Serikali iilipe dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali iilipe dowans

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MJINI CHAI, Feb 7, 2011.

 1. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,765
  Likes Received: 574
  Trophy Points: 280
  Heshima wakuu,
  Nachukuwa nafasi hii kuwasihi wana JF kuangalia upande wa pili wa shilingi, kwani tumekuwa tukiangalia upande mmoja wa shilingi husika, Kuhusu ujio wa RICHIMOND/DOWANS Tanzania Kama sijakosea,
  1. Tanzania yakabiliwa na upungufu wa maji ya kuweza kuendesha Mitambo ya kuzalisha umeme hivyo kupelekea Tanesco kutoa umeme kwa mgao

  2. Mjadala wa upatikanaji wa umeme wa dharura kufanyika ndani ya baraza la mawazili, hoya zikatolewa kuwa
  (a) Wataletwa wataalamu wa Mvua kujaza mabwawa ya Mtera na Kidatu ili umeme upatikane
  (b) Yawashe majenereta ya IPTL kuzalisha umeme hapa mengi yalijitokeza
  (c) Iletwe kampuni ya dharura itakayo zalisha umeme kwa muda huo wa shida na hili LIKAKUBALIKA
  Wapewa dhamana wa nchi hii hapa ndipo Historia itakapojirudia kwa kufuata sheria za nchi yetu na kwa masilahi ya Nchi yetu hata kama tulikuwa na shida waliwaingiza watanzania kwenye Historia Mbaya ambayo haijawahi kutokea hapo nyuma, hivyo basi kwa kuwa tumewapa dhamana Serikali yetu ifanye yafuatayo;

  1. Ikubali kulipa Deni/Tuzo kwa RICHIMOND/DOWANS kwa kuingia mkataba usio na Tija kwa Nchi kwani wa kulaumiwa ni wale tukiowapa dhamana na kutuingiza 'mkenge' hivyo nasisitiza na kuiomba serikali yetu kuwalipa Dowans na wale wote waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria kulingana na nyadhifa zao

  2. Mkurugenzi wa UWT,Mkurugenzi wa TAKUKURU, Mwanasheria Mkuu wa serikali, Waziri wa nishati na Madini, katibu mkuu wa wizara ya Madini na nishati, Hazina, wakurugenzi TANESCO na Mwanasheria wao, na wengineo waliohusika kwa njia moja au nyingine WASHITAKIWE NA WAFILISIWE KUFIDIA deni tutakalo lipa Dowans

  Kutokulipa Deni la Dowans;

  1. Ni aibu kwa Nchi ikinzingatiwa kuwa tuliingia Mkataba
  2. umeme unapokosekana wananchi wa kawaida ndio wanaoumia/kupata shida, mfano hakuna utabibu wa upasuaji mkubwa unaofanyika hata X-rays haifanyiki wengi wanakufa kwa kukosa huduma hizo na kuna taukio mengi ambayo yanawagharimu watu kwa kukosa Nishati hii muhimu

  TAFADHALI SERIKALI LIPENI DENI LA DOWANS
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,992
  Trophy Points: 280
  duhh kazi kwelikweli
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Vipi huwezi kubadili hii title ya thread yako? post nzuri lakini title inatutia kichefuchefu.​
   
 4. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,765
  Likes Received: 574
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni kweli Title inatia kichefu chefu hata wakati naandika hii kitu naumia sana rohoni, lakini ukweli unabaki palepale tuvumilie tu hii hali ya SIMANZI na naamini ndiyo itakayo tupelekea Tanzania kuwa na UADILIFU kwenye mambo ya KITAIFA, kwani hata wenzetu ambao walikuwa na machafuko ni lazima kuwe na JAMBO la simanzi la kulikumbuka ambalo wananchi wake hawataki kulirudia na hapa kwetu kati ya mambo hayo mojawapo ni hili la DOWANS
   
 5. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,765
  Likes Received: 574
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hapo ndipo waTZ tunatakiwa kuangalia upande mwingine wa Coins na tufikie muafaka wa jambo hili, kuna watu wanateseka na kukosekana kwa Umeme kwani Nasikia DOWANS wamegoma kuzalisha umeme
   
Loading...