serikali imenywea - Mwanahalisi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

serikali imenywea - Mwanahalisi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyambala, Feb 26, 2009.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  SERIKALI IMENYWEA..................................Gazeti la MwanaHALISI  SERIKALI imeshindwa kusema lolote kuhusiana na kushiriki katika wizi wa mabilioni ya shilingi kupitia kampuni ya Kagoda Agriculture Limited.

  Taarifa za gazeti hili, toleo la wiki iliyopita, zilimnukuu wakili mmoja wa mjini Dar es Salaam akisema, chini ya kiapo, kwamba aliambiwa na Rostam Aziz kuwa fedha hizo zaidi ya Sh. 40 bilioni zilikuwa ni za kugharamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa 2005.

  Wakili huyo, Bhyidinka Michael Sanze, ananukuliwa akiwasiliana na Kamati ya Rais ya Kushughulikia wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwamba miongoni mwa wahusika wakuu katika wizi huo, ni rais mstaafu Benjamin Mkapa.

  Wengine aliowataja ni Rostam, Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula, gavana wa BoT, Dk. Daud Ballali, Mkurugenzi wa Mipango na Uchumi BoT, Peter Noni na wakili wa kujitegemea, Bered Malegesi.

  Mwanasheria mashuhuri nchini, Mabere Marando alipotakiwa maoni yake juu ya kigugumizi hiki cha serikali, alisema, “(Serikali) hawawezi kusema kitu.”

  Alisema, “Mimi nadhani serikali imepigwa na butwaa. Hawakujua kama vitu hivi vitaibuliwa. Hawakujua haya! Inawezekana wameshangaa haya mliyoandika.”

  Sanze, wakili katika kampuni ya mawakili ya Malegesi – Malegesi Law Chambers – ya Dar es Salaam, anasema katika andishi lake kuwa alishuhudia mikataba ya uchotaji fedha alipokuwa katika ofisi za kampuni ya Caspian Construction Limited ambayo inamilikiwa na Rostam, mfanyabiashara na mbunge wa Igunga.

  Sanze, katika hati ya kiapo, anadai kuelezwa na Rostam kuwa alikuwa kwenye kikao cha Mkapa, Mangula na Ballali ambapo anasema “alishuhudia Mkapa akitoa amri kwa Ballali” ya kutoa fedha hizo na kumkabidhi yeye (Rostam).

  Siku nane tangu taarifa hizo zitoke, serikali haijesema lolote na viongozi mbalimbali ambao gazeti hili limejitahidi kuwasiliana nao, ama wamesema hawataki kuzungumza lolote au hawana la kusema.

  MwanaHALISI ilimtafauta Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili kutaka kujua msimamo wa serikali baada ya ushahidi huo kuanikwa hadharani, lakini hakuweza kupatikana.

  Msaidizi wake, Ole Kuyani alimtaka mwandishi kuwasiliana na msaidizi mwingine alimyetaja kwa jina moja la Ibambiro, kwa maelezo kwamba huyo ndiye yupo karibu zaidi na bosi wake kwa wakati huo.

  Ibambiro alipatikana na baada ya kuelezwa kile ambacho MwanaHALISI inahitaji kutoka kwa waziri mkuu, aliahidi kupiga simu baada ya kuwasiliana na Pinda.

  Gazeti lilipoona kimya kimekuwa kirefu, lilipiga tena simu ofisini kwa waziri mkuu, lakini aliyepokea alijibu kwa ufupi. “Tumekuahidi kukupigia. Subiri utapigiwa.”

  Hadi tunakwenda mitamboni, ofisi ya waziri mkuu haikupiga simu MwanaHALISI.

  Waziri mkuu Pinda aliahidi wananchi kupitia vyombo vya habari Desemba mwaka jana, kwamba “Serikali haigopi Kagoda na kwamba masuala yote yanafuatiliwa na yataelezwa bayana uchunguzi utakapokamilika.”

