Serikali inapowakatili raia wake kodi za kuingiza magari: Nini kifanyike?

Mimi kama Mtanzania nasikitishwa na viongozi wetu wa serikali na watunga sheria kwa ujumla.

Kodi za Magari ambazo Watanzania wengi wanalipa wanapotoa magari nje si za msingi na hazijafikiriwa kitaalamu. Kwa sasa kuna watu wanalipa kodi zaidi ya 50% ya gharama ya gari. Hizi hapa ni faida za gari kuingia Tanzania kwenye uchumi wetu.

1. Mafuta: Gari itaweka mafuta ili kutembea na kwenye mafuta kuna kodi, kunampa biashara gas station ambayo inatoa ajira na kulipa kodi, ujenzi wa gas station unasaidia kampuni za cement kama twiga, magari ya kubeba mafuta yanapata kazi, bank zinapata pesa kutokana na mikopo na biashara na zinaajiri, tanesco inapata pesa za umeme wa kusukuma mafuta n.k.
2. Maisha: Magari yanaraishisha maisha na kufanya shughuli ziweze kufanyika kwa haraka zaidi. Inaongeza "Productivity", magari yanasaidia kwenye maafa, kusafirisha abiria kama taxi, kwenye sehemu za mbali kama vijijini, kufanya biashara kama za utalii, ulizi, kubeba wagojwa.
3. Vipuli: Magari yana kaa zaidi ya miaka kumi kwa muda huo yatanunuliwa vipuli vya utengenezaji, maduka ya vipuli yatalipa kodi na kuajiri, vijana watapata kazi za ufundi, serikali itapata kodi ya uingizaji wa vipuli, viwanda vitatengenezwa n.k hii ni kwenye vipuli tu.
4.Matari: Magari yanahitaji matairi hivyo maduka ya matairi yatauza na kulipa kodi, vijana watapata kazi kwenye kampuni hizi, mabaki ya matairi yatatumika kwenye shughuli nyingine na serikali itafaidika.
5. Utengenezaji: Kampuni za utengenezaji kama kupiga rangi zinafanya biashara na kulipa kodi, zitaajiri, zitaagiza au kununua rangi na kulipia kodi n.k

Hizi ni faidi chache tu za kuingiza gari. sasa je serikali ikipunguza kodi na iwe kama nchi nyingine 8%-10% watapata hasara gari ukilinganisha na watu kuacha kabisa kuingiza magari??. Kama serikali itaanza kuingiza kodi kwenye magari ya mizigo na magari ya ujenzi itakuwa hasara kubwa kwa nchi. Tatizo la viongozi wetu ni kwamba wakiona vitu vinaongezeka kidogo wanakimbilia kuweko kodi wakithani kwamba vitu vitaongezeka tu bila kujali athari za uchumi.
 
Umesahau moja, au 2, Wanapunguza msongamano barabarani, na mizoga ya magari chakavu.
 
Angalia hata excemption tuliokuwa tunapata sisi walimu imesogezwa hadi miaka minane je tutweza kweli na mishahara hii midogo
 
Mwelekeo wa kutoza kodi Tanzania haueleweki.

Mfumo huu sijui unalenga kumsaidia nani na kwanini!kimsingi kodi ni muhimu kwa maendeleo ya Nchi yetu, kila mtu anatakiwa kulipa kodi awe masikiini au awe tajiri.

Mfumo ulenge kumtoza kodi zaidi mwenye nacho.

Kama mtu ana uwezo wa kumiliki gari alipe kodi tena hata mpaka 50%, mwenye uwezo wa kuishi mjini alipe kodi ya kichwa!!!! Kampuni za migodi walipe kodi ya faida waipatayo hadi 50% kusiwe na mchezo katika kodi. Wachezaji mpira walipe kodi, wanamziki walipe kodi.

