Serikali imefilisika?

Mto wa mbu

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2021
Posts
4,515
Reaction score
11,383
Mwaka wa fedha 2021/2022 serikali ilipanga kuongeza watumishi idara ya Elimu ili kuinua kiwango Cha Elimu nchini

Mwezi October Ummy Mwalimu alisema serikali itaajiri walimu elfu 10, kabla ya December, mpaka mwaka unaisha hakuna Mwalimu aliyeajiliwa

Leo Waziri Bashungwa kasema wameomba kibari Cha kuajiri walimu elfu7, yaani kwenye bajeti walisema wataajiri elfu 10,, sahivi wanasema ni elfu 7, tumebaki na miezi 5 kumaliza mwaka wa bajeti.

Unajenga madarasa kwa mkopo, yapatayo elfu15 afu unaajiri walimu elfu7, je serikali haina hela za kuajiri walimu wa kufundisha watoto wetu? Kama hela zipo why wapunguze idadi ya kuajiri from elfu 10 to elfu7?

Ebu tujibu nyie watu wa CCM
 
Hebu subiri hao 7000 waajiriwe kwanza usitupre-empty matumaini hao 3000 ni wachache kuliko watakaoajiriwa if the plan is successful. Then baada ya hapo tutauliza waseme wamefeli au wataajiri, but at least watakuwa wameajiri zaidi ya asilimia 70 ya matarajio which is okay as long wanaendelea kuajiri serikali so ndio hii hii au?
 
Oky viajira uchwara watoto wetu hawafundishwi,,, afu unasema ajira elfu 7 zinatosha
 
Sina Imani na hii nchi kwa kweli ,ni uhuni uhuni tu unaendelea huko juu ...
 
Hi nchi propaganda zimezidi, waziri anaweza kudanganya bila hofu kwa sababu hatuna ustaarabu wa kuwajibika
Subiri Kwanza upate hata hao elfu saba (7,000) ndio uhoji 3,000
 
Mhhh mkuu ajira inahitaji pesa,kumbe kuna walimu wakujitolea,wale wakujitolea inabidi wawe wa kwanza kuajiriwa.
Kama tuko serious na elimu hata elfu 10 ni idadi ndogo haikidhi matakwa ya taifa.Wapo wahitimu walimu zaidi ya laki mmoja wapo mitaani wengine miaka 5.
 
Jibu limeenda shule hili. Asante
 
Wapo wahitimu walimu zaidi ya laki mmoja wapo mitaani wengine miaka 5.
Lengo la serikali kuajiri ni kuondoa tatizo la upungufu wa watumishi na siyo kuhakikisha wahitimu wote wanapata kazi.

Wahitimu watumie elimu na maarifa waliyoyapata ktk masomo yao kujiajiri
 
Maswali mengine Ingekuwa Bora kwa wahusika serikalini waje humu kujibu
 
Lengo la serikali kuajiri ni kuondoa tatizo la upungufu wa watumishi na siyo kuhakikisha wahitimu wote wanapata kazi.

Wahitimu watumie elimu na maarifa waliyoyapata ktk masomo yao kujiajiri
Mbona hueleweki, kama lengo ni kuhakikisha wote wanapata kazi kwanini idadi ipunguzwe?
 
Cha kushangaza kuna wahitimu wa fani ya ualimu zaidi ya elfu 90 mtaani! Halafu wanataka kuajiri Walimu elfu 7 pekee! Na kati ya hao 7000 unakuta kuna ndugu zao humo humo, kuna watakao toa rushwa!

Wakati huo huo vyuo vikuu na vile vya kati navyo vinaendelea tu kudahili wanafunzi kutoka familia masikini (maana hakuna mtoto anayetokea familia inayo jiweza, anaye jiunga na chuo kusomea ualimu) kusomea masomo ya ualimu!

Hakika huu ni udhaifu mkubwa sana kwa serikali ya ccm.
 
Subiri mwezi wa 6 wewe
 
Kuna chawa wa mama ndo huwa wanasifia hivyo vitu kwa nguvu,sasa waulize walete majibu nini kilitokea kutoka elfu kumi na kuomba elfu saba.
Wengune tunasubili mzunguko wa fedha ili tuendelee kufanya biashara kama zamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…