Serikali iingilie kati tiba ya Dr. Ndodi wananchi wanaliwa fedha nyingi na hawaponi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali iingilie kati tiba ya Dr. Ndodi wananchi wanaliwa fedha nyingi na hawaponi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kingcobra, Apr 23, 2011.

 1. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Ndugu zangu wanaJF,

  Mengi yameongelewa humu JF juu ya mtu anayejiita Dr. Ndodi kuhusu utapeli wake. Mwanzoni nilidhani wanamwonea lakini mimi mwenyewe nimeshuhudia kwa macho yangu. Kuna kijana mmoja wa kiarabu ni jirani yangu anasumbuliwa sana na pumu. Baada ya kumwona na kumsikia ndodi kupitia vipindi vyake vya TV na radio nilimshauri huyo kijana amwone ndodi. Alipofika kwenye zahani magomeni mwembechai aliambiwa dawa inauzwa sh. 70,000 na utaratibu ni kwamba unanunua kwanza ndipo upate maelezo ya namna ya kutumia. Aliponunua akaenda kumwona ndodi. Maelezo aliyopata ni kwamba dawa aliyonunua ataitumia kwa wiki moja tu. Baada ya hapo itabidi afuate dawa nyingine kwa bei hiyohiyo na ataendelea kufanya hivyo kwa wiki kumi. Yule kijana alishangaa sana. Alitaka kuacha dawa ili arejeshewe fedha lakini ilishindikana. Aliporudi nyumbani, mimi pamoja na jirani wengine tulimshauri asikate tamaa bali atafute namna ya kupata fedha ili ahakikishe kuwa anamaliza dozi nzima. Bahati nzuri ndugu zake ambao wapo Oman walimchangia kiasi kikubwa cha fedha na akamudu kulipa fedha yote yaani sh. 700,000 mpaka akamaliza dozi. Kinachosikitisha ni kwamba mpaka sasa hakuna nafuu yoyote aliyopata. Pumu bado inamsumbua vilevile. Mbaya zaidi alipokwenda kwa ndodi aliambiwa kuwa eti inawezekana hakuwa anazingatia muda wa kunywa. Kwa hiyo, itabidi aanze dozi upya kwa bei ya sh. 600,000 kwa dozi nzima. Jambo hilo ndilo lililoniuma kiasi cha kuamua kuleta humu jamvini. Ukweli ni kwamba kijana wa watu alikuwa anazingatia sana muda. Mimi mwenyewe nilimsisitiza sana tangu mwanzoni kwamba dozi ya muda mrefu huwa ni muhimu sana kuzingatia muda na nilimshauri aiseti simu yake ya mkononi iwe inamkumbusha na alifanya hivyo.

  My take:
  Kuna wimbi kubwa limejitokeza katika miaka ya hivi karibuni ya watu kugeuza afya za binadamu wenzao kuwa mitaji. Wengi wao kama ilivyo kwa ndodi wanatumia hata misahafu kama biblia kuvuta wateja wengi. Madhara yake ndiyo hayo yaliyomkumba kijana wa kiarabu. Fedha nyingi zinatumika na hakuna nafuu inayopatikana. Ebu fikiri, katika hali ya sasa ya maisha magumu, mgonjwa analipa zaidi ya shilingi milioni moja na haponi, inaumiza kiasi gani. Ifike mahali Serikali iwaonee huruma watu wake kwa kuchukua hatua madhubuti ya kuwabana akina ndodi. Kwanza wachunguzwe kama kweli tiba zao ni za kweli. Pili wachunguze uhalali wa bei wanazowatoza wagonjwa.
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Huyu ndodi mbona analalamikiwa na watu wengi sasa! Inawezekana kuna ukweli. WanaJF wenye influence kwenye system watusaidie kumfuatilia huyu tapeli. Nasikia kuna wakati serikali ilitaka kumfuatilia na yeye alishtuka na kuacha kujitangaza. Lakini hivi karibuni naona amerejea kwa kasi kubwa.
   
 3. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu, kama nawe una amini katika dini zetu 2 zinazo2eleza kuna maisha baada ya kifo, basi tutashangaana sana huko tuendapo. Watu wamegeuza dini zetu mtaji, kwa kufungua vitabu vyetu vya dini wanatutapeli na kufanya ndio nyenzo ya maisha yao. Tulaani vitendo hvi na hatua za haraka za kisheria zichukuliwe.
   
 4. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwanza nampa pole sana kijana wa watu kwa kutapeliwa kiasi hicho. Kwa kweli inatia uchungu sana hasa kwa mwanachi ambaye hana uwezo wa kuchukua hatua yoyote ile zaidi ya kuendelea kuumia.

  Mimi nashauri ianzishwe operation maalum ya kuwapitia watu wote wanaojiita madaktari na kuwakagua kwa kina uhalisia na uhalali wa tiba zao na zichukuliwe hatua za kisheria tena kali ili kutoa funzo kwa matapeli wengine. Ndodi ni tapeli tena mkubwa. Anawavuta wananchi wengi kwa porojo zake anazoongea kama cherehani. Mimi ni mmoja wa watu waliotapeliwa na ndodi na niliandika thread kulaani kitendo hicho na kutoa wito kwa serikali imfuatilie ili wananchi wengi zaidi wasitapeliwe.
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa ni tapeli maana watu wengi wanamlalamikia.
   
 6. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Pole sana; nakubaliana na wewe sasa hivi watu wanatumia matatizo ya watu kuwa mtaji! Inasikitisha sana. Sasa ushauri wangu, mwambie huyo rafiki yako atafute mmea uitwao (scientific name) Euphorbia hilta (mziwaziwa- Swahili au Athma weed- English) na majani ya mpapai, akaushie ndani then:-
  -Asokote sigara avute au
  -Aunguze chumbani wakati wa kulala (kama udi)
  Inatuliza; haiponyeshi!
   
 7. mjunguonline

  mjunguonline Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndodi!Ndodi!Ndodi!
  Huyu mjomba ni Tapeli wa Kimataifa.Kuna siku 1 kwenye STARTV,alimkodi maza mmoja hv kuja kutoa ushuhuda wa tiba ya huyo TAPELI.Mtangazaji wa STAR akamuuliza yule MAZA,kwamba alitumia aina gani ya MATUNDA na kufanikiwa kupona mwanaye?Yule Maza akajitafuma sana na akashindwa kujua hata tunda gani lililo mponyesha mwanaye!Huyu Mjomba kifupi ni Mwizi Mkubwa huyu.Wananchi inabidi wawe na Mwamko!Vinginevyo wataliwa fedha zao bure.
   
 8. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Serikali inashindwa kumchukulia hatua kwa vile Dr Ndodi analindwa na sheria ya Tiba asilia na tiba mbadala ambayo inawatambua waganga wa kienyeji wote. TFDA wamejitahidi kumdhibiti kwa kutumia sheria namba 1 ya mwaka 2003 ya kudhiditi vyakula, dawa na vipodozi lakini wamegonga mwamba
   
 9. K

  Kivia JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Makanisa yamekuwa mitaji ya kutapeli watu siku hizi. Ndo yale yale ya vikombe vya babu loliondo, bibi tabora, ndodi wa mahotelini makubwa, kina DECI nk. Yote hayo matunda ya makanisa.
   
 10. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sasa hivi anahamasisha watu waende wakapate dawa bure ila waende na pesa ya kumuona daktari (yeye ndodi). Sababu ya kutoa dawa bure anadai kuna mtu mmoja alimlipia pesa ya vipindi vya kwenye tv. Inawezekana hata hakulipiwa chochote ila alipanga dili na huyo mama mtoa ushuhuda ili kuwavuta watu maana nasikia hata hiyo pesa ya kumuona daktari nasikia haishikiki.
   
 11. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Kwani Ndodi anatumia Kanisa au Biblia? Jaribuni kujua kutofautisha mambo? Ukweli matapeli wapo na lazima wajaribu kutumia maeneo yanayoaminika ili wawapate! Taadhari ni kwamba yalitabiriwa na kwa sababu watu hawataki mafundisho ya kweli na wanataka mambo rahisi ya kufanikiwa kwa Shortcut lazima wadanganywe. Ila nawasihi watumishi wa kweli wawafundishe wtu wao na pia wakemee jambo hili hadharani maana ukimya wao ndiyo maumivu yetu
   
 12. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #12
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilivyousikia ushuhuda wa yule mama startv, alafu ndodi nae akatangaza ofa ya kupata dawa bure isipokuwa uende na kiingilio tu, ilibidi nami niende kesho yake hapo magomeni kufukuzia ofa. Kichonistua ni ukubwa wa hicho kiingilio chake nikaambiwa sh.50,000. kwa kweli sikuamini ikabidi niondoke haraka sana. Afu huwa hatangazi ktk media hicho kiingilio ni mpaka uende ili akakutapeli hukohuko. Kweli huu ni wizi jaman.
   
 13. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Ukosefu wa elimu unaiangamaiza Tanzania! Bado tumejifunika kwenye blanketi la ujinga na umbumbumbu!
   
 14. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,669
  Trophy Points: 280
  Ndodi ni kiboko niliwahi kwenda siku moja kumwona,nikaambiwa kuongea nae ni TSHS 50,000/=hapo bado sijaambiwa dawa,Eeeh niligeuka faster na kuondoka,huyu jamaa yuko kimaslahi zaidi na sio kuwasaidia watu kama anavyodai.
   
 15. howard

  howard Senior Member

  #15
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wajinga ndio waliwao huyo jamaa ni tapeli tu
   
 16. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  pole mwarabu me nakushauri uje loliondo kwa babu na jero yako tu upate kikombe cha uzima na kama hutak utaendelea kutapeliwa tu maana hapo bado hujaenda kwa sheik yahya atakwambia kuita jini moja laki 2. magomen ni makaz ya matapeli,wakabaji, walaghai ht mafisadi wapo take care bro.
   
 17. E

  Egyptian Member

  #17
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakumbuka yule mama baada ya kumsikiliza majibu yake mimi niligundua kuwa sio shuhuda bali ni mtu wa karibu na ndodi. Jinsi alivyo anza kujieleza ilionesha hajui ila alimshukuru ndodi,jinsi alivyobanwa kwa maswali na mtangazaji basi alianza kujichanganya na hatimaye nikagundua ni mtaalam wa
  Ndodi pia katika zahanati yake.Sio huyu mama tu bal hata chanel 5(eatv) aliwahi kuleta mabinti wawili na mambo nikaona ni yaleyale kuwa ni wahudumu wake.Naamini wafuatiliaji wa vipindi vyake wanaweza kuongezea juu ya hao mashuhuda.
   
 18. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Magomeni ni makazi ya SHEIKH-TWAIN
   
 19. z

  zamlock JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  jaman huyu bwana ni msabato mwenzangu na mimi na msifu kwa mafundisho yake tu lakini kwa uganga wake sijakubaliana nao mpka kesho kwa sababu navyo wajua wasabato huwa ni watu wa huruma sana na wanapenda kusaidia sana lakini kwa ndondi sijamkubali na sijaona usabato wake kwa watu wenye kuteseka na magonjwa mbali mbali pia kama Mungu ndiye aliyemjalia kuwa na uwezo wa kutibu basi ilitakiwa atumie nafasi hyo kuwasaidia watu kwa ghalama kidogo
   
 20. spike

  spike Member

  #20
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  poleni unaweza kuspendi hela nyingi pasipo kujua wakati ulitakiwa usitumie hata laki moja, kama uko dar ndio rahisi kabisa tafuta simbi nikuelekeze ni dozi ya siku 3, achana na matapeli hao
   
Loading...