Serikali ifufue Kampuni ya mbegu na kiwanda cha mbolea

Suip

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,338
803
Napenda kishauri serikali hasa Wizara ya Kilimo kuwa fedha inayotumia kwa ruzuku ya pembejeo ingetumika kufufua mashamba ya uzalishaji mbegu hapa nchini kama Tanseed zamani na kiwanda cha mbolea Tanga,
Inavyoonekana serikali inaagiza sehemu kubwa ya mbegu toka nje mathalan mbegu ya mahindi ambayo huagizwa nje kama Zambia,Malawi,Afrika kusini na Kenya na mbolea toka Japani
PhotoGrid_1488206163904.png
PhotoGrid_1488198422798.png
.
Na mbegu hizo huuzwa ghali wastani wa Tsh 6000/=kwa kilo na mbolea huuzwa kati ya Tsh. 60000/=hadi 70000/= kwa mfuko wa kg 50.
Kwa kuwa serikali imefufua shirika la ndege la ATCL ambalo watakaosafiri nalo ni wananchi wachache lakini ukifufua Kampuni za mbegu na kiