Babu wa Kambo
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 559
- 808
Mzozo unaendelea Wizara ya Afya, baada ya punguzo la 30% ya Mishahara, sasa Serikali imewaachisha kazi madaktari wote walioajiriwa hivi karibuni (chini ya miezi 6 tangu waajiriwe) waliokuwa wakifanya kazi katika hospitali za mashirika ya dini (Faith based organizations) kama Bugando na KCMC kwa kile kilichodaiwa "kuhakiki watumishi hewa". Hawa ni wale madaktari wa Serikali ambao ajira zao zilipelekwa FBOs wakati wenzao walipangiwa hospitali za umma. Kwa hiyo serikali imezuia kupeleka mishahara hali iliyopelekea madaktari hao kusimamishwa kazi hadi mishahara yao itakaporudi.
Nimeambatanisha barua ya mmoja wa madaktari walioathirika na zoezi hili (nimeficha jina na refference number ya barua ili kumlinda). Yeye na wenzie zaidi ya 20 wamesimamishwa kazi hospitali ya Bugando kwa kile kilichoelezwa "zoezi la kuhakiki watumishi hewa"
Hawajaambiwa tarehe ya kurudishwa kazini, na mbaya zaidi wameachishwa kazi kwa notisi ya chini ya mwezi mmoja kinyume na sheria ya utumishi inayomtaka muajiri kutoa notisi ya mwezi mmoja kabla, au amlipe mtumishi mshahara wa mwezi mmoja kama compensation ya kuchelewesha notisi.
Licha ya hayo madaktari wote walioachishwa kazi Bugando hawajalipwa mishahara yao kwa miezi miwili ya mwisho (May and June) na kwa kuwa wameshaachishwa kazi hawajui hatma ya mishahara yao wanayodai watalipwa lini.
Mbali na Bugando, hospitali nyingine za rufaa zilizoathirika na agizo jili la serikali ni KCMC, Huruma Hospital, Seliani, Ikonda etc.