  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alipoulizwa Polisi inachukua hatua gani baada ya kupatikana ushahidi wa Sanze kuhusika kwa Kagoda na vigogo wengine katika ukwapuaji wa fedha BoT, alisema “hilo aulizwe Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).”

  “Nimekuelewa. Lakini kwa ujumla, sisi hatujadili ushahidi hadharani. Ushahidi unajadiliwa mahakamani,” alisema Manumba.

  Juhudi za gazeti kumpata DPP hazikuweza kuzaa matunda. Awali alipopigiwa simu juzi Jumatatu, DPP Eliezer Feleshi alipokea na baada ya mwandishi kujitambulisha alisema, “nipo kwenye kikao, nipigie baadaye.”

  Alipoulizwa apigiwe baada ya muda gani, Feleshi alisema, “ni baada ya saa moja.” Gazeti liliendelea kumtafuta Feleshi juzi Jumatatu lakini simu yake ilikuwa inaita bila kupokelewa. Hadi tunakwenda mitamboni Feleshi alikataa kujibu simu.

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika hakupatikana, lakini msemaji wa Wizara ya Sheria na Katiba, Omega Ngole, alipoulizwa juu ya msimamo wa ofisi yake, kuhusiana na waliotajwa na wakili Sanze katika sakata la Kagoda, alisema hayo ni mambo ya kujadili ofisini.

  Simu ya Mwanyika Na. 0713 324854 kila ilipopigwa ilitoa jibu, “simu unayopiga haipatikani, jaribu tena baadaye.” Ilipigwa tena na tena, lakini jibu bado lilikuwa ni hilohilo.

  Kwa mujibu wa andishi la Sanze, alishuhudia mikataba hiyo kwa kusaini baada ya kuthibitishiwa na Malegesi kuwa alishakwenda kujiridhisha kwa Ballali na Mangula. Sanze alisisitiza, “Rostam mwenyewe alisema, ‘system yote inajua.’”

  Alipoulizwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba amepokeaje taarifa zilizotolewa na Sanze kuhusu “sakata la Kagoda” hasa kwa kuwa zimetaja viongozi wa CCM, aliingia kati na kusema, “Kama ni masuala ya Kagoda, mimi sina la kuzungumza.”

  Mwandishi alipomueleza kuwa inajulikana wakati wa “sakata la Kagoda” yeye hakuwa katibu mkuu wa CCM, isipokuwa Sanze anasema fedha zimewasilishwa katika chama, Makamba alisisitiza, “Kama ni Kagoda hilo sina jibu.”

  Makamba akakata simu. Gazeti linamtafuta Makamba ili pamoja na mambo mengine, ajibu swali: Zipo taarifa zozote katika chama zinazoonyesha kwamba Rostam Aziz aliingiza fedha zilizochotwa EPA, katika kampeni za CCM?

  Inspekta Jenerali wa Polisi nchini (IGP), Said Mwema hakupatikana. Simu yake Na. 0754 785557 ilikuwa inaita bila kupokelewa.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hoseah, alipoitwa kwa simu yake Na. 0784 763741, simu yake ilikaa kimya. Baadaye ilipopigwa tena ilijibu, “samahani simu unayopiga haipatikani kwa sasa.”

  Mwanyika ndiye alikuwa mwenyekiti wa Timu ya Rais ya kufuatilia yaliyogunduliwa na maodita wa Ernst & Young katika ukaguzi wa akaunti ya EPA kwa mwaka 2005/2006. Wajumbe wengine wa timu hiyo ni IGP Mwema na Hoseah.

  MwanaHALISI iliwasiliana na Dk. Willibrod Slaa, mbunge wa Karatu na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ili kutoa maoni yake ambapo alisema serikali haiwezi kujibu lolote kwa sababu inajua kila kitu kuhusu Kagoda.

  “Nyaraka mlizotumia, hata mimi ninazo. Nimejiridhisha kwamba haya mliyosema ni sahihi, na kwamba serikali inayajua. Lakini haitaki kusema ukweli huu kwa sababu, inahusika katika wizi huu,” alisema Dk. Slaa.

  Wakili Marando anafika mbali zaidi. Anasema, “Serikali haijapuuza, tatizo hawajui la kufanya. Nimeiona affidavit (hati ya kiapo) ya Sanze ni sahihi.”

  Anasema, “Mimi sioni kama Watanzania watasahau haya. Serikali na CCM wanajua kwamba viongozi wa vyama vya upinzani watatumia hoja hizo katika kampeni.”

  Hii ni mara ya kwanza Mkapa kutajwa katika sakata la kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, lakini ni mara nyingi Rostam amehusishwa na ukwapuaji huo ndani ya BoT.

  Hadi sasa, watuhumiwa 20 wamefikishwa mahakamani kuhusiana na sakata la ufisadi wa fedha za EPA, lakini kumekuwa na ugumu kwa serikali kushughulikia wahusika wa Kagoda:

  My opinion:

  Haya mambo yaliongelewa sana sana hapa JF na nnadhani wakuu walipuuza kwa kujua anywayz ni watanzania wangapi wana access na internet? Lakini inapotokea kwenye public tena kwenye gazeti siamini akina Mkamba, Chiligati kama kawaida yao kukaa kimya kwa wiki nzima. RA naye vp si alishatishia kulishtaki gazeti hili aliishia wapi?
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mods naomba mfute hii thread maana ni continuation ya ille ya sakata la kagoda!
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,556
  Likes Received: 18,268
  Trophy Points: 280
  Kagoda, Kagoda, Kagoda, ...ni kelele za mlango, mwenye nyumba bado amelala maana anajua kila kitu.
   
 4. T

  Tofty JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2009
  Joined: Nov 6, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  duh....kaazi kweli kweli!!!
   
 5. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Baada ya kifo cha mgombea mwenza wa CHADEMA, hayati Jumbe, gazeti la Tanzania Daima kupitia Ngurumo, liliandika kuwa "Mkapa aagiza ushindi upatikane kwa gharama yoyote". Aliyasema hayo akiwa mkoani Kagera, tena kwenye kambi ya jeshi ya Kaboya. Affidavit ya Sanze inaonyesha ubabe huo wa kumshinikiza Ballali atoe fedha haraka kwa Rostam. Ndugu zangu, jambo hili linanuka ukweli mtupu!
   
 6. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kagoda hata ikirudiwa mara 100 haipwai kwani ni wizi mkubwa wa rasilimali za TZ,kama ushindi unapatikana kwa wizi kama huo,uongozi huo ni batili,wanasheria mpo??Tanzania inaongozwa na serikali iliyoingia madarakani kwa kununua kura kwa fedha walizoiba BOT ndio maana wanailinda Kagoda kwa gharama yoyote ili isishitakiwe.Jibu litapatikana tu kama si 2010 ni wakati mwingine kwa dhambi na wizi au dhuluma iliyofanyika haipotei kama haijapatiwa ufumbuzi itafufuka tu hivyo wahusika wakae tayari labda wafe kabla ya suala hilo kufufuliwa.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hakuna kunyamaza kuhusu kagoda na Watanzania tutafanya makosa makubwa tukiliachilia hili kupita hivi hivi. Haiwezekani mtu tu katuibia bilion 40 halafu serikali yetu inakuwa bubu, hii ina maana serkali ya CCM inahusika moja kwa moja. Kauli wanazotoa baadhi ya viongozi wa chama hicho kwa njia ya kigugumizi kusema eti CCM haihusiki na wizi huo ni ushahidi tosha kwamba walihusika. WATANZANIA TUSIKUBALI HILI KABISAAAAAAAAAAAAAAAAA!
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapa Modi usifute kitu ,tunaendeleza mawazo mepya na kule kwa zamani kumeshakuwa mzigo na makaburasha yamekuwa mengi ,huu naona ni ukurasa mpya.

  Serikali iliyopo madarakani inahusika na wizi ndio maana yake,Chama kilichopo madarakani kinahusika na wizi ndio maana yake, Ni Chama tu mtu mmoja mmoja asingeweza kuiba ,ila wote wale vigogo wa Chama kwa kushirikiana ndio wamewezesha wizi kutokea ,Kikwete hana budi kujiuzulu na kuivunja serikali iliyokuwepo madarakani ,msajili wa Vyama anasemaje kwa hili ? Mambo ya kusema Upinzani jitahidini muchukue viti vya ubunge mikoani kwa mchezo huu unaochezwa na CCM ,hivi anaweza kukifungia Chama cha CCM ? AU na yeyey nio mshirika ,bila ya shaka yeyote ni mshirika tu ,ndio maana anakuwa mkali kwa kina Mrema.

  Utawala wa CCM ni wa kitapeli na umeuza hazina ya nchi na kama haitoshi wamekwapua na Benki kuu.Hawana tofauti na majambazi kuna wakati ujambazi ulikuwa umeshika kasi maana walikwisha ona hakuna wa kuwagusa ,wakubwa wote ni wezi hivyo na wao wakaamua kubeba silaha kuvamia mabenki mchana kweupe.Utawala wa CCM hauna tofauti na majambazi hawa tena huu ujambazi wa CCM umevunja rekodi kwani wamevamia Benki kuu ,kasi mpya ari mpya .Mungu hayupo pamoja na utawala huu ndio maana ukaona kila kitu kinakuja juu na wahusika wanaumbuka ,hii ndio faida ya jambo linalopatikana kwa dhulma ,Mwenye Kudhulumu hajizidishii kitu isipokuwa hasara tu ,Kikwete anaelewa maana ya maneno hayo kwa kina kabisa, toka achukue madaraka ni hasara tu anayohesabu hakuna faida.

  CCM ni genge la majambazi walio hatari sana maana wanaogopana wao kwa wao ,kila mmoja ni mbabe akijua ana siri ya mwenzake amebeba na anaijua kwa kina ,hivyo atakalo fanya hana wa kumzuia au watazama wote na ndio siri hizo zinavyoanza kumwagika. Yule Rostam alijua kuwa hatozama peke yake lazima ataondoka na wengine wakiwemo walimo ndani ya utawala wa juu.
  Dondoo: Ninapomtaja Kikwete nakusudia utawala mzima wa CCM.
   
  Last edited: Feb 26, 2009
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Serikali sio imenywea bali imewekwa kwenye kona ,juhudi za viongozi wa vyama vya upinzani zinahitajika,mikutano ya nguvu inahitajika kwenye miji mikuu yote hapa Tanzania ,hakuna kulala na kusubiri Utawala wa CCM ujiweke sawa na kukurupuka ,they must wawekwe bize all the time.
  Ni lazima mikutano idumishwe mpaka kufikia uchaguzi mkuu tusiwawache CCM wajipange ,huu si wakati wa kuwasubiri watajibu nini watatengeneza nini ,vyama kibao vya upinzani viwe vinapishana mikoani na wilayani ,kunadi uzembe wizi na wezi ulioshamiri ndani ya utawala wa CCM ,mnajua ukitaka mwizi apate kisago usimnadie kwa mara moja tu ni lazima sauti yako iwe inatoka kwa kufululiza ,jamani mwizi huyoo x infinity ndipo utakapoweza kuvutia watu na kukupa msaada wa nguvu na hatimae kumkamata au kumpa kisago mwizi na huu ni wakati wa kumnadia mwizi wetu ambae tumeshamuona ameiba BOT ,hivyo kilichobaki ni kupaza sauti hadi WaTanzania wote waweze kujumuika ili kumkamata na kumpa kisago mwizi huyu mambo ya kwenda na mwizi mmoja mmoja watatuponyoka,hapa Mwizi ni CCM tu hakuna mwingine mambo ya kutuambia tumkamate mmoja mmoja yanatupotezea wakati, natumai nimeeleweka
   
 10. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndio maana huwa nahisi kuwa pesa zote za EPA hazijarudishwa. Sidhani kuwa kuna cent hata moja iliyorudi popote (Mungu anisamehe kama nimekosea).

  Wapinzani wanatupa wakati mgumu sana kuamua. Yaani hata tukiwa tunataka kuchagua mbadala inashindikana katika hali kama hii. CHADEMA, CUF amueni wananchi wachague nini 2010. Mimi nitawaunga mkono, maana hii sio dalili ya matumaini hata kidogo (acha iwe mbaya kabisa).

  Kinachohitajika sio kukaa na kusema hapa JF tu. Bali ni kuamua, kujipanga na kuwafikia wananchi na kuwaeleza ukweli. Nchi inaliwa. Waliwahi kusema, usipoliwa hutaliwa (sijui walimaanisha nini wallah).
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Karibu wataizima JF ,hivi karibuni alisikika mamluki mmoja akimshauri Raisi kuwa asiwache vyombo vya habari kubwabwaja.
   
 12. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Asante mtoa hoja.

  Serikali iliyopo Madarakani ni kagoda products. Kuipeleka Kagoda mahakamani ni sawa na kuipeleka serikali iliyopo madarakani mahakamani. Na kama itafikishwa mahakamani kosa litakuwa ni kununua kura za wananchi kwa fedha za wizi toka BOT (Pesa za wananchi) na kwa kosa hilo serikali iliyopo madarakani itakuwa ni batili. Kwa mantiki hiyo Kagoda haitapelekwa mahakamani mpaka mwisho wa dunia. Beredi Malegesi na Rostam Aziz wanajulikana kwamba wamechota pesa za EPA, kwanini mpaka leo hawajakamatwa kama wezi wengine wa EPA?, hawa watu wawili ni kiungo kikubwa sana katika wizi huu kati ya wezi na serikali.
  Kama kweli watanzania tumechoka na uchafu huu basi ni bora na muhimu kuungana kwa pamoja bila woga na kuukana uchaguzi wa mwakani. kukubali kwenda kwenye uchaguzi kwa kutumia katiba iliyopo ni kuipa CCM ushindi.
   
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Changamoto ya kudai Katiba mpya kwa kupitia bungeni haitafanikiwa ,ila kwanza inahitajika kuanzisha mtafaruku huo hapo bungeni na baadae upelekwe kwa wananchi ,makelele ya kumnadi mwizi yaanzie bungeni na kuendelea kelele hizo kusikika nje ambako kutapatikana uungwaji mkono wa kumsaka na kumkamata mwizi.

  WaTanzania tumejifunga na KATIBA ya Chama kimoja ya CCM ,na vyama vya upinzani bungeni naona bado havijaamua kulivalia njuga suala hili ,na kulipa kipau mbele wala sijui wanasubiri kitu gani,maana inaonekana siku watakapo livalia njuga wataambiwa muda hauturuhusu kwa uchaguzi upo karibu hivyo tupishe uchaguzi halafu ndio tutaanza,kwa kweli kwa upande mwengine wabunge wa upinzani wanaonyesha kama wana woga au hawajiamini kulivalia njuga suala hili ,maana hapa tulipofikia kwa kweli suala la Katiba ni jambo muhimu kabisa na bila ya kubadilisha Katiba hii ili iendane na mfumo wa vyama vingi itakuwa ni kuwasumbua wananchi kuwapeleka kwenye misururu ya upigaji kura ni kuwadanganya wananchi wanaowaunga mkono upinzani maana hakuna udhibiti wa matokeo, tume nzima ya uchaguzi inaendeshwa na CCM ,unategemea nini ,hivyo wabunge hawana budi kutoa kauli yao ya pamoja ili kuilazimisha serikali kubadili Katiba na mambo yote muhimu hata ikibidi uchaguzi uchelewe basi ni bora mara milioni kuliko kuingia kichwakichwa kwenye uchaguzi.
   
Loading...