Serikali Ikifanya Hili, Wahitimu Wote Watapata Ajira.

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,645
2,000
Kumekuwa na kilio kikubwa sana cha vijana wanaohitimu ngazi mbalimbali za elimu kukosa ajira. kilio hiki ni cha dunia nzima.

hapa kwetu walio katika ajira ama nyadhifa mbalimbali wamekuwa wakitoa mwito kwa vijana kuwa wajiajiri. lkn vijana wamekuwa wakilalamika kuwa hawana mitaji.

vijana pia wanaona mwito wa kutaka wajiajiri hauna mashiko maana wanaoutoa wao pia wameajiriwa.

mm nimekaa chini na nimekuja na suluhisho la kilio hiki cha vijana. " kwa kuwa vijana wanalalamika hawana mitaji, na kwa kuwa wanaotoa mwito wa vijana kujiajiri wao wako kwenye ajira miaka mingi. basi serikali iweke sheria kuwa mtu akae kwenye ajira miaka 10 tu na astaafu. ili vijana waingie kwenye ajira nao wapate mitaji, baada ya miaka 10 wanang,atuka.

kwenye nafasi za kisiasa iwe hivyo hivyo.

hili likitekelezwa litatoa nafasi kila mtu kutumia ajira kama sehemu tu ya kupata mtaji ili ajiajiri.

katiba inaweza kufanyiwa marekebisho ili kukidhi matakwa haya. tusiwe wabinafsi tusaidie vijana wetu
 

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,645
2,000
Ndiyo inawezekana, kukiwa na utashi na kama huu wimbo wanao imbiwa vijana hauna unafiki
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom