Serikali ikikwama tuambiwe ukweli wananchi tuamue

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,725
Reaction score
17,222
Kuongoza ni kuonyesha njia (Nyerere). Hatima ya Tanzania iko kwa watanzania wenyewe, waelezwe wajue kama njia ya wanakotakakwenda ina mbigili, matope au changarawe ili wasijekuvisahau viatu vyao vinavyofaa kwa safari yao kutokana na kunyimwa taarifa na kiongozi wao. Kiongozi asitoe matumaini mema kwa watu wake kama hakuna matumaini, heri tuambiwe hali halisi ili kila mtu akadirie ugumu wa kazi iliyoko mbele yake. Wazungu walifika pale walipo kwa kuambiana ukweli wa mambo, watawala wao waliwaambia wao ni bora kuliko makabila mengine duniani, pamoja na hivyo wakawaambia watu wao kuwa na asiyefanyakazi na kulipa kodi ni adui wa taifa lao zima. Wagiriki waliitangulia dunia lakini watawala wao walikosea sana kwa kuwaficha kuhusu jukumu lao kwa taifa lao, ndiyo maana Wagiriki wa leo hawatishi tena kama mababu zao.

Sio siri tena, dunia imebadilika ghafla, hakuna wajomba tena wa kutusaidia kama zamani, wajomba wamejaa masharti mengi yaliyotufikisha hapa tulipo leo. Waliitumia misaada yao kwetu kama fimbo za kutuchapia hadharani mchana kweupe kwa kushirikiana na watawala wetu. Watawala wetu walikubali kupatiwa vioo vya kujiangalia ndevu zao za kipilipili kwa kubadilishana nao na milima ya dhahabu. Pamoja na kuondoka na almasi zetu lakini pia wanatudai madeni makubwa sana tusiyojua yametufanyia nini cha maana. Urusi, China na Marekani wakipatana hali yetu itakuwa mbaya sana, hakuna hata tone moja la msaada litatudondoea.

Viongozi wetu tusione aibu kutwambia pale mtakapokwama ili kuepuka ule usemi wa "waache waone wenyewe" na "mficha maradhi wacha asubiri kifo kimkute ili watu wajionee wenyewe"

Sisi wananchi nadhani hatujaandaliwa vya kutosha kuhusu safari tunayokwenda, ndiyo maana malalamiko ya chinichini ni mengi sana miongoni mwetu kuanzia watoto wa shule hadi wazee. Viongozi wetu hawatuelezi ila wanatutisha kwa matamko na kutupatia matumaini yasiyokuwa na formula ya kukokotolea. Baadhi ya majibu ya maswali yetu huwa yanatolewa bila ya kuonyeshwa formula iliyotumika kuyapata.

Hakuna mtu mmoja atakayekuwa na majibu ya maswali yote ya watanzania isipokuwa watanzania wenyewe, kazi ya viongozi itabakia kuwaunganisha na kuwaonyesha tu njia watakayoitumia kuyatafuta wenyewe majibu ya maswali yao.

Tunafahamu kuwa hakuna kiongozi asiyependa kupigiwa makofi, vigeregere na vifijo na watu wake, kila kiongozi angependa kuwafanyia jambo zuri watu wake ili wampigie makofi, ukiona kiongozi hawafanyii watu wake jambo hilo ujue lipo jambo linalosababisha asilitende. Wakati ni huu wa viongozi wetu kutueleza kama lipo jambo litakalokwamisha kukosa kugigiwa makofi na wafuasi wao badala ya kujikaza kisabuni. Kukiri nadhani sio udhaifu, bali kujifanya inawezekana kumbe imekwema ni udhaifu mkubwa.
 
sisi wananchi tulijitoa kushiriki kutoa maoni tume ya katiba wakatuona wajinga wakakaa dodoma wakajilipa maposho wakayazika maoni yetu, juzi kwenye uchaguzi tuliamua kuchagua yule tulimtaka wao wakatuletea wakwao, wamekwama tayari wanaogopa kurudi kwetu, kutuuliza kulikoni?? ipo siku watanyosha mikono
 
Tuelezeni ukweli msitutishe kwa kauli zenhu buuuaaaaaaaaaaana
 
Back
Top Bottom