Serikali imesitisha michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA kwa mwaka huu

Kachumbi

Member
Aug 26, 2014
70
30
Mashindano yanayotegemewa kufanyika Mwanza,Maandalizi yaliyokuwa yanafanyika katika chuo cha Butimba yameingia dosari baada ya kuhisi kuna harufu ya rushwa na ufisadi, inasemekana lakini.

Kuna rundo la watu walijitokeza kuanzia jana na leo asubuhi kupigania nafasi ya kuwemo kwenye kamati,muda si mrefu wameambiwa wa stop kwa shughuli zote walizokuwa wanajitolea mpaka taarifa itakapotoka tena.

Mwenye la ziada atujuze.

======

SERIKALI YASITISHA MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA KUPISHA ZOEZI LA KUMALIZA UPUNGUFU WA MADAWATI NCHINI

SERIKALI imetoa tamko la kuhairisha mashindano ya umoja wa michezo na Taaluma kwa shule za Msingi na Sekondari Tanzania (Umitashumta na Umisseta) ili kupisha zoezi la kumaliza upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari hadi hapo yatakapotangazwa tena.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Waziri wa ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene amesema mashindano hayo yameahirishwa ili kupisha zoezi la kumaliza upungufu wa madawati kwenye shule za msingi na sekondari kwani wadau muhimu wa mashindano hayo wote wanahitajika katika kumaliza tatizo hilo.

Amesema kuwa mpaka jana zilikuwa zimebaki siku 17 tu ambazo Rais John Magufuli alikuwa amezitoa kwa ajili ya kumaliza tatizo la upungufu wa madawati nchini hivyo amewataka wadau wote wa mashindano hayo kuvuta subira hadi hapo zoezi hilo litakapomalizika ndipo waendelee na mashindano hayo.

Amesema mashindano hayo yanashirikisha viongozi wote katika ngazi ya halmashauri, mikoa na wizara ambapo viongozi hao ndio wanaoshiriki katika kusimamia na kufanya ufutiliaji wa zoezi la utengenezaji wa madawati kama alivyoagiza Rais Magufuli.

“Kwa vile muda uliobaki kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais la utengenezaji wa madawati ni finyu kwa maana siku 17 tu, serikali imeona ni busara sana kuahirisha michezo hiyo ili nguvu zote zielekezwe kwenye utengenezwaji wa madawati na michezo hiyo itafanyika tarehe nyingine itakayopangwa na kutangazwa,” amesema Simbachawene.

Ameongeza kuwa, “Nitoe wito kwa walimu wetu waendelee kuwahimiza wachezaji wote walioteuliwa kuendelea na mazoezi katika shule zao wanazosoma, hii itakuwa ni sehemu ya kujitayarisha kwa ajili ya mashindano hayo muhimu mara yatakapopangwa.”

Michezo ya Umisseta ilipangwa kufanyika kitaifa Jijini Mwanza ambapo ilitakiwa ianze June 13 hadi 22 mwaka huu huku ile ya Umitashumta ilipangwa kuanza June 25 hadi Julai 5 mwaka huu ikiwashirikisha jumla ya washiriki 6,200.


Chanzo: Michuzi
 
Hawajui hii ni serikali ya not as usual eti wambie wakatulie wasije jikuta cello maana watapata nafasi wakizani Kuna mafungu

Mwisho wa siku hayo mafungu wayakose wazirie michezo hapo ndi wataijui ile namba ipi iliyokuwa inaibwa kuwa wataisoma namba
 
...inasemekana serikali imezuia kwa muda mashindano ya umisseta na umitashmuta hadi itakapotangazwa baadaye!!!!

Maafisa elimu wa mikoa na wilaya walitaka kutengeneza vitegauchumi vyao
 
Nipo hapa mwanza,kuna mbinu chafu zilikuwa zinafanyika,watu wapo kwa ajili ya kupga pesa,wakubwa wengi hawakuwa bize kwenye mchakato wa kupata vijana sahihi,ngaz za juu wapo bize balaaa...pamoja na hayo ni vzr yaendelee maana mikoa mingine ilikuwa imeishaanza safari !!
 
Serikali imesitisha michezo ya umiseta na umishumta mpaka itakapotangazwa tena. Maamuzi hayo yalitolewa jana jioni wakati ambao baadhi ya mikoa ikiwa njiani kuelekea mwanza kwa mashindano ya taifa yaliyotegemewa kuanzia tarehe 13/06/2016. Sababu ya kusimamishwa ni ukosefu wa fedha.

Hapa wadau nauliza je serikali hii inayoonekana Kama si rafiki wa MICHEZO, michezo ya shule ya msingi na sekondari itarudishwa tena Au hii ni gia ya kuyafuta kimoja?

Je hii haitaathiri viwango vya wanamichezo wetu wa baadae?
 
Eti mwanafunzi anachangia sh 1500,ngazi ya shule sh 150,ngazi ya kata 150..ya tarafa 300,yaani ni upuuzi mtupu..
 
Serikali imesitisha michezo ya umiseta na umishumta mpaka itakapotangazwa tena. Maamuzi hayo yalitolewa jana jioni wakati ambao baadhi ya mikoa ikiwa njiani kuelekea mwanza kwa mashindano ya taifa yaliyotegemewa kuanzia tarehe 13/06/2016. Sababu ya kusimamishwa ni ukosefu wa fedha.

Hapa wadau nauliza je serikali hii inayoonekana Kama si rafiki wa MICHEZO, michezo ya shule ya msingi na sekondari itarudishwa tena Au hii ni gia ya kuyafuta kimoja?

Je hii haitaathiri viwango vya wanamichezo wetu wa baadae?
Shangilia kama mlivyozoea
 
Ni kweli imefutwa!! Ila si misuse of resources, how come unazuia Michezo wakati booking zimeshafanyika, wanafunzi baadhi wako safarini, kila kitu Kiko okay! Na wanakwenda kwenye fainali! Sio kwamba Ndio inaanza, huu ni ubadhirifu.
 
Kwan had wanaanza ktk ngz ya chin means mashuleni bajet haikuwepo. Mbona tutakuwa kama tunakurupika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom