Serikali imefuta mchakato wa kutangaza ada elekezi kwa shule binafsi

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
SERIKALI imefuta mchakato wa kutangaza ada elekezi tangu katikati ya Mei mwaka huu, ambapo udhibiti wa ada hizo sasa utafanywa na Kamishna wa Elimu na Idara ya Ukaguzi. Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo jana jioni alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara hiyo na kuongeza kuwa mchakato huo umefungwa baada ya kujadiliana na wamiliki na Kamati ya Bunge.

Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, usimamizi wa utoaji wa michango na ada holela katika shule hizo utashughulikiwa kwa mujibu wa sera, ambapo kutatakiwa kuwepo kwa kibali kwanza. Alisema kutokana na hatua hiyo ya Serikali, ambayo inalenga kupata muda wa kutafakari suala hilo na kutafuta namna bora ya udhibiti, sasa hakutakuwa na ada elekezi ila michango itadhibitiwa.

Awali katika mjadala, baadhi ya wabunge walipinga mchakato huo na kutaka Serikali kujikita katika kuboresha shule zake na kuachana na utoaji wa ada elekezi. Akizungumza katika mjadala huo, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM) alisema hakuna sababu ya kuwa na ada elekezi kwa shule binafsi. Lugola alisema kama Serikali ikitaka shule binafsi zife, ni kuwalipa vizuri walimu wake, kuwajengea nyumba zao, kuwa na madarasa na kuweka chakula na hayo yakikamilika, hakuna mtu binafsi atakayepandisha ada.

Kwa mujibu wa Lugola, kama hayo hayatafanyika, kila mtu ana uamuzi wa kumpeleka mtoto katika shule anayotaka hata Ulaya. “Kuna tatizo gani na hizi shule za binafsi? Kwanza wamerundikiwa kodi nyingi mara kupaka rangi magari na mengineyo, sasa watarudishaje hizo fedha? Ndiyo maana wanatoza ada kubwa,” alitetea.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Zubeda Hassan (CHADEMA), alielezea kushangaa ni kwa jinsi gani ada elekezi itawekwa, wakati hakuna viwango vya utoaji elimu kwa watoto.Mbunge wa Maswa, Mashimba Ndaki (CCM), alisema suala hilo la ada elekezi watakaonufaika ni watu wenye fedha kwani ndiyo wanaowapeleka watoto katika shule binafsi na kusahau kuboresha shule za Serikali ambazo ni kwa watu wenye vipato vya kawaida.

Ndaki alisema iwapo shule za Serikali zingekuwa bora, zingechukua wanafunzi wote na zile za binafsi zingekosa wateja kwa gharama zao hizo kubwa, hivyo hakuna sababu ya kuwawekea ada elekezi. “Shule binafsi wanapata wateja kutokana na miundombinu mibovu, matatizo ya walimu yanayotokana na kutotendewa haki katika shule za Serikali tofauti na shule binafsi ambazo wanawathamini walimu na kufanya watoe elimu bora,” alisisitiza.

Alitaka waziri, badala ya ada elekezi angekuja na mkakati madhubuti wa kuboresha shule za Serikali kwa kuwapa mahitaji yao walimu, kununua vitabu mashuleni na kuboresha miundombinu na shule hizo na hilo lingesababisha wapunguze wenyewe ada zao. Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Mahawe (CCM) alisema Sheria ya Elimu ya 1978, inasema elimu siyo biashara bali huduma, lakini sasa wanaotoa elimu hiyo binafsi wanaonekana kama wao ni maadui.

Alisema shule binafsi, zinasaidia kusomesha Watanzania lakini bila kuthaminiwa wakati nchi nyingine watu binafsi wanasaidiwa kuwalipa mishahara, hapa nchini wanawapiga chini licha ya kuwa wanasaidia kusomesha hata watoto yatima, ili kuondoa watoto wa mitaani huku akieleza yeye katika shule yake anasomesha watoto 67. Mahawe alisema shule binafsi wanalipa kodi zaidi ya 10, licha ya kuwa wameokoa kupeleka watoto kusomeshwa katika nchi za Kenya na Uganda huku akiomba wizara kuwapatia dawati wizarani ili wawape ushauri hususan katika mitaala.

Mbunge huyo alilalamikia shule binafsi kutengwa na wizara kwani hivi karibuni walitoa mafunzo kwa walimu wa watoto wa darasa la kwanza mkoani Dodoma bila kuwashirikisha.
 
kabla ya ada elekezi, kuwepo mkakati wa kuweka viwango vya utoaji elimu katika shule zote. masuala ya ukubwa wa ada iwe ni kwenye huduma nyinginezo kama vile ubora wa chakula, mazingira ya nje ya shule nk
 
Ingefanyika tathmini ni wabunge wangapi wanamiliki shule ili kuondoa kitu kinachoitwa mgongano wa kimaslahi.....!!

Kama ni kweli basi Ndalichako kashapigwa bao hapa...mwenye kumiliki shule hawezi kumtetea mwananchi ambaye ndiye ng'pmbe wake wa kumkamua.

Chukulia mfano wa Nauli za mabasi au mafuta...kuna logic gani ya kuregulate nauli za mabasi na bei za mafuta halafu inapokuja kwenye ada za shule tena za sekondari na msingi ushindwe kufanya hivyo?

Mbona vyuo vikuu kuna ada elekezi??
 
Wabunge wengi wana maslahi binafsi na hizi shule binafsi. Pia kuna wapiga deal kama akina Kangi Lugola ambao ni wepesi kupokea mkwanja then wakashupalia hoja kutetea yasiyoteteleka
chalii,kifo cha mende,ndembe ndembe!
Magufuli 0-3 TeamSukari na TeamAda Elekezi!
 
Hakuna mantiki ya ada elekezi,sijui waliokua wanawaza hayo walikua na akili gani maana nilipinga ujinga huo tangu mwanzo.Ukichukua bajeti nzima ya wizara ya elimu ukigawa na idadi ya wanafunzi unakuta serikali inatumia zaidi ya miln 2 kwa mwanafunzi wake kuliko private schools na bado public education ni poor kuliko private
 
Tatizo hawa wabunge wetu wanadhani shule binafsi ni kwa ajili ya watoto wenye wazazi wenye uwezo. Wanasahau kuwa wanafunzi wengi wanakosa nafasi katika shule za umma na wazazi wao maskini wanategemea wawapeleke katika shule hizi za binafsi. Wanasahau wao ndio kila siku hushinda au wanapeleka vimemo wizarani kuomba na kushinikiza watoto wao na wa ndugu zao wahamishiwe shule wanazotaka wao hali mlala hoi hana nafasi hiyo.

Shule binafsi sio kimbilio la wenye uwezo tu, bali hata mlala hoi ambaye mtoto wake hakuchaguliwa kujiunga na shule za umma angependa mtoto wake andelezwe kielimu katika shule binafsi na hawa ni wengi zaidi kuliko watoto wa viongozi na matajiri
 
Tatizo hawa wabunge wetu wanadhani shule binafsi ni kwa ajili ya watoto wenye wazazi wenye uwezo. Wanasahau kuwa wanafunzi wengi wanakosa nafasi katika shule za umma na wazazi wao maskini wanategemea wawapeleke katika shule hizi za binafsi. Wanasahau wao ndio kila siku hushinda au wanapeleka vimemo wizarani kuomba na kushinikiza watoto wao na wa ndugu zao wahamishiwe shule wanazotaka wao hali mlala hoi hana nafasi hiyo.

Shule binafsi sio kimbilio la wenye uwezo tu, bali hata mlala hoi ambaye mtoto wake hakuchaguliwa kujiunga na shule za umma angependa mtoto wake andelezwe kielimu katika shule binafsi na hawa ni wengi zaidi kuliko watoto wa viongozi na matajiri
mkuu,hao walala hoi hawaja katazwa kutafuta hela ya kuwapeleka watoto hao ktk shule za binafsi...tusitake kila mmoja aishi kama shetani
 
mkuu,hao walala hoi hawaja katazwa kutafuta hela ya kuwapeleka watoto hao ktk shule za binafsi...tusitake kila mmoja aishi kama shetani
Ndiyo maana tuliomba ada elekezi ili tuweze kuzimudu, kupandisha ada kwa kudhani kila anayeingia private school ni tajiri. ada elekezi haikuwa lazima iwe sawa kwa shule zote wangalipanga hata madaraja ya shule mzazi aamue kumpeleka wapi kulingana na uwezo wake. Tumeweza kupanga madaraja kwenye usafiri wa mabasi ya kwenda mikoani, tungeweza pia kwenye shule binafsi.
 
mkuu,hao walala hoi hawaja katazwa kutafuta hela ya kuwapeleka watoto hao ktk shule za binafsi...tusitake kila mmoja aishi kama shetani
Tatizo lako unafikiria shule binafsi kwa muktadha wa Fedha Schools na sio hizi binafsi tunazoziona huku uswahilini.
 
Alitaka kuchezea biashara ya kanisa! Ameishia kuigungia Al -Muntazir tu, coz wao ni lile tabaka la pili la nchi! Hawezi kuzigusa "saints"


Shukrani kwa waziri wa elimu kusikia kilio na kufuta ada elekezi, ni vizuri sasa kuboresha shule za serikali na hivyo vya private vitajifia vyenyewe au vitashusha ada baada ya kukosa wateje
 
Ndalichako kashafeli for this issue..!! ❌❌❌❌❌❌❌❌❌❌⁉✖

Kumbe she is very WEAK katika kujenga hoja..!! Very weak... !! Wabunge wengi ni wamiliki wa shule binafsi... so IKO WAZI WATAPINGA ADA ELEKEZI KWA NGUVU ZOTE... SBB WANAKAMUA KABISA WANANCHI, ADA ZAO NI LAANA...!!

Oooh Ndalichako, very weak.. sikutegemea awe hivyo...!! ❌❌❌❌‼‼

Ada za shule zote hadi BINAFSI LAZIMA ZIWE REGULATED...lazima ADA elekezi iwepo...!! Lazima..!!

Wakati wa kampeni Rais Magufuli aliahidi sana KUZI CONTROL HIZI SHULE KTK ADA NA MICHANGO... just 6 months now, WAZIRI WA ELIMU anaonekana kushindwa vibaya kwenda na KAULI YA RAIS ya wakati wa kampeni...!!

Shule zinatoza 6 Mil kwa mwaka, zingine 15 Mil... zingine hadi tshs 60 Mil.. while UNIVERSITY ADA PEKEE is just tshs. 1 Mil...!!

Hapa tayari SERIKALI YA MAGUFULI imefeli swala hili la ELIMU...!! Hv kuna nn nchi hii..?

Wabunge ndio waharibifu wakubwa sana ktk nchi hii...

Hili swala lazima Rais aamue mwenyewe...sbb naona hakuna utekelezaji... KAMA VYUO VIKUU VINGI ADA HAIFIKII tshs 2 mil... iweje shule za sekondari ADA iwe zaidi ya tshs 2Mil...?

Lazima serikali IJE NA ADA ELEKEZI... NA TULISEMA ISIZIDI Tshs 2 Mil... asiyetaka anaacha...!! ELIMU NI HUDUMA muhimu sana SIO BIASHARA...!! Asiyetaka akafungue shule KENYA AU UGANDA...!!!

Ndalichako FAILED here..❌❌❌❌❌❌❌❌❌
 
Tunayaona tuliyosema hayawezi tokea yakishindikana zaidi, nchi inaliwa na wenye akili mingi hii....
Hivi inawezekanaje shule moja ada mill 7 na nyingine bure....alafu useme wanapata elimu sawa na uwafanyie majaribio sawa.....
Ada elekezi ilikuwa muhimu lakni kwa impulse ile ni dhahiri ingebuma tu.....wana CCM wengi ndio wahujumu wakubwa wa mfumo wa elimu yetu...ona wachangiaji wengi wa hoja hiyo bungen ni wenye maslah binafs na shule hizo......
Tunaharibu wenyew kisha tunatafuta wa kulaumu....
 
Back
Top Bottom