Serikali ikikurupuka kwa hili Machafuko yataanza mara moja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ikikurupuka kwa hili Machafuko yataanza mara moja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Johnsecond, Mar 7, 2011.

 1. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nguvu ya watu iko pale pale msipojibu hoja za CDM, eti kwa kutumia dola mtaipeleka nchi pabaya sana. Mnachotakiwa ni kujibu hoja zao ili kuweza kuridhisha wananchi, cha kujiuliza ni hiki hapa, kama wananchi wangekuwa wanawasikiliza nyie basi wangejaaa saana kwenye mikutano yenu na wasingeenda kuwasikiliza CDM. Hii inadhihirisha kuwa CDM wanakubalika saana kuliko nyie. hivyo katika hili msikurupuke kumtumia mtu kama tendwa kutishia kukifuta CDM, Nawahakikishia leo Tendwa akisema nakifuta CDM siku hiyo hiyo maandamano ya nchi nzima yataanza.

  Hivyo fikirieni kabla ya kutenda, sihitaji consultation fee kwa hili nimewapa bure serikali.
   
 2. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  KWELI hawa watu hawajajua kabisa maana ya upinzani na multi-party kwa ujumla.
  Angalia USA pamoja na mambo mengi anayojitahidi kufanya lakini hutakosa kusikia maneno ya kejeli,chuki binafsi,vijembe n.k kutoka kwa wapinzani wake Republican.

  Hilo ni swala la kawaida kabisa.
  CCM walipaswa baada ya kuona na kusikiliza hizo hoja wazijibu kwa vitendo kama kupunguza mfumuko wa bidhaa,kuongeza mishahara kama China wanavyofanya kwa sasa.Huwezi kunieleza mshahara ule ule utakidhi mahitaji wakati zaamani nilinunua sukari 1600 leo 2200, petrol iko juu,nauli ziko juu ..je huyo mtu ataishije??Hapo ndipo serikali inapotakiwa ichukue hatua za haraka zaidi wala sio kuanza kulaumiana na CDM au watu wengine.Wenye matatizo ni wananchi wala sio CDM kama wananyotaka kusema.
  Wajaribu kupunguza mishahara ya watu wakubwa kama wabunge,mawaziri etc wapunguziwe kabisa hiyo mishahara yao au wawekewe tax kubwa zaidi na hizo pesa ziende moja kwa moja ku-subsidize wale wenye low income ,hili linafanywa na nchi za wenzetu na limeonekana kuwa linafaa sana.
  Ukweli ni kwamba kuna income gap kubwa kati ya rich and the poor na hapo social instability haiepukiki lasivyo wawasaidie hao wasiojiweza.
  This can be done wihout affecting other social development projects.
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Hao inaonekana mwisho wa ufahamu wao umeshafikia mwisho na kuona kuwa kufuta CDM ndio suluhisho,eeh wadanganye waone mamabo yatakavyobadirika ghafla.
  Wananchi ndio wenye shida na matatizo ,CDM wanachokifanya ni kuwatetea tu na kupaza sauti zao,sasa tatizo liko wapi??messanger huwa hauliwi siku zote.
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna machafuko wala nini. Nguvu za dola zitachukua mkondo wake na mmeshawekwa kwenye target
   
 5. T

  TUWEKANE BAYANA Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wengine bwana.. Unakuja jamii forum kututishia amani umetumwa?! Kukamatwa unaona hatari sana wewe? Mandela yule pale kakamatwa avotoka kawa raisi.. Hii ni nchi huru, kama mambo ya muhimu ambayo serikali inatakiwa haitupi na kimya pia tukae? Watajuaje mahitaji yetu bila kuwaambia?!
   
Loading...