Serikali imeaibika sana kwa hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali imeaibika sana kwa hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyumbu-, Mar 11, 2011.

 1. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Wanajamvi,

  MCT (Media Coucil of Tanzania), imetoa hukumu ya haki kwa gazeti la Mwananchi dhidi ya serikali. Kwa ufupi , ni kwamba serikali ililitishia gazeti la Mwananchi kufungiwa eti kwa kuandika habari za uchochezi dhidi ya serikali wakati wa kampeni za uchaguzi.
  MCT, pamoja na mambo mengine, wanahitimisha kwa kusema , serikali iliyanyamazia kwa makusudi magazeti yaliyokiuka maadili kwa kuandika habari za udhalilishaji, na badala yake ikayaandama magazeti kama Mwananchi yaliyoandika habari kwa weledi mkubwa. Japo hakutaja ni magazeti gani hayo yaliyoandika mbofumbofu, mimi nafikiri alimaanisha Daily news na Habari leo na vikaragosi vyao vya Rai.... Soma ripoti hii hapa chini ujilidhishe.....Honagera Jaji Kisanga , you are always a hero...maaana nakumbuka hata wakati wa Mkapa, ulitoa maoni ambayo hayakumpendeza Mr. Clean...lakini ukweli wake u wazi leo zaidi kuliko wakati ule. Thanks


  Serikali haikulitendea haki gazeti la Mwananchi
  Kamati ya Jaji Mstaafu, Robert Kisanga, baada ya utafiti wake imemetoa taarifa inanyoonyesha kuwa serikali haikulitendea haki gazeti la Mwananchi kwa kulitolea vitisho vya kulifungia mwaka jana. Soma muhtasari wa taarifa hiyo kama ulivyosomwa kwa waandishi wa vyombo vya habari Februari 9,2011 jijini Dar es Salaam.
  ---------------------- Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Ripoti ya Kamati Maalum ya Kuchunguza Tuhuma na Tishio la Serikali Dhidi ya Gazeti la
  [FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Mwananchi [/FONT][/FONT]na Jinsi Lilivyoripoti Habari za Uchaguzi Mkuu 2010

  [FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]
  Ndugu Wanahabari, Habari za asubuhi na karibuni hapa Baraza la Habari Tanzania. ​
  Mnamo tarehe 20 Oktoba, 2010 Baraza la Habari Tanzania (MCT) lilipokea barua kutoka kwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), ikiwa na kichwa cha habari kilichosomeka: ​
  [/FONT]​
  [/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]"Vitisho vya Serikali dhidi ya Gazeti la Mwananchi". [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Katika barua hiyo, Mhariri alidai kuwa Serikali ilikuwa imetishia kulisimamisha na hata kulifungia kabisa gazeti hilo kama lisingesitisha mara moja kuchapisha habari zenye mwelekeo wa ‘uchochezi’ na ‘kuidhalilisha’ serikali. Mhariri alisema kwa kuwa [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Mwananchi [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]hawakuamini kuwa walikuwa wakichapisha habari za namna hiyo, walimwandikia Msajili wa Magazeti barua wakimwomba awape ushahidi au mifano ya habari na picha za aina hiyo ili waweze kujua hatua za kuchukua. Hata hivyo, Mhariri katika barua yake alisema badala ya kupewa mifano waliyoomba, Msajili aliwaandikia onyo kali na kutishia kulifungia gazeti hilo ikiwa lisingeacha mwenendo wake hasi dhidi ya Serikali. Baada ya hatua hiyo ya Serikali, Mhariri Mtendaji wa MCL alifikisha rasmi maombi kwa Baraza la Habari Tanzania akiliomba liunde

  kamati, kwa mujibu wa Katiba ya Baraza na taratibu zake, ili kuchunguza madai hayo mazito ya Serikali dhidi ya Mwananchi. Bodi ya Baraza la Habari (MCT) ilikutana Novemba 18, 2010, kuzungumzia pamoja na mambo mengine, maombi ya MCL. Bodi ilijiridhisha kwamba shauri hilo liligusa maslahi ya umma na uhuru wa vyombo vya habari na hivyo lilihitaji kuundiwa kamati maalum itakayochunguza madai hayo kama ilivyoainishwa katika Katiba ya MCT. Hivyo basi, Bodi ilinishauri kuunda kamati hiyo. Nami nilikubali. Mnamo tarehe 26 Novemba, 2010, niliteua wajumbe watatu ambao ni Profesa Luitfried Mbunda, Bi. Gemma Akilimali na Bw. Attilio Tagalile ili kuunda kamati maalumu ya kuchunguza tuhuma na tishio la Serikali dhidi ya gazeti la
  [/FONT]
  [/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Mwananchi [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]na jinsi lilivyoripoti habari za uchaguzi mkuu wa 2010 kwa mamlaka niliyopewa na kifungu 23(1) cha Katiba ya Baraza la Habari Tanzania. Moja ya malengo ya Baraza la Habari Tanzania kama ilivyoainishwa katika katiba yake Kifungu cha 3(e) ni kama ifuatavyo: "Kuweka jalada la matukio yanayoweza kukwaza usambazaji wa habari za maslahi kwa jamii, kulihuisha jalada hilo, na kuchunguza matendo ya watu mmoja mmoja, mashirika au vyombo vya serikali, katika ngazi zote, yanayolenga vyombo vya habari, na kuweka hadharani taarifa za chunguzi hizo". Niliiagiza kamati ya uchunguzi kuangalia ikiwa madai ya serikali dhidi ya [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Mwananchi [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]yana uhalali; pili kuangalia kama tishio la serikali linaingilia isivyostahili uhuru wa vyombo vya habari na wa uhariri; na tatu kuchunguza ikiwa uandishi na mwenendo wa gazeti la [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Mwananchi [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2010 vilikiuka [/FONT][/FONT]Mwongozo wa Maadili Katika Kuripoti Habari za Uchaguzi Mkuu 2010. [FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Pia Kamati iliangalia kama uandishi na mwenendo wa [/FONT][/FONT]Mwananchi [FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]ulikiuka [/FONT][/FONT]Kanuni za Maadili kwa Waandishi wa Habari. [FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Jana, Februari 8, 2011, Kamati Maalum iliwasilisha ripoti kwangu na kwa Bodi ya Baraza. Kwa ufupi, ifuatayo ndiyo ripoti ya uchunguzi wa kamati: Kwa mujibu wa watu wengi waliohojiwa na Kamati Maalum, gazeti la Mwananchi liliripoti kwa haki na usawa kwa vyama vyote ikiwemo chama tawala CCM . Watu hao walitoa maoni kuwa tishio na tuhuma za serikali dhidi ya gazeti la Mwananchi ni la kisiasa na si

  vinginevyo, ukichukulia kwamba utendaji wa kazi wa gazeti ni wa hali ya juu na unaofuata weledi ukilinganisha na magazeti mengine mengi. Wengi wa waliohojiwa pia hawakuwa na shaka kwamba tuhuma na tishio la serikali dhidi ya
  [/FONT]
  [/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Mwananchi [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]ni ukiukwaji wa haki ya uhuru wa habari. Kamati ilibaini kwamba tuhuma na tishio la serikali dhidi ya [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Mwananchi [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]viliingilia isivyostahili uhuru wa habari na wa kutoa maoni, na Kamati iliona kwamba tuhuma hizo zilitishia maslahi na uhai wa gazeti la [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Mwananchi. [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]Vilevile Kamati Maalum iligundua kwamba kuna baadhi ya magazeti yalioonywa na Serikali kwa lugha isiyo kali licha ya kwamba yalichapisha madai hasi mazito. Pia Kamati Maalum iligundua kwamba kuna baadhi ya magazeti ambayo yalikuwa yakishapisha tuhuma nzito lakini badala yake serikali iliwaalika kwa majadiliano. Kwa hili Kamati Maalum iliona kwamba hakukuwa na uwiano sawa. (yaani kulikua na [/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]double standards[/FONT][/FONT][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]). Kamati Maalum imependekeza kwamba kabla ya kuchukua maamuzi yoyote ambayo yataminya uhuru wa chombo cha habari, ni muhimu kufuata kanuni ya kumpa mtuhumiwa haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa. Vilevile Kamati Maalum ilipendekeza kwamba sheria mbaya zinazokandamiza uhuru wa kutoa habari na maoni zirekebishwe au kufutwa kabisa. Kwa upande mwingine serikali iwezeshe kuundwa kwa sheria ambazo ni rafiki kwa vyombo vya habari kama ambazo wadau wamezipendekeza. Bodi ya Baraza imeridhika na inaridhia ripoti ya Kamati Maalum . Bodi inakubali hitimisho na mapendekezo ya Kamati na itayafanyia kazi zaidi. Taarifa nzima ya Kamati Maalum itachapishwa hivi karibuni kwa manufaa ya umma.
  Jaji Dk. Robert H. Kisanga
  [/FONT]
  [/FONT]Rais, Baraza la Habari Tanzania

  [FONT=Book Antiqua,Book Antiqua][FONT=Book Antiqua,Book Antiqua]
  February 9, 2011 ​
  [/FONT]
  [/FONT]
   
Loading...