Danken Mbombo
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 651
- 339
Ni wazi Taifa letu halina walimu wazuri na wa kutosha katika masomo ya sayansi na hisabati. Walimu wazuri waliokiwepo ama wamestaafu, ama wamefariki na ama ndiyo wenye dhamana za uongozi. Shule nyingi za binafsi zimekuwa zikiwaleta waalimu wa masomo hayo toka nchi jirani kama Kenya na Uganda. Wakati serikali inafanya jitihada za kuongeza waalimu wa masomo hayo ingekuwa jambo la maana sana kama serikali kwa makusudi ingelegeza masharti ya kuingia nchini waalimu wa masomo ya sayansi na hisabati. Nchi nyingi duniani zinafanya mikakati kama hii kwa lengo la kijikwamua. Tusijifanye hatujakwama wakati ukweli tumekwama na tunahitaji mbinu za kujinasua. Haya ma-PhD yetu mengi hayasaidii kitu, yanatudidimiza tu na mitakwimu yao ya kwenye makaratasi: …. utasikia ooh kiwango chetu cha elimu kimepanda wakati ukweli elimu yetu ipo ICU.