thelovechild
Member
- Oct 16, 2012
- 17
- 7
Hakuna cha kukanusha, acha na dunia ijue tuko kwenye hali gani. Na tunajua utawala huu si wa kusikiliza wananchi wanahitaji nini. Sisi ndio tupo mtaani, tunajua mahitaji yetu, leo hii hao wamekaa kwenye viti vyao wanajifanya hawasikii sauti zetu, hawaoni maumivu yetu na bila shaka hawaumizwi na machozi yetu. walikuja kwa unyenyekevu na upole sana walipoomba kupewa nafasi kutawala. Wakae wakijua, kila wafanyalo tutalihesabu na hatutasahau.Wanabodi,
Uzalendo ni kutokubali na kutonyamaza kimya wakati rais wako anaposemwa vibaya kwa hoja za uongo na media za nchi nyingine, bali ni kwa media zetu kujitokeza, kuukanusha uongo kwa kuusema ukweli na ikibidi serikali yetu sio tuu ikanushe bali pua ihitaji kuombwa radhi!.
Pamoja na matatizo yote na mapungufu yote ya rais wetu Magufuli, kwa sababu na yeye ni binadamu na sio malaika, Watanzania wote wazalendo wa kweli wa nchi yetu, tusikubali rais wetu kudhalilishwa kwa kusemwa vibaya, na kusingiziwa uongo na media za nje bila ya media za ndani kukanusha na kumtetea, au kuunyamazia udhalilishaji kama huu ni sawa na kushangilia rais wetu kudhalilishwa.
Hoja hii ni kufuatia makala hii
SABC News - Tanzania’s Magufuli descends from darling to despot:Sunday 9 April 2017
Kulikopelekea kuibuka kwa mjadala huu SABC NEWS: Magufuli kutoka rais apendwae mpaka kuwa dikteta!
Wito.
Natoa wito kwa Waziri wa Habari, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu au Idara ya Habari Maelezo kuukanusha uongo huu unaoenezwa kumhusu rais wetu, kwa sababu uongo ukisemwa sana na kuachwa bila kukanushwa mwishowe sio utaonekana kama ni ukweli, bali utageuka ukweli.
Jumatatu Njema.
Paskali.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!
Tension between Tanzania's 'bulldozer' president and opposition
NB dunia inaona...