JK Sahani Moja na Upinzani Hotuba ya Agosti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK Sahani Moja na Upinzani Hotuba ya Agosti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Aug 22, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135


  JK Sahani Moja na Upinzani Hotuba ya Agosti

  Watanzania tuna utamaduni wa kushangaa mazuri na kufurahia mabaya kwa kutazama tu anayeyasema ni nani na wakati gani bila kuzingatia anayoyasema yana tija au ni porojo tu za jukwaa kujisafishia mkate wake.

  Mpaka leo huwa najiuliza alitoa wapi ujasiri na undumilakuwili ule Mzee wangu Ben katika kampeni za mwisho za CCM pale jangwani 2010 alipoamua bayana kuwatukana wapinzani ati ni wanafiki wakubwa kwa kuhoji serikali imefanya nini kama vile hawana macho.

  Ni mwaka tu sasa unakatika hata kauli hii ya Mzee Ben bado haijafutika katika masikio yetu alipoibuka ghafla kutoka Nairobi katika usuluhishi wa ghasia za baada ya Uchaguzi Nchini Kenya ambapo alirejea huku ujio wake ukitanda wingu zito la kashfa ambazo si mahala pake kuzizungumza maana si mintarafu ya makala nayokusudia leo.

  Namtazama Mzee Ben kama kioo na chagizo muhimu katika kusaidia kutanzua mkwamo wa kiuchumi Nchini lakini kwa hili nasema hapana tena iliyoshiba huku nikisukumwa sasa na matokeo ya utitiri wa kauli za wanasiasa wenye njaa ambao nao wametumbukia katika mkumbo huu wa kuukebehi upinzani akiwemo mjomba wangu Mzee wa Viwango na Spidi.

  Inawezekanaje katika Nchi hii ambayo leo tunaadhimisha miaka hamsini ya Uhuru hali ya miundo mbinu na huduma za kijamii ni duni kuliko maelezo ya kawaida huku tukiendelea kujinasibu kwa nyimbo nyingi nzuuri za kisiwa cha amani na tuna rasilimali nyingi, ambazo kamwe hatujui zinamsaidia nani?

  Wenye kuyaona haya mapema wengi wanaishia kutiwa tonge mdomoni na wengine kulambishwa asali na kuusahau shubiri hii ya ukali wa maisha unaowakabili watanzania.

  Sishangai Rafiki yangu Mjomba aliyejitahidi kwa kutunga Beti zenye mantiki na ukosoaji wa hali ya juu kwa uozo huu wa serikali na yeye leo tayari domo limejaa zege maneno hayatoki tena baada ya kupewa ulaji na Adui yake Mkubwa mpango wa Malaria ambaye hata pale katika tamasha kubwa la malaria hakumwalika lakini baada ya kelele za wanahabari wakamkumbuka na leo haemi kitu tena zaidi ya kushabikia ujinga.

  Akianzia kule TCRA, baadaye Zain na sasa katika dawa butu za Maralia.
  Kama haitoshi kila ukifunua mdomo kuwaambia watanzania tudai haki yetu kwa nguvu ya Umma maana mazungumzo yameshindikana baadhi ya wenzetu wenye msongo wa mawazo na ufinyu wa fikara bado watakwambia nyie mmezoea vurugu tu hebu iacheni serikali ifanye kazi.

  Ashkum si matusi, kazi gani hiyo ambayo bado wanataka kuifanya na wameshindwa kuimaliza katika kipindi cha miaka hamsini isiyokuwa na tija ya kuridhisha, narudia tena tija ya kuridhisha au ni wizi tu na udangayifu kwa umma.

  Hakuna sababu tena ya mtanzania kusimama akipinga maandamano ya CDM, hii ndio njia sahihi iliyobakia kuonyesha nini hasa tunahitaji na si porojo na hotuba ndeefu ambazo kila siku zinaediwa kisha copy na paste.

  Msingi wa hoja yangu ni hapa kuna fununu kwamba baada ya kimya kirefu Mkuu wa Nchi anajipanga kutoa Hotuba Mwisho wa mwezi huu ikiwa ni sehemu ya kureview na kupoza makali kwa hekaheka nyingi zilizolikumba Bunge la serikali yake kipindi hiki.

  Na pengine kutoa mkono wa Iddi kwa waumini wa Dini ya Kiislam.
  Linalotarajiwa hapa ni mkuu wa Nchi kuzungumza tena kwa ukali huku akijinasibu kwa kuvaa usiriasi usioonekana katika matendo yake zaidi ya kufanya maigizo hayo katika luninga.

