YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,995
Ili kukuza haraka kilimo na ufugaji Tanzania serikali inatakiwa ifanye mambo yafuatayo
Serikali katika kauli mbiu za HAPA KAZI tu mojawapo ya kauli kama ya wizara ya maji kauli mbiu iwe
"KUHAKIKISHA UPATIKANAJI WA MAJI YA KUTOSHA KWA AJILI YA BINADAMU,MIFUGO NA KILIMO" na nashauri wizara ya maji,mifugo na kilimo iwe wizara moja.
Na ili tufike mbali katika kilimo,ufugaji na maji kuwafikia watanzania wote nashauri
1.Mito yote inayomwaga maji baharini isiruhusiwe kufanya hivyo kwani ni kupoteza maji bure badala yake itengenezewe njia iende maeneo mengine ya Tanzania kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji mkubwa na mashamba ya mifugo sehemu zingine za Tanzania na pia iende kulisha mabwawa ya ufugaji wa samaki wa kibiashara sehemu mbali mbali.
Inauma sana kuona mito inamwaga maji baharini usiku na mchana bure
2.Wizara ya kilimo ianzishe wakala wa kuvuna maji ya mvua na kuyahifadhi kwenye mabwawa makubwa maeneo mbali mbali ya nchi.Mikoa mingi ina milima ambayo kipindi cha mvua maji mengi mno huporomoka kwenye hiyo milima kuelekea mabondeni na baadaye maji hayo kupote bure.Wizara ya kilimo ingeweza kutega hayo maji kwa kuchimba mabwawa makubwa au kuweka vizuizi au mageti kuhakikisha maji yanayoporomoka wakati wa mvua toka milimani yanatiririka kuelekea kwenye mabwawa (resevoir) ya kudaka maji yanayotiririka na kuyahifadhi na kuyatumia kwa kilimo cha umwagiliaji na pia kwa ajili ya mifugo ya kisasa au ufugaji wa samaki na kilimo cha mbogamboga nk
Maji yatiririkayo toka milima mbali mbali yakidakwa yaweza ifanya nchi yote kila eneo kuwa na maji mengi ya kutosha wakati wote kwa matumizi ya binadamu,kilimo na ufugaji.Vijiji vingi vilivyo karibu na milima katika mipango ya maendeleo kila kijiji kiwe na bwawa la kuvuna maji yatiririkayo toka milimani ili yasipotee bure kwa kuzama tu chini ya ardhi.Wayadake na kuyahifadhi kwenye mabwawa yawafae wakati wa kiangazi kwa kuyatumia,kwa mifugo,ufugaji samaki na umwagiliaji
HAPA KAZI TU
yehodaya123@gmail.com