Kashaga na wenzako unatusaidiaje kwa haya pamoja na serikali hii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashaga na wenzako unatusaidiaje kwa haya pamoja na serikali hii?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gerald, Mar 12, 2011.

 1. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hello wana JF
  Ningependa kutoa maoni yangu kama ifuatavyo

  Nashukuru wana JF kwa michango yenu na habari mnazotuletea sisi kwetu ikiwa ni changamoto kwetu kujua mambo yanavyokwenda nchini mengine ni mazuri na mengiyao ni mabaya inadhihirisha wazi kuwa hiki ni kijiji cha great thinkers.

  Mtazamo
  Katika siku kadhaa sasa najaribu kufikiri hii nchi inaendaje ukizingatia tokea bunge likae miswada inayohusu nchi ambayo ni muhimu kabisa inapingwa kujadiliwa au kulindwa kwa waheshimiwa fulani kwa kinga ya spika bungeni kwa maslai aidha ya chama fulani au kikundi fulani
  Mifano:-
  Katiba,Mauaji ya Arusha, Dowans, IPTL, Tanesco, Migomo,TRL,ATCL, IV, Mikopo,Afya(mwananyamala), Mabomu(wizara ya ulinzi), Mikataba yote tata na mfumuko wa bei usioeleweka kikomo chake kitakua lini NK. Hizi zilikua hoja za msingi bunge letu tukufu kujadili na kutatua haya matatizo

  Ukitafakari kwa kina utakuta kila wizara ni uozo mtupu labda kidogo hizi wizara mbili ya miundombinu na ya ardhi zina uhai kwa sasa.

  Katiba:-
  Tunashukuru wasome walitufungulia kongamano la mustakabadhi mzima wa kutungwa upya na sio marekebisho ya katiba pale UDSM je? wanaharakati mnafanya nini mpaka sasa? pia wana JF mnashinikizo gani kwa serikali ili tupate katiba mpya kabla ya uchaguzi 2015? au ndio majibishano tuuu umu JF wakati msingi mzima wa haya matatizo nchini ni katiba? Tuamke tusibishane kivyama bali wote kwa pamoja tuipe shinikizo serikali kwa haraka zaidi tupate katiba yetu ndio utakao kua ukombozi wetu wa 2015.

  Utendaji:-
  Nikitafakari kwa ujumla serikali ya awamu ya tatu ingawa ilikua ni ya kidictator ila kwa ujumla wake tuliona result zake kama Daraja la mkapa, barabara, uchumi, bei za bidhaa kutopanda karibu awamu zake zote nk.
  Hii serikali ya awamu ya nne kweli mpaka sasa sijajua ni nini hasa ilichokifanya zaidi ya kusikia (mchakato wake umeshakwisha tunasubiri kazi kuanza)

  Mfano:-
  Kama uliweza kulifuatilia bunge karibia wizara zote kila project zipo kweny mchakato kuisha na kazi itaanza muda si mrefu
  1. Wizara ya nishati na madini- Alikuja na mlolongo wa project ambazo tokea mwaka 2005 mpaka leo ni michakato tuuu wakati hapo kenya project ya kujenga mitambo ya kuzalisha umeme (MW120 ivi sina uakika) , ilifunguliwa juzi walitumia miezi 14 vipi hapa kwetu? Ngeleja tueleze na michakato yako kama kweli walikua hawana lao jambo na dowans iweje tokea january mpaka leo serikali pamoja na tanesco wameshindwa kununua mitambo ya haraka kuokoa taifa katika hili janga? technical department mnatuambia nini? au ndio tunavilaza?
  2.Wizara ya sheria- warema na mama yako da! Mama katiba ilimuumbua kwa aibu akauzuria kongamano la ufunguzi pale UDSM na huyu warema naye Dowans inamuumbua wasomi tuna watu hapa?
  Elimu-Huyu mweshimiwa naye ndio kabisaa
  Afya- Wamekuja na kali ya bajaj za kubebea wajawazito tutafika kweli?
  Ulinzi-Mabomu tupu sasa na ukiukwaji wa haki za binadamu
  Na baadhi ya wizara nyinginezo.

  Siasa:-
  Kuna baadhi ya chama ambacho kinajiita mkombozi wa wanyonge sawa tunakubaliana nacho na vingine vingi vyenye dola nk, hapa ndio hasa wana JF kuna utata mkubwa.
  1.JF lazima tukubali hoja za kila mtu pasipokutoa tusi kwa mchangiaji yeyote hata kama threads yake aina maana mfano kama hii yangu aina maana kwako basi zaidi toa ushauri wenye tija.
  2.Wachangiaji jaribu kuleta mada yenye ukweli na sio propaganda za mtaani ukizingatia JF ni WW inachekiwa.Thread za vyama au itikadi ilimradi uitoe kukashifu au kukisifia chama fulani bila source alisi itakua ni upotoshaji wa habari.

