Serikali inapambana na bei ya sukari huku ikipandisha bei ya Mafuta

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,654
Sukari imeanza kuwa dili mitaani. Wafanyabiashara ni kama vile wameamua kususia uuzaji wa sukari. Hakuna anayetaka kuuza kwa bei elekezi ya serikali.

Cha kushangaza ni kuwa wakati bei ya sukari inapanda, ya mafuta nayo ipo almost vile vile wakati bei ya mafuta katika soko la dunia ilishuka mpaka negative. Yan dealers wakaanza kulipwa ili kuchukua mafuta kiwandani.

Kwanini serikali isishushe bei ya mafuta ili kupunguza costs za uzalishaji ili sukari ishuke bei?

Watakuja hapa wa kukurupuka na kusema kuwa serikali haipangi bei ya mafuta. Ni kweli haipangi bei ya mafuta duniani ila inauwezo wa kupanga bei ya mafuta ndani ya nchi kama inavyofanya hivi sasa.

Siku zote bei ya mafuta inapokuwa kubwa hata Tax inayopokea serikali huwa kubwa. Na bei ikishuka serikali nayo hupokea tax kidogo kutokana na mafuta. Hivyo serikali haitaki bei ishuke ili iendelee kupata mapato makubwa.

Ila wakati kama huu ndyo mafuta yalitakiwa kupungua ili kupunguza gharama za uzalishaji na viwanda viweze kuuza kwa bei ndogo.
 
Back
Top Bottom