Ndugu zangu wanaJF,
Mengi yameongelewa humu JF juu ya mtu anayejiita Dr. Ndodi kuhusu utapeli wake. Mwanzoni nilidhani wanamwonea lakini mimi mwenyewe nimeshuhudia kwa macho yangu. Kuna kijana mmoja wa kiarabu ni jirani yangu anasumbuliwa sana na pumu. Baada ya kumwona na kumsikia ndodi kupitia vipindi vyake vya TV na radio nilimshauri huyo kijana amwone ndodi. Alipofika kwenye zahani magomeni mwembechai aliambiwa dawa inauzwa sh. 70,000 na utaratibu ni kwamba unanunua kwanza ndipo upate maelezo ya namna ya kutumia. Aliponunua akaenda kumwona ndodi. Maelezo aliyopata ni kwamba dawa aliyonunua ataitumia kwa wiki moja tu. Baada ya hapo itabidi afuate dawa nyingine kwa bei hiyohiyo na ataendelea kufanya hivyo kwa wiki kumi. Yule kijana alishangaa sana. Alitaka kuacha dawa ili arejeshewe fedha lakini ilishindikana. Aliporudi nyumbani, mimi pamoja na jirani wengine tulimshauri asikate tamaa bali atafute namna ya kupata fedha ili ahakikishe kuwa anamaliza dozi nzima. Bahati nzuri ndugu zake ambao wapo Oman walimchangia kiasi kikubwa cha fedha na akamudu kulipa fedha yote yaani sh. 700,000 mpaka akamaliza dozi. Kinachosikitisha ni kwamba mpaka sasa hakuna nafuu yoyote aliyopata. Pumu bado inamsumbua vilevile. Mbaya zaidi alipokwenda kwa ndodi aliambiwa kuwa eti inawezekana hakuwa anazingatia muda wa kunywa. Kwa hiyo, itabidi aanze dozi upya kwa bei ya sh. 600,000 kwa dozi nzima. Jambo hilo ndilo lililoniuma kiasi cha kuamua kuleta humu jamvini. Ukweli ni kwamba kijana wa watu alikuwa anazingatia sana muda. Mimi mwenyewe nilimsisitiza sana tangu mwanzoni kwamba dozi ya muda mrefu huwa ni muhimu sana kuzingatia muda na nilimshauri aiseti simu yake ya mkononi iwe inamkumbusha na alifanya hivyo.
My take:
Kuna wimbi kubwa limejitokeza katika miaka ya hivi karibuni ya watu kugeuza afya za binadamu wenzao kuwa mitaji. Wengi wao kama ilivyo kwa ndodi wanatumia hata misahafu kama biblia kuvuta wateja wengi. Madhara yake ndiyo hayo yaliyomkumba kijana wa kiarabu. Fedha nyingi zinatumika na hakuna nafuu inayopatikana. Ebu fikiri, katika hali ya sasa ya maisha magumu, mgonjwa analipa zaidi ya shilingi milioni moja na haponi, inaumiza kiasi gani. Ifike mahali Serikali iwaonee huruma watu wake kwa kuchukua hatua madhubuti ya kuwabana akina ndodi. Kwanza wachunguzwe kama kweli tiba zao ni za kweli. Pili wachunguze uhalali wa bei wanazowatoza wagonjwa.
Makanisa yamekuwa mitaji ya kutapeli watu siku hizi. Ndo yale yale ya vikombe vya babu loliondo, bibi tabora, ndodi wa mahotelini makubwa, kina DECI nk. Yote hayo matunda ya makanisa.
Sasa hivi anahamasisha watu waende wakapate dawa bure ila waende na pesa ya kumuona daktari (yeye ndodi). Sababu ya kutoa dawa bure anadai kuna mtu mmoja alimlipia pesa ya vipindi vya kwenye tv. Inawezekana hata hakulipiwa chochote ila alipanga dili na huyo mama mtoa ushuhuda ili kuwavuta watu maana nasikia hata hiyo pesa ya kumuona daktari nasikia haishikiki.
Ukosefu wa elimu unaiangamaiza Tanzania! Bado tumejifunika kwenye blanketi la ujinga na umbumbumbu!Nilivyousikia ushuhuda wa yule mama startv, alafu ndodi nae akatangaza ofa ya kupata dawa bure isipokuwa uende na kiingilio tu, ilibidi nami niende kesho yake hapo magomeni kufukuzia ofa. Kichonistua ni ukubwa wa hicho kiingilio chake nikaambiwa sh.50,000. kwa kweli sikuamini ikabidi niondoke haraka sana. Afu huwa hatangazi ktk media hicho kiingilio ni mpaka uende ili akakutapeli hukohuko. Kweli huu ni wizi jaman.
Ndodi!Ndodi!Ndodi!
Huyu mjomba ni Tapeli wa Kimataifa.Kuna siku 1 kwenye STARTV,alimkodi maza mmoja hv kuja kutoa ushuhuda wa tiba ya huyo TAPELI.Mtangazaji wa STAR akamuuliza yule MAZA,kwamba alitumia aina gani ya MATUNDA na kufanikiwa kupona mwanaye?Yule Maza akajitafuma sana na akashindwa kujua hata tunda gani lililo mponyesha mwanaye!Huyu Mjomba kifupi ni Mwizi Mkubwa huyu.Wananchi inabidi wawe na Mwamko!Vinginevyo wataliwa fedha zao bure.
Magomeni ni makazi ya SHEIKH-TWAINpole mwarabu me nakushauri uje loliondo kwa babu na jero yako tu upate kikombe cha uzima na kama hutak utaendelea kutapeliwa tu maana hapo bado hujaenda kwa sheik yahya atakwambia kuita jini moja laki 2. magomen ni makaz ya matapeli,wakabaji, walaghai ht mafisadi wapo take care bro.