  Matokeo:-
  Kumekua na matokeo mabaya sana katika mwezi uliopita na kuendelea sasa katika JF specialy wachangiaji katika mada ya siasa
  Mfano- chama fulani kilianzisha maandamano ya kimsingi kabisa kudai haki za wananchi yakiwemo mambo muhumi na yenye msingi katika taifa letu ambapo chama fulani kwenye uchaguzi uliopita uliahidi kuboresha zaidi kama Maji, Umeme, Elimu,Afya,Ufisadi na maisha bora kwa kila mtanzania. Je ni kweli maisha bora hayo yapo sasa?
  Najiuliza hichi chama kilichoanzisha haya maaandamano kwenda kuwaelimisha raia kwamba wasikubali kulipwa kwa Dowans, Kudai katiba Mpya, kupanda kwa garama za umeme, na bei za vyakula kuwa juu leo hii kimekua ni chama cha kuvunja amani? wale maelfu walioandama ukanda wa ziwa walivunja amani? Jamii inaitaji hoja za msingi zijibiwe au kutatuliwa sio kutoa propaganda hasa baadhi yao wameshaingia uku JF (Kashaga) na wenzake, Je waziri mstaafu sumaye ni wa hicho? Na sasa wanatumia kodi zetu kwenda kufuta kwa raia hoja za msingi wanazotakiwa kuzijibu na kupandikisha kuwa chama fulani kinaleta uvunjifu wa amani sidhani kama zitafutika kama maisha yataendelea kua ivi. Wasomi mpowapi? hata serikali hamlioni hili? na wengine kwenye luninga akianzia na mkuu wao kutoa hoja zisizo kizi matakwa ya raia bali maslai ya chama chake. Ahsante wasomi kwa kutoa maoni ya hotuba ya mweshimiwa mkiipinga kuwa aikua kwa ajili ya maslai ya taifa, na nyie mapropaganda jibuni haya kwanza au wajibikeni kwa vitendo. kama ajira yako ipo kwa ajili ya kupotosha ukweli Tafadhali wakati huu inaitajika matendo zaidi sio porojo.
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka Gerald thanks....

  Kwa upande wangu naweza kusema tuko karne ya 21 lakini kwa bahati mbaya tuko na watawala (sipendi kuwaita viongozi) ambao bado wako karne ya 18...


  • Hawa wanadhani Watanzania hatuoni matumbo yetu kuwa yana njaa wakti ya kwao yameshiba,\
  • Hawadhani kuwa tunaona ya kuwa miili yetu ni midhaifu na hakuna huduma ya uhakika wakati wao mafua wanaenda India

  • Wanadhani hatuoni watoto wetu hawapati fursa ya elimu iliyobora, hawaendio shule na kama wakienda basi watakaa sakafuni, walimu hakuna na vifaa vingine vya elimu wakati watoto wao (wakijigamba ni watoto wa wakulima) wanasoma shule za msingi za Tshs 17M kwa mwaka
  • Wanadhani hatuoni pengo linalozidi kati yao walioko kwenye utumishi wa umma na maswahiba wao waliowafungulia milango ya kutafuna utajiri wa nchi hii kwa njia za kuwakopea na kuwapa fedha za kuendesha udhalimu wao

  • Wanadhani hali ya magogoni ndivyo ilivyo na Mahoma Manyika......Hawafikiri kuwa tunaweza kuona na kutaka kutuficha kila kitu

  Matokeo ya "kutokudhani" kwao ndiyo yanayowafanya "kukata umeme" wakidhani hatutayaona matumbo yetu yanayonguruma kwa njaa, hatutagundua tumelalia magagulo au hatutaona wanavyotuibia utajiri wetu...

  Hivi ndivyo wanavyodhani ya kuwa kwa upuuzi wanaojaribu kuumwaga katikati ya watu, njaa zetu hatutziona.

  Ni wakati wao kufahamu ya kuwa "Hata kama macho yatapofushwa kwa mabomu makali ya kemikali za machozi na kupoteza kabisa uono, bado njaa na shida zetu tutaziona"

  Wanaotaka kutupumbaza tusahau njaa zetu kwa porojo zao, hawa ni wapuuzi wa kuwapuuzia maana wao wamekaa kuelekea dirisha ambalo [pepo za mafisadi na majambazi wa uchumi wetu walalahoi wa Tanzania unavuma kuelekea kwao kutoka kwa mabwana wao........ashakum si matusi
   
Loading...