  Hii haitoshi kwa kuwavaa wapinzani na kusimanga juhudi zao muhimu kabisa za kushinikiza mabadiliko, tunataka kuona huduma za uhakika kwa watanzania wa leo na kwa hakika tunawajibika kuendelea kulipigia hili kelele kupitia Nguvu ya Umma hadi kieleweke.


  ADIOS

  Ahadi za Bwana Mkubwa hizi hapa: KWA OMBI MAALUM ndani ya Thread

  [​IMG] JF Senior Expert Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]

  Join Date : 22nd October 2009
  Location : Mtimbwani
  Posts : 500

  Rep Power : 23

  [h=2][​IMG] Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015[/h]
  AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...
  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  mkuu na huu mgao ndio kabisa unatuongezea hasira,maana DAR ES SALAAM imekuwa DARK ES SALAAM!
   
 3. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hapo kuna nyimbo nzuri utazisikia Mkuu
   
 4. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Atatuambia tuwe makini tusije tukajikuta tunaingia kwenye migogoro kama majirani zetu
  hasa Libya
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu tusubiri tu aseme manake katika hali kama hii Nchi iko kwenye sintofahamu ya mambo mengi na mkuu anakaa kimya inakuwa kazi kwelikweli. Tuzisikie kauli zake
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu hakuna jipya na zaidi zaidi ni ahadi kuwa bado serikali iko kwenye mchakato na mipango lukuki ambayo haijulikani itaisha lini
   
 7. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Umelenga katika vibwagizo vya hotuba hiyo na vile waasi wameingia Tripol leo sijui itakuwaje
   
 8. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kimbunga hiki kimya kwa kweli dawa yake sijui itakuwa nini, mambo yanaparaganyika unawasikia watu wanavurumisha matamko kutoka nje ya Nchi kwa mambo ambayo hata hayana tija kabisa
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  NA anaonekana hana wasi wasi na yanayotokea hapa nchini kama vile hayamgusi moja kwa moja na sijui hata akihutubia ni wangapi watakamsikia maana asilimia kubwa watakuwa gizani kama sio wote
   
 10. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nchi ya M ichakato na bado linafanyiwa upembuzi yakinifu, sijui kosa ni kukua kwa kiswahili au watumiaji. Maana Mkuu haya maneno yamekuwa silaha ya viongozi wazembe, na kibaya hata wafanyabishara nao wameyaiga.

  Mwezi uliopita nilitafuta pair moja ya tairi low profile. Kila ukienda dukani jamaa anakwambia bado nafanya mchakatio mpaka tumeagiza NBI
   
 11. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  mzee Yusufu ameshaandaa hotuba,subirini mipasho mpaka mchonge ngenga! Mmesahau mla huliwa? Kelele za mlango.....! Na lile tabasamu la kumtoa nyoka pangoni wadanganyika kwishey babuji!
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu ukipiga gharama za huuo upembuzi na mchakato unajikuta nusu ya gharama za mradi zilishaliwa mpaka uje ukae uanze mradi wenyewe ni kwamba ni lazima uongezeke gharama
   
 13. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #13
  Aug 22, 2011
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Yetu macho na masikio,kisha za kuambiwa unachanganya na za kwako.
   
 14. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Safari hii tunazichanganya mapema kabisa tunataka ujumbe huu autambue. Wakati anatupanga na mbwembwe za kwenye luninga mbayuwayu hatupo tena
   
 15. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Si unasikia wanatak kutoana roho Geita, barabara ya Kamanga Sengerema kuunga na ya Geita michakato imeshazidi makadirio ya ujenzi kwa kiwango cha Muramu. sasa walikuwa wanachakata nini hapo.

  Sitashangaa siku hiyo umeme ukawaka hata miji ulikoshaulika walau wasikie vitisho vya bwana mkubwa
   
 16. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,348
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  a.k.a DARK CITY
   
 17. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Watts zimepunguzwa kutibu kadhia ya Mza. Moro napo nasikia kumekucha Giza Mtindo mmoja
   
 18. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu ukiuliza sana na ukifuatilia sana unaweza pata ugonjwa wa moyo
  Mambo mengine bongo hii yanapasua kichwa na unaweza jiuliza hao wanaoyafanya ni watu kweli walio na utashi au ni wanyama
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hili giza ni hatari kwa usalama wa nchi. Wasuka nywele hawana ajira, vinyozi hakuna kitu, wakamua juice ya miwa hola, majambazi sasa ndio wanaweza ku attacck kwa raha zao si wanapenda gizani na sasa giza ndio limetamalaki!!
   
 20. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Utasikia"Tumepiga hatua kubwa sana na wataalam wa mambo ya uchumi wametusifu sana, sisi tunakuza uchumi wengine wanaangaika na maandamano" SIJUI HUWA ANAMAANISHA UCHUMI WA KWENYE MAKARATASI?
   
Loading...