ukilinganisha na watu kuacha kabisa kuingiza magari??. Kama serikali itaanza kuingiza kodi kwenye magari ya mizigo na magari ya ujenzi itakuwa hasara kubwa kwa nchi. Tatizo la viongozi wetu ni kwamba wakiona vitu vinaongezeka kidogo wanakimbilia kuweko kodi wakithani kwamba vitu vitaongezeka tu bila kujali athari za uchumi.