Serikali imeshindwa kushughulikia mgawo wa umeme

Serikali imeshindwa kushughulikia mgawo wa umeme

Ichwampaka

Senior Member
Joined
Nov 19, 2018
Posts
145
Reaction score
118
Serikali,
Tunaomba mtuondolee kero ya mgao wa umeme hasa hapa Dar es Salaam. Miezi kama hii sisi hatukuzoea kusikia majenereta kila mahali Kariakoo, hivi sasa kila ki saluni cha kunyoa nywele kina jenereta. Umeme unakatika hovyo hovyo kwa siku hata mara sita. Siku nyingine unakatika siku nzima. Siye huku Mbagala tumeshazoea wiki nzima kutokuwa na umeme.

Mbona wenzenu walikuwa na vyanzo hivi hivi vya umeme lakini ulikuwa haukatiki kama hivi sasa?. Halafu wenzenu walisambaza umeme vijiji kote nyie mbona kwa muda mreefu hajamsambaza kabisa umeme.

Wenzenu walikuwa wanaweka umeme kwenye majumba ya kueleweka tu, nyinyi mnawawekea hadi walala hoi kabisa wenye matembe- kisa mnajali utu wa mtu na kuwa nyumba ya mtu ni nyumba kwake hata kama wewe unaona ni tembe

Tafadhali sana tuondolee hii kero. Kesho nitaleta malalamiko kwa Jeshi la Polisi na serikali kwanini mmetupunguzia milio ya risasi mitaani, hadi leo tumepoteza utaalamu wa kujua ni bastola Magnum 38 au ni SMG. Wenzenu ilikuwa kila siku shaba zinapigwa mitaani hadi tulikuwa experts wa kubaini aina ya silaha.
 
Kawadanganye Chadema, tupo kwenye lait tlak.
 
Mbagala gani hiyo umeme unakatika wiki nzima,maana mimi nipo mbagala lakini sikumbuki mara ya mwisho lini umeme kukatika....Nadhani itakuwa ni tatizo eneo ulilopo siyo mgao huo.

Wasiliana na wahusika inapotokea hali kama hiyo
 
Uongo wa nini?

Toka Magufuli ashike nchi umeme mtaani kwetu kukatika imekua tukio la ajabu
Ni nadra sana
 
Back
Top Bottom