HUWEZI KUMILIKI GARI USIAGIZE! SIYO NCHI INAJAA MAGARI YALIYOCHOKA
 
Niliponunua gari nchi za nje na kulitumia huko kodi ilikuwa 6%, nilishtuka wakati nimenunua gari nje na kuliingiza Tanzania gharama nilizolipia zilizidi gharama za kununua gari.

Ukinunua gari $5000 utegemee gari hadi lifike nyumbani kwako toka kifungoni mwa serikali na bandari zitakutoka zaidi ya Tsh zaidi ya 14 - 15 millioni. Hapa kuna tatizo. Sijapata kuna mfumo kama huo duniani, ni Tanzania pekee.

Ni dhahiri mtindo huu unasababisha rushwa kwa vile wasio na uwezo wataishia kutoa kidogo ili wapate gari, na njaa waliyonayo wengi jambo hili kuepukika ni vigumu kwa vile mazingira yametengeneza mazingira.
 
Ili bajeti zetu za kila mwaka ziwe endelevu ni lazima maoni ya walipa kodi yazingatiwe. kama ilivyo kwa mchakato wa katiba basi kuwe na mchakato wa maoni kuhusu njia bora ya kukusanya mapato ya taifa. ilivyo sasa mamabo yapo kama vile BORA LIENDE. ndio maana wanywa soda na bia hawaishi kuadhibiwa kwa kuongezewa kodi kila mara. inaonekana hatujajipanga vizuri kwenye suala la kodi. Mfano, nchi ina utajiri mkubwa wa madini je, mapato yake yanaendana?
 
ushauri mzuri. Kuhusu traffic jam tatizo liko Dar pekee hivyo watoe baadhi ya huduma. Imagine uwanja wa taifa, hospitali ya taifa, mawizara, vyuo vikuu zaidi ya 20! Huu ni ujinga
 
Kamundu

Umesahau kimoja mkuu! Yakichakaa yanauzwa kzmz chuma chakavu hivyo sioni sababu ya kuweka dumping fee wakati tayari ni raw materials for other product
 
Last edited by a moderator:
Habari za jioni wana JF!
Hapa nataka kuzungumzia kidogo bajeti ya 20012/2013 na marekebisho ya kodi ya magari!

Iko hivi:
a) Hakuna excemption kwa wafanyakazi wa serikali,
b) Magari ya mashirika ya dini yatalipiwa kila kitu
c) Magari chakavu yanapigwa penalty less than 8 years not 10 years kama ilivyokuwa

Hii imepitishwa na ile wanaita general budget and imeanza kauwa implemented pale TRA!

Jamani hivi wafanyakazi wa kawaida wa serikali wana benefits gani! manake ilikuwa walau hii ya excemption kwa wale wachache walioweza kuchukua mikopo wananunua magari walau ya biashara ndogondogo sasa excemption imefutwa mfanyakazi gani wa serikali wa kawaida anaweza kununua gari kwa Tanzania! Wabunge chondechonde msiipitishe hii kwenye budget ya wizara ya fedha bila kujali itikadi za kisiasa na bila kujali kuwa ninyi kwa sababu ya uwezo wenu wa kifedha mtaweza kutoa magari yenu! Chonde chonde wabunge wetu sisi walalahoi wa serikali hapa hatutatendewa haki kiukweli!

Magari ya mashirika ya dini hasa vijijini ndo ambulence za wananchi akitokea mgonjwa wananchi wanakimbilia kanisani kuomba msaada wa gari! Leo magari haya yalipiwe kodi mimi naona hii si sawa! Tunawakilisha kero zetu!

Me nafikiri tukubali mzunguko wa shekeli nchi hii ni mdogo there is no equal distribution of money! Watu wachache wanashikilia uchumi wa nchi sasa kama hizi sheria zikupitishwa maana yake mtu wa kawaida hawezi kuingiza gari nchini! Aliye nacho ataongezewa ndipo tunapokwenda!

Mimi sidhani kama kwa kufanya marekebisho haya itasaidia kukuza uchumi wa nchi! Serikali ikusanye kodi kwa wafanyabiashara ukienda kkoo ni maduka mangapi hutoa risiti hana maduka hasa ya wahindi wanakupa bei mbili bidhaa pamoja na risiti ina bei yake na bila ina bei yake! Hivi ninavyoongea kuna watu wameshindwa kutoa magari yao policy imebadilika gafla na watu hawajajiandaa wako frustrated! Ni changamoto ki ukweli!

Haya ni mawazo yangu lakini wabunge mliangalie hili kwa jicho la ziada!
 
Ushuru kwa magari ya taasisi za dini ni kasheshe na hata hivyo ni kutokutumia akili zao kikamilifu. Kwani makanisa au BAKWATA wanaagiza gari kila mwaka? Nimefanya kazi sehdmu fulani kwa wamisionary tangu mwaka 86 hadi 94, gari la mwisho walinunua 92 na mengine ya zamani zaidi ya hapo nimekwenda kuwatembelea juzi nimeyakuta. Kama unavyosema. Wafanyabiashara hawalipi kodi kwa kiwango kinachotakiwa. Wabunge watakusikia sasa? Wale wa upinzani wataipinga lakini wale wa kwenu hawanatatizo nayo.
 
Kwani ukiwa mfanyakazi lazima ununue gari? kama umefikia kiwango cha kumiliki gari basi pesa unazo lipia kodi, badala ya kulilia bei ya mchele au unga iwe chini maana ndio uhakika wa maisha ya kila siku.
Kama vipi nunua punda kwani na yeye analipishwa kodi?
 
Control ya ushuru wa magari ya mashirika ya dini na watumishi ni ngumu sana , mara nyingi imekuwa ikitumika vibaya ndio maana imeondolewa. Kuna watumishi wa kada za kawaida wanaagiza magari kila mwezi!
 
Habari za jioni wana JR!
hapa nataka kuzungumzia kidogo bajeti ya 20012/2013 na marekebisho ya kodi ya magari!
yako hivi
a) hakuna excemption kwa wafanyakazi wa serikali,
b) Magari ya mashirika ya dini yatalipiwa kila kitu
c)magari chakavu yanapigwa penalty less than 8 years not 10 years kama ilivyokuwa
hii imepitishwa na ile wanaita general budget and imeanza kauwa implimented pale TRA!

Sina hakika sana na hapo kwenye red....budget ninayo may be tafsiri za kilichoandikwa kama hawakukiweka wazi lakinia madam JUDITH MGASSE (or any knowlegeable person.....) ni ukurasa au kipengele kipi cha budget kilichoprovide haya??
 
Control ya ushuru wa magari ya mashirika ya dini na watumishi ni ngumu sana , mara nyingi imekuwa ikitumika vibaya ndio maana imeondolewa. Kuna watumishi wa kada za kawaida wanaagiza magari kila mwezi!

Mkuu hii ni ngumu kwani utaratibu unapata exemption after 5 years sasa hili la kila mwaka linakujaje?? in addition pale TRA kila kitu kiko controlled kwenye compyuter na TIN no inayotumika ni moja ambayo mtumishi wa umma anaitumia kulipia kodi kila mwezi...
 
Nadhani dawa ni kwa mashirika ya dini kuongeza gharama kwenye huduma za kijamii wanazotoa ili angalau wananchi waanze kulalamika. Nchi ya mazezeta.
 
Kuweni wajanja kama CHADEMA nunueni PICKUP kwani hizi kidogo KODI ipo chini. au nunueni magari yenye cc chini ya 1000 Pia KODI ni chini.
 
Siyo kweli mleta mada fuatilia vizuri pale TRA watakuelewesha,Exemption kwa wafanyakazi hazijaondolewa,
na wala za mashirika ya dini hazijaondolewa.Na wewe Maundumula acha kusema vitu vya uongo,mfanyakazi
wa serikali anasamehewa gari moja tu,baada ya miaka 5, anaweza kulilipia kwanza ndipo anapewa msamamaha
mwingine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom