Serikali inapowakatili raia wake kodi za kuingiza magari: Nini kifanyike?

Dawa ya serikali ya magamba ni kubadilisha plate number. Magari yote kuanzia 2015 yaanze kusomeka T 2015 CDM hapo ndipo adabu itapatikana
 
Mkuu hii ni ngumu kwani utaratibu unapata exemption after 5 years sasa hili la kila mwaka linakujaje?? in addition pale TRA kila kitu kiko controlled kwenye compyuter na TIN no inayotumika ni moja ambayo mtumishi wa umma anaitumia kulipia kodi kila mwezi...

Upo wapi wewe?Watu wanatumia majina ya watu wengine amabao ni wafanyakazi kuingiza magari!
 
Mkuu hii ni ngumu kwani utaratibu unapata exemption after 5 years sasa hili la kila mwaka linakujaje?? in addition pale TRA kila kitu kiko controlled kwenye compyuter na TIN no inayotumika ni moja ambayo mtumishi wa umma anaitumia kulipia kodi kila mwezi...
Mkirua exemption kwa mashirika ya dini si kila baada ya miaka 5 ila wanapokuwa na miradi mipya ikipitia ngazi husika (Wilayani na Mkoani kisha wizarani) basi unapata exemption. Ukweli ni kwamba kuna watu wengi wanaifaidi hiyo exemption na serikali inawafahamu badala ya kuwashuhulikia wao tu inaumiza wananchi wote kama kwenye swala la mafuta ya taa...!
 
Upo wapi wewe?Watu wanatumia majina ya watu wengine amabao ni wafanyakazi kuingiza magari!
Nipo Dar es Salaam... Soma hoja niliyoijibu then urudi kuuliza swali lako hapa kwasababu unachokisema wewe ni tofauti na nilichokifafanua.
 
Ni mada nzuri. Rekebisha mwaka 20012 bado sana kufikia. Umerudia ndani na kwenye heading. Napita tu
 
Kwani ukiwa mfanyakazi lazima ununue gari? kama umefikia kiwango cha kumiliki gari basi pesa unazo lipia kodi, badala ya kulilia bei ya mchele au unga iwe chini maana ndio uhakika wa maisha ya kila siku.
Kama vipi nunua punda kwani na yeye analipishwa kodi?

Ukipunguza bei ya mchele na sembe, umemuua mkulima!
 
Kwani ukiwa mfanyakazi lazima ununue gari? kama umefikia kiwango cha kumiliki gari basi pesa unazo lipia kodi, badala ya kulilia bei ya mchele au unga iwe chini maana ndio uhakika wa maisha ya kila siku.
Kama vipi nunua punda kwani na yeye analipishwa kodi?

You are so hush....Lol
 
Jamani wanajf,


Nimekuwa nafuatilia baadhi kodi zilizopandishwa kwenye bajeti ya serikali mwaka huu. Cha ajabu ni kuwa kodi hizi hasa hili la kwenye magari na umri wa magari ya kuingiza nchini si tu ni kero bali ni kuua ari ya watanzania wanaojiinua kiuchumi na kibiashara. Kitendo hichi ni kinyume kabisa na mwenendo wa serikali yenyewe ambayo EWURA kwa mfano wanapotangaza bei mpya basi makampuni yanapewa grace period zimalize stock iliyopo ndani. Katika hili utangua serikali yetu inawajali matajiri kuliko watanzania walio wengi – maskini wanaotaka kujikomboa.


Fikiria mtanzania aliyeamua kufuata sheria iliyokuwepo kabla ya July inayotaka mtu kuagiza isiyozidi miaka kumi ili asilipishwe dumping fees. Sasa ni watu wengi wameagiza magari yao tena kwa kukopa ili wakaanzishie biashara zao. Kwa bahati mbaya serikali imebadili mwaka wa kuingiza bila dumping fees uwe 8 years. Bila kujali sasa serikali inataka wote ambao gari zao zitaingia baada ya mwezi Julai kulipa dumping fees. Hii ina maana mtu aliyetarajia kulipa labda 1,800,000 kama kodi sasa atalipa karibu million 5 kama kodi tu. Kwa mujibu wa makampuni mbalimbali yanayotoa magari bandarini watu wengine watalipa kodi mpaka kufikia million kumi na sita. Hii ni sawa na kununua gari lingine nzuri tu tena bila ya kodi ya uchakavu.


Cha ajabu watanzania ni kuwa hizi kodi zimeanza kulipishwa wakati hata finance bill haikupitishwa na bunge. Finance bill ilikataliwa bungeni kama sikosei na sasa inategemewa kuwasilishwa mwezi wa nane. Je, wabunge wetu hili mnalionaje? Kwani msiiamuru serikali isilipishe wale wote walionunua magari yao kabla ya mabadiliko ya sheria? Ni wazi kuwa siyo kosa kubadili sheria, lakini siyo kuwalazimisha watu gharama ambazo hawakuyapanga. Huu ni uhuni wa hali juu kabisa wa kuwafanya watanzania maskini waendelee kuwa maskini na kuwaacha wenye fedha waendelee kuifaidi nchi kwani ndo wanaweza kukwepa kodi na kumiliki wanachotaka kumiliki.


Kwa upande mwingine wa kiuchumi, serikali yetu ingepata hela za kutosha kama ingeruhusu watu wengi wakamiliki magari kwani kutokana na matumizi ya mafuta serikali ingekusanya hela nyingi sana. Mfano, kama sikosei, kwa kila lita moja ya petrol serikali inachukua sh 500, sasa piga mahesabu. Ni kiasi gani kinakusanywa sasa hivi na serikali yetu. Ni ngapi ingekusanywa kama tungekuwa na magari mengi?


Ongezea na makato mengine kama vile leseni, road license, etc etc. Yaani mpaka basi tu.

WABUNGE WETU Please amkani na hili suala mkalishughulikie mapema sana
 
Nashhndwa kuwaelewa mkuu. Kigezo cha uchakavu wa gari ni mwaka wa utengenezaji au ni muda/km zilizotumika? Poor Tanzania
 
Nilishawahi kuzungumzia hili swala kodi za magari ni za ajabu na zinarudisha Tanzania nyuma kimaendeleo. Kodi ni muhimu kwa kipato cha nchi lakini ukiweka kodi kubwa sana kwenye bithaa muhimu kama magari na wakati huohuo magari hayapatikati Tanzania yote yanatoka nje ni sera ya kimasikini na kijamaa.
Kuna watu wengi sasa hivi hawawezi kuingiza magari si kwasababu ya bei ya magari bali ni kwasababu ya kodi ya ajabu ambayo imewekwa na wanasiasa ambao hawajui vizuri uchumi unavyofanya kazi. Mfano mimi binafsi siwezi kupeleka gari sasa Tanzania kwasabau ya kodi ni ya juu sana.
Pesa ya kodi ambazo zinapatikana na gari na umuhimu wake kwenye uchumi ni mkubwa sana kuliko kodi inayotozwa bandarini. Njoja niweke machache hapa
1. Gari linasaidia kuongeza shughuli za maendeleo kama usafiri na biashara
2. Matairi: Bila magari hakuna biashara ya matairi na matairi yanatoa ajira na kodi
3. Spare: Bila magari hakuna spare ambazo zinatoa ajira na kodi
4. Mafuta: Bila magari kodi ya mafuta na ujenzi wa Gas station hautakuwepo au utapungua.

Sasa kabla ya hao wabunge kuongeza kodi wanatakiwa kujiuliza maswali

1. Je gari mpya ambayo itakaa miaka kumi au kumi na tano itaweza kuingiza kodi kiasi gani na kusaidia kiasi gani kwenye uchumi?
2. Je ni pesa ngapi Tanzania inakosa kwasababu watu hawaingizi magari kwa kodi kua kubwa
3. Kuna faida gani kuweka kodi kwa CC? gari dogo inamaana kodi ndogo, mafuta kidogo, je magari madogo yanaweza kwenda sehemu kama Lushoto kule juu? sasa kuna faida gani kuweka kodi kubwa kwa magari makubwa?
 
Kuna hawa waheshimiwa wanaotaka kuipeleka Serikali mahakamani kudai kwamba kodi ya magari machakavu ni ya kibaguzi kwa vile iinabagua watu masikini dhidi ya matajiri.

Ukinunua gari lililotumika miaka kumi au zaidi unalipia kodi kama asilimia 20. Ukinunua jipya hulilpi kodi hii. Mimi nawaunga mkono, ila sijui uwezo wa sheria kutusaidia sisi akina yahe.

hivi neno masikini lina maana gani hapa? mtu akianza kufikiria kununua gari unamwita maskini? siku hizi kuna maneno kama walalahoi, wajasiliamali nk huwa yananichanganya sana,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom