Serikali imeshindwa kudhibiti mauaji

Serikali imeshindwa kudhibiti mauaji

Joined
May 28, 2013
Posts
91
Reaction score
17
Wiki inayomalizika leo, wananchi waliendelea
kushuhudia matukio makubwa ya mauaji na vitendo
vingine vya kihalifu vinavyoashiria kwamba Jeshi la
Polisi na mamlaka nyingine za usalama pengine
hazina tena uwezo au utashi wa kulinda raia na mali
zao. Hali ya usalama imeendelea kuzorota kwa kasi ya ajabu, hivyo hakuna mwananchi anayeweza
kujidanganya hivi sasa kwamba maisha yake yako
salama na kwamba atapata mahali pa kukimbilia
iwapo maisha yake yatakuwa hatarini.

Tunaelewa fika kwamba kauli hiyo hapo juu ni nzito,
lakini tumeitoa bila woga wala kutafuna maneno
kwa kutilia maanani ukubwa wa tatizo. Tatizo la
mauaji ya watu wasiokuwa na hatia katika nchi yetu
hivi sasa ni kubwa. Silaha zimezagaa ovyo mitaani na
zinauzwa kama njugu, huku zikitumika kuwaua watu kwa lengo la kupora mali zao, kuwatia vilema
vya maisha au kulipiza visasi. Hali hiyo ni mbali na
mashambulizi wanayofanyiwa baadhi ya watu kwa
lengo la kuwadhuru, ikiwa ni pamoja na
kuwamwagia tindikali, kuwateka nyara,
kuwanyofoa macho na kuwang’oa meno na kucha. Hoja yetu kuu hapa ni kwamba, wananchi wamejaa
woga na hofu kwa kutokuwa na uhakika wa
usalama wao. Jambo linalochochea hali hiyo ni Jeshi
la Polisi kutoonekana kufadhaishwa wala kukerwa
na hali hiyo.Baya zaidi ni pale Serikali inapobaki tu
kuwa mtazamaji wa hali hiyo ya kutisha pasipo kubuni mbinu za kuhakikisha Jeshi la Polisi
linawajibika vilivyo. Inakuwaje kila kukicha mauaji
yanaendelea katika sehemu mbalimbali nchini, huku
Polisi nao wakithibitika kuhusika na vifo vya raia
wasio na hatia katika baadhi ya matukio? Katikati ya wiki, wafanyabiashara wawili maarufu katika Mikoa ya Arusha na Manyara waliuawa katika
matukio tofauti kwa kupigwa risasi na watu
wasiojulikana. Kama hiyo haitoshi, siku mbili
zilizopita mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam aliuawa jijini kwa kupigwa risasi na watu
wasiojulikana wakati akitoka benki, huku wasichana wawili raia wa Uingereza wakimwagiwa tindikali
mjini Zanzibar na watu wasiojulikana. Kuhusu tukio
la Zanzibar vyombo vya habari duniani kote
vimeandika na kutangaza sana tukio hilo, ambalo
linasemekana litaathiri sana utalii wa Zanzibar kwa
muda mrefu. Kama tulivyoeleza hapo juu, matukio hayo ni kama
tone moja tu la maji katika Bahari ya Hindi, kwani
matukio ya aina hiyo katika kipindi cha miezi sita
iliyopita ni mengi mno kuyaorodhesha katika safu
hii. Wananchi hawajasahau matukio ya kutekwa na
kuteswa kwa Absalom Kibanda na Dk Ulimboka jijini Dar es Salaam, wala hawajasahau kupigwa risasi na
kujeruhiwa kwa Padre Ambrose Mkenda, kuuawa
kwa kupigwa risasi kwa Padre Ambrose Mushi na
kumwagiwa tindikali kwa Sheikh Saroga wote wa
visiwani Zanzibar. Ajabu ni kwamba Serikali imetia pamba masikioni na
tunahisi inafanya hivyo makusudi. Ukimya wa
Serikali unatokana na kulikumbatia Jeshi la Polisi na
kushindwa kuliwajibisha, kwani jeshi hilo
limethibitika kuibeba Serikali na chama tawala dhidi
ya vyama vya upinzani. Ni maoni ya wengi kwamba mpaka pale jeshi hilo litakapojivua minyororo ya
utumwa wa kisiasa, likavunja ndoa na wanasiasa na
kuwa jeshi lenye weledi, ndipo tutakapoona mwisho
wa mauaji na uhalifu mwingine ambao
umepandikiza hofu na kuchafua taswira ya nchi
yetu.
 
Pinda: "....kwa sababu tumechoka sasa..."
 
Back
Top Bottom