Serikali Inaishi kwa Matumaini...

Serikali Inaishi kwa Matumaini...

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2014
Posts
3,344
Reaction score
2,537
Serikali ya Tanzania inaishi kwa matumaini kwani haina fedha, kwa sasa inategemea makusanyo ya kodi ya mwezi kutoka TRA ambazo hazizidi milioni 900 kwa mwezi, ambapo katika hizo bado mishahara ya kila mwezi ya wafanyakazi wake, gharama za uendeshaji wa shughuli za siku kwa siku za serikali na kulipa madeni yake ya ndani na nje na kwa makandarasi wa miradi ya barabara.

Sasa serikali baada ya kukopa bank ya NMB na NBC kulipa mishahara ya wafanyakazi, kiwango cha kukopa kwake kilifika mwisho, mathalani bank ya NBC ambapo serikali ina hisa, kiwango chake kama mwanahisa cha kukopa kilifika mwisho hivyo ikazuiwa na mwanahisa mwenzake kutokukopa.

Hivyo taarifa zinasema Serikali imeingia makubaliano na bank ya Baclays ili kuweza kukopa kulipa mishahara ya kila mwezi kwa wafanyakazi wake.

Ndiyo maana kwa sasa bank nyingi hazikopeshi raia mmoja mmoja (mteja wa bank).
 
Ni aibu sana kwa serikali kuishi "From hand to mouth".

Serikali kila wakati inaasa wananchi kujenga utaratibu wa kujiwekea akiba; sasa kama yenyewe haiwezi kuonyesha mfano mwanachi atahamasika vipi?!
 
Mkulu si alisema huko nje ziko pesa nyingi na ni jinsi tu unavyojipanga na kuomba wao wanatoa tu, sasa imekuwaje tena!?
 
Hii habari ni ya kweli kabisa.inahuzunisha kuona taasisi za serikali zipo hatua za mwisho kuandaa bajeti ya 2015/16 wakati release of funds kwenye bajeti inayotekelezwa haifiki hata nusu.
 
Vilaza fulani watahoji chanzo cha hii habari wakati hii ndio halihalisi kwa sasa.
 
Hii ni habari ya kweli kabisa. Mimi nafanya kazi katika taasisi inayotegemea makato kutoka hazina. Amini usiamini mpaka sasa hatujapata mshahara wa mwezi uliyopita kwa sababu hazina haina fedha ya kutuma kwenye benki yetu , mpaka sasa tunaishi kwa matumaini.
 
Na iendelee hivi hivi tuone kidume anaeifagilia gvt na majoka ya makengeza.....
 
Serikali ya Tanzania inaishi kwa matumaini kwani haina fedha, kwa sasa inategemea makusanyo ya kodi ya mwezi kutoka TRA ambazo hazizidi milioni 900 kwa mwezi, ambapo katika hizo bado mishahara ya kila mwezi ya wafanyakazi wake, gharama za uendeshaji wa shughuli za siku kwa siku za serikali na kulipa madeni yake ya ndani na nje na kwa makandarasi wa miradi ya barabara.

Sasa serikali baada ya kukopa bank ya NMB na NBC kulipa mishahara ya wafanyakazi, kiwango cha kukopa kwake kilifika mwisho, mathalani bank ya NBC ambapo serikali ina hisa, kiwango chake kama mwanahisa cha kukopa kilifika mwisho hivyo ikazuiwa na mwanahisa mwenzake kutokukopa.

Hivyo taarifa zinasema Serikali imeingia makubaliano na bank ya Baclays ili kuweza kukopa kulipa mishahara ya kila mwezi kwa wafanyakazi wake.

Ndiyo maana kwa sasa bank nyingi hazikopeshi raia mmoja mmoja (mteja wa bank).

Una uhakika na hiyo namba? Mimi nadhani ni billion 900.
 
Nakubaliana na hii habari kuna ukweli,kwani hata Tra wanahaha sanaa kukusanya kodi kws sasa,mfano customs kampuni nyingi za clearing zinafungiwa eti tu akitengeneza document isipolipwa zaidi ya siku tatu unafungiwa kampuni,hata kama mzigo haujafika yaani meli ikiwa haijafika unalazimishwa kulipa,na wsnasema wazi serikali haina hela hivyo inabidi tuwabane mlipe kodi haraka
 
Baba Asha alisema serikali yake inakusanya billion 900 kwa mwezi. Je alidanganya umma wa watanzania na ulimwengu au aliuziwa mbuzi kwenye gunia kama kawaida yake?
 
Bandiko lako lina ukweli kwa sana tu kwa sababu pesa inayoonekana sana katika mzunguko kwa wingi ni sh 1000,2000,na kwa nadra 5000.Nyingi ni chakavu.Kupata noti mpya au 10000 ni nadra sana kulingana na ufuatiliaji wangu. Bars hazijai sana kama kawaida yake maana ndio sehemu inayoonyesha matumizi ya watendaji wa serikali. Hali hii ngumu iko tangu mwaka jana mwishoni.Matumizi kwa sana yamepungua,kama yapo kwa sana ni kwa wale walioko jikoni.
 
Rekebisha siyo 900mil kwa mwezi bali 900bil kwa mwezi ndiyo makusanyo ya serikali kwa mwezi. Mengine hali ya ukata wa serikali imekuwa ikizungumziwa toka kitambo sana lakini inabaki kuwa nadharia ambayo kuthibitisha kwake ni issue.
 
900bil Mnazijua nyie?
 
Back
Top Bottom