Serikali ilimpenda, ilimchukia au ilimuogopa Reginald Mengi?

Serikali ilimpenda, ilimchukia au ilimuogopa Reginald Mengi?

Afrika ukifanikiwa unapewa kesi za kijinga,mara kesi ya utakatishaji pesa,mara madawa ya kulevya.sasa cjui tunataka wahindi na wazungu ndio wafanikiwe.serikali zenyewe zinachangia kurudisha nyuma watu wake.Ngozi nyeusi ina taabu sana
 
Hapa unapata Picha kumbe ukiwa TAJIRI hii nchi unatakiwa uwe makini kuliko kitu chochote,la sivyo utapotea na ndipo naamini sasa Kesi zinazoendelea huko mahakamani kuhusu hawa matajiri nyingi ni chuki za serikali na kukomoana.
 
Nasikia siku za mwisho Mengi alitaka kuanzisha viwanda vya kutengeneza simu. Na JPM alimuunga mkono mia kwa mia.

Mengi hakumjua vyema JPM enzi zile akiwa waziri, hakujua kuwa alikuwa akimuunga mkono mtu kama Kafulila ambaye alikuwa mwiba wakati wa awamu ya nne.

Mtu mwenye fikra za ndani kabisa za kibiashara ni vigumu kuwa na mapatano na CCM ambayo msingi wake mkuu ni ujamaa uliojazwa vichwani mwetu na mawazo ya Mwalimu Nyerere kwamba ubepari ni unyama.
 
Watu walikua wanaitikia tu,zidumu fikra za mwalimu,ila wajanja walishtuka walionanatupeleka kwenye umasikini.
 
Ukweli tangu tupate uhuru serikali zote hakuna ambazo zimewahi kumjali mfanya biashara mzawa mweusi. Zote zimekuwa zikiweka mazingira ya kupendelea wageni. Haya yaliyomkuta Mengi yanathibitisha hilo.

Ni wakati sasa serikali kuweka juhudi ya kuinua wafanya biashara wazawa wanaoweza kuja kuwa wachangiaji wakubwa wa uchumi kuliko hawa wahindi wanaweka hela Canada na Uswis

Ni kwa kuwa wageni wanatoa 10%
 
Hao waliokua wanampinga akina malima,ndio waliokua mstari wa mbele kumuaga nao wana majonzi,wkt yupo hai walimpinga.binadamu ni shida sana

..ccm walikuwa wanamlaani in public.

..lakini privately walikuwa omba-omba kwake na wakipokezana kwenda kumchomoa pesa zake.

..ccm walimchukia kwasababu alikuwa akifadhila watu wengi hata wapinzani, ila hawakuwa na jinsi kwani na wao walihitaji fedha zake.
 
Ukweli tangu tupate uhuru serikali zote hakuna ambazo zimewahi kumjali mfanya biashara mzawa mweusi. Zote zimekuwa zikiweka mazingira ya kupendelea wageni. Haya yaliyomkuta Mengi yanathibitisha hilo.

Ni wakati sasa serikali kuweka juhudi ya kuinua wafanya biashara wazawa wanaoweza kuja kuwa wachangiaji wakubwa wa uchumi kuliko hawa wahindi wanaweka hela Canada na Uswis
Yaan hata kabla hawajaipeleka canada hela yao haichangamani na ya sis waswahili, Angalia; Wana hospital zao, wana shule zao, Wana garage zao, wana maduka yao, wanapharmacy zao, hawapandi daladala, mtoto akifika ngazi ya chuo kikuu anapelekwa india na canada na hii ni kwa vile hawana chuo kikuu hapa nchini cha fan wanayoitaka, wana benki zao, nk
 
Na kitabu kama hiki cha Mzee Mengi kilitakiwa ndio kiwe kinatumika huko mashuleni(literature review) maana kinaelezea mazingira/changamoto halisi za kitanzania na kinaamsha ari/udadisi wa wanafunzi.

Sio vile vitabu vya kikuda kikuda sijui Song of lawino,3 suitors 1 husband.

Lkn kwa vile tunapendelea elimu yetu ya hapa na pale ngoja tuendelee kusoma 'Hawa the bus driver'.
 
..mkoloni aliwabana wazawa wasiingie ktk shughuli za biashara.

..baada ya kupata uhuru likaja AZIMIO LA ARUSHA ambalo nalo liliwabana wazawa wasiweze kufanya biashara kubwakubwa.

..vilevile azimio la arusha ndiyo chanzo cha mentality waliyonayo waTz walio wengi ya kumhisi vibaya na wakati mwingine kumchukia yeyote yule aliyefanikiwa kiuchumi.
 
Umenichekesha ulivyotafsiri neno "the spirit of success".. Yani umetafsiri kikatoliki na kiswaziswazi
 
KILIO kikubwa cha bilionea Reginald Mengi ni sera za Serikali kiuchumi. Mpaka amefariki dunia, amekuwa kielelezo cha mtu mwenye uthubutu wa kupinga utaratibu wa Serikali hususan utoaji fursa za uwekezaji.

Mwanzoni mwa miaka ya 1970, Mengi aliporejea nchini akitokea Scotland, alikokwenda kusomea shahada ya Uhasibu, alikuta nchi imeshashika usukani katika mfumo wa ujamaa. Na kwa vile ndoto yake ilikuwa biashara, aliona mazingira yalikuwa magumu mno.

Katika kitabu chake, "I Can, I Must, I Will; The Spirit of Success", kwa maana ya "Naweza. Lazima. Nitafanikiwa; Nafsi ya Mafanikio", anasema kuwa nyakati za ujamaa fursa zilikuwa chache na zilitolewa kwa upendeleo kwa Watanzania wenye asili ya Asia.

Anasema Watanzania weusi walidhibitiwa kufanya biashara na kufanikiwa kwa sababu walihofiwa kama wangekuwa na fedha nyingi, basi wangehodhi siasa za nchi kutokana na nguvu kubwa kubwa ya kiuchumi ambayo wangekuwa nayo.

Anatolea mfano alipoanzisha kiwanda cha vinywaji baridi cha Bonite Bottlers (Coca Cola), kwamba mwaka 1987, Mwalimu Julius Nyerere alikikosoa kwa maelezo kuwa malighafi zake zilitoka nje, kwamba huo ulikuwa ubepari.

Mengi anasema, kiwanda cha Fahari Bottlers Limited, kilianzishwa mwaka 1983, Nyerere akiwa madarakani, kikawa kinazalisha bidhaa za Pepsi, alikiruhusu kwa sababu kilikuwa cha Watanzania wenye asili ya Asia na Nyerere hakukikosoa.

Ukimsoma Mengi, utaona kwamba matumaini ya kufanikiwa zaidi kibiashara ni baada ya Rais wa Pili, Ali Hassan Mwinyi, kuingiza sera za ulibelari na kuruhusu kila mtu afanye anachoweza ilimradi asivunje sheria. Hata hivyo, alilalamika kuwa kipindi cha Mwinyi bado Mwalimu Nyerere alikuwa na nguvu sana.

Kipindi cha Rais wa Tatu, Benjamin Mkapa, uliibuka mgogoro mkubwa kati ya Mengi na aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji, Wilson Masilingi. Sababu ilikuwa uwekezaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, sasa inaitwa Hyatt Regency, The Kilimanjaro.

Mengi alitaka kuwa mwekezaji wa hoteli hiyo, lakini alinyimwa, wakapewa wawekezaji kutoka nje. Mengi aliishambulia Serikali kwamba haikuwa ikiwapa kipaumbele wazawa, na kupendelea zaidi wageni. Haya ni malalamiko ya muda mrefu ya Mengi.

Aliamini kuwa wazawa wanapaswa kupewa kipaumbele katika fursa za uwekezaji ndani ya nchi. Hata pale wazawa wangekuwa na uwezo mdogo, Mengi aliamini kwamba lilikuwa jukumu la Serikali kuwawezesha kufikia viwango vinavyokidhi uwekezaji husika.

Kipindi cha Rais wa Nne, Jakaya Kikwete, mara kadhaa Mengi aliingia kwenye mgongano na mawaziri. Zipo nyakati alituhumiwa kuihujumu Serikali ya Kikwete. Aliyekuwa mbunge wa Mkuranga, Adam Malima, aliwahi kumsema Mengi bungeni kuwa alitumia vyombo vyake vya habari kujitangaza kuliko Rais.

Hoja hiyo ya Malima ilisababisha mzozo mkubwa bengeni, huku Mengi akisimama imara kujitetea. Televisheni ya ITV ilirudia taarifa za Mengi na Rais Kikwete kuonesha kwamba Malima hakusema kweli. Mengi pia alimwandikia barua Spika Samuel Sitta kulalamika. Mwisho Malima aliomba radhi.

Wakati wa Kikwete, ukatokea mzozo kati ya Mengi na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba. Tuhuma zilitolewa na Sophia kuwa Mengi hakuwa mwana CCM na alikuwa anaihujumu Serikali, vilevile alimtuhumu kutaka kuwania Urais.

Mengi aliitisha mkutano na vyombo vya habari, akaonesha kadi zake za Tanu kisha ya CCM ya mwaka 1977. Akasema hajawahi kuwa na mpango wa kuwa Rais. Hata hivyo, ilikuwa dhahiri kwamba hakukuwa na kuaminiana kati ya Mengi na mawaziri wa Kikwete.

Uliibuka mvutano mwingine pale Mengi alipoitisha vyombo vya habari na kulalamika kwamba alipewa taarifa kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri, kwamba kuna waziri alipendekeza Serikali imfilisi Mengi mali zote.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, alimpa Mengi siku saba awe amethibitisha madai yake. Mengi akamjibu siku saba alizompa ni nyingi sana, kwamba siku moja ingetosha. Siku iliyofuata, mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, wakati huo akiwa mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alimtaja Masha kuwa ndiye alitoa wazo la kumfilisi Mengi kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri. Sakata hilo likaisha kimyakimya.

Hautasahaulika mzozo kati ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo dhidi ya Mengi. Mzozo ulihusu uwekezaji sekta ya madini na uvunaji gesi asilia. Muhongo alisema hakuna mzawa mwenye uwezo. Mengi aliamini wazawa wakipewa kipaumbele wataweza.

Aliwahi kufanya kikao na vyombo vya habari na kuelezea taarifa alizozipata ndani ya jeshi la polisi kuwa kulikuwa na mpango wa kumwekea dawa za kulevya mtoto wake ili kumkamata nazo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kuifanya jamii imuone yeye na familia yake ni wauza dawa za kulevya.

Mizozo hiyo ya mara kwa mara ambayo Mengi alikuwa nayo dhidi ya Serikali, na kwa kukumbuka kauli yake kwamba Watanzania wazawa (weusi), walianza kubaguliwa kwenye fursa za kiuchumi tangu wakati wa Nyerere, kwa hofu kwamba wangehodhi siasa na utawala, je, Serikali ilikuwa ikimuogopa Mengi au ilimchukia?

Pamoja na misimamo hiyo, Mengi aliwahi kuwa Mwenyekiti wa wa Bodi ya Magazeti ya Serikali (TSN), Kamishna wa Tume ya Mishahara (SRC), Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu Tanzania (NBAA), Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), Kamishna wa Tume ya Kupambana na Ukimwi (TACAIDS) na kadhalika. Nafasi hizo zote ni za kuteuliwa na Rais. Amekuwa akiteuliwa tangu wakati wa Nyerere hadi Kikwete. Je, Serikali ilimpenda?

Mengi hakufurahia mfumo wa Serikali kujigeuza dereva wa biashara badala ya kuwaacha huru wafanyabiashara. Aliumia kuuawa kwa vyama vya ushirika. Alisema, vyama hivyo viliuawa ili kuwafanya Watanzania weusi wasiendelee na kupata nguvu kubwa ya kiuchumi. Kwamba wangehodhi siasa.

Aliamini kuwa Watanzania wenye asili ya Asia walipendelewa na Serikali. Takriban muongo mmoja uliopita, alitaja majina matano ya wafanyabiashara Watanzania wenye asili ya Asia kuwa wanafilisi nchi. Aliwaita mafisadi papa. Je, Mengi alikuwa mbaguzi? Hakuwapenda Watanzania wenye asili ya Asia?

Tumuombee Mengi pumziko jema. Kila mja ni wa Mwenyezi Mungu na kwake ndipo yalipo marejeo ya lazima.

Ndimi Luqman MALOTO
Hata mimi naamini kama Mengi, ukiangalia kwa unakini utaona wafanyabiashara wa Kihindi na Kiarabu wanapata favour sana na wamekamata sana baadhi ya wakubwa na biashara zao zinakuwa tu, Mfano Akina Shubash Patel, Rostam Aziz na wengineo. Hafu ukiangalia wafanyabiashara weusi wao kila kukicha ni kusemwa au kuwekewa kodi kubwa nk, hata fursa za uwekezaji ni finyu sana.
 
Serikali inayo ongozwa na sera imara za ccm ni serikali inayo jali na kuheshimu wawekezaji wazawa nikiri kuna viongozi kazaa waliingia kwenye migogoro na wawekezaji wa ndani kwa manufaa yao binafsi laki serikali madhubuti ililiona na kuwashuhulikia mapema mfano ni hao ulio wataja,wengi wamepelekwa ubalozini na wengine wako bench,inatosha kusema we are on right truck.
Rostam je?
 
Yaan hata kabla hawajaipeleka canada hela yao haichangamani na ya sis waswahili, Angalia; Wana hospital zao, wana shule zao, Wana garage zao, wana maduka yao, wanapharmacy zao, hawapandi daladala, mtoto akifika ngazi ya chuo kikuu anapelekwa india na canada na hii ni kwa vile hawana chuo kikuu hapa nchini cha fan wanayoitaka, wana benki zao, nk
Kuna hizo bank 2, Bank of India na Baroda hatari sana kwa kupeleka pesa nje ya nchi
 
Na kitabu kama hiki cha Mzee Mengi kilitakiwa ndio kiwe kinatumika huko mashuleni(literature review) maana kinaelezea mazingira/changamoto halisi za kitanzania na kinaamsha ari/udadisi wa wanafunzi.

Sio vile vitabu vya kikuda kikuda sijui Song of lawino,3 suitors 1 husband.

Lkn kwa vile tunapendelea elimu yetu ya hapa na pale ngoja tuendelee kusoma 'Hawa the bus driver'.
Huwezi replace vitabu vya fiction na hii non-fiction ya Mzee mengi.
Vyote vyapaswa kuwepo.
Vitabu kama hiki cha mzee kinafaa kwa lessons za biashara (commerce and entrepreneurship)..
 
Sawa sawa tuendelee kutumia hivyo vitabu vya fiction maana si tunataka kua na jamii kubwa ya walimu wa arts huko mbeleni(application za kazi za ualimu mwaka huu ni 90,000 walioitwa kazini 4,000).

Tuendeleze ile elimu yetu ya hapa na pale.
Huwezi replace vitabu vya fiction na hii non-fiction ya Mzee mengi.
Vyote vyapaswa kuwepo.
Vitabu kama hiki cha mzee kinafaa kwa lessons za biashara (commerce and entrepreneurship)..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Joka kuu ume define vizuri. Chanzo cha roho ya kwann kati sis wenyewe kwa wenyewe ni hili azimio.
..mkoloni aliwabana wazawa wasiingie ktk shughuli za biashara.

..baada ya kupata uhuru likaja AZIMIO LA ARUSHA ambalo nalo liliwabana wazawa wasiweze kufanya biashara kubwakubwa.

..vilevile azimio la arusha ndiyo chanzo cha mentality waliyonayo waTz walio wengi ya kumhisi vibaya na wakati mwingine kumchukia yeyote yule aliyefanikiwa kiuchumi.
 
Mzawa anatakiwa asubiri kazi za serikali zitangazwe huko Tume ya utumishi,asubiri neema ya kuongezewa salary kwny mei mosi,aitwe kwny interview huko kwny viwanda vya MO huku requirement ni awe na degree na experience ya 3 yrs akalambishwe gross ya Tsh. 325,000 per month na mambo kama hayo.

Mambo ya kumiliki viwanda wanahisi kama vile mzawa hastahili kabisa.
Hata mimi naamini kama Mengi, ukiangalia kwa unakini utaona wafanyabiashara wa Kihindi na Kiarabu wanapata favour sana na wamekamata sana baadhi ya wakubwa na biashara zao zinakuwa tu, Mfano Akina Shubash Patel, Rostam Aziz na wengineo. Hafu ukiangalia wafanyabiashara weusi wao kila kukicha ni kusemwa au kuwekewa kodi kubwa nk, hata fursa za uwekezaji ni finyu sana.
 
Mzawa anatakiwa asubiri kazi za serikali zitangazwe huko Tume ya utumishi,asubiri neema ya kuongezewa salary kwny mei mosi,aitwe kwny interview huko kwny viwanda vya MO huku requirement ni awe na degree na experience ya 3 yrs akalambishwe gross ya Tsh. 325,000 per month na mambo kama hayo.

Mambo ya kumiliki viwanda wanahisi kama vile mzawa hastahili kabisa.
Wanasiasa wa chama tawala, wanaogopa kuona Watu weusi wa Tz wakimiliki uchumi, nachoshangaa kipindi cha uhujumu uchumi wahindi na waarabu hawakuguswa, ila weusi ndo walipata misukosuko wengine wakafungwa na kufilisiwa nchi ilikuwa na wafanyabiashara wengi wa kati lakini hadi leo ni maskini wa kutupwa na wengine walifariki
 
Wanasiasa ndiyo nduyo waliotufikisja kwenye umaskini tulionao, waliogopa vyama vya ushirika wakaviua kwa maslahi yao binafsi wote tuna kumbuka vile vyama hivi vilikuwa na nguvu kubwa ya kifedha .

Tuna kumbuka chama cha ushirika Nyanza kilikuwa kilishika nafasi ya nne au ya tano kiliwalipia ada watoto waliokosa nafasi za serekali, kiliwasomesha wataalamu vyuo kama makerere n.k

KNCU kilikuwa kinshika nafasi ya tisa kulisomesha watoto shule hiki ndicho kilimpeleka mengi UK kwenye masomo yake.

Hofu ya kisiasa ya kutaka kulinda maslahi yao wakaviuwa na ndipo umaskani na ufukara ukatamalaki nchini.
 
Back
Top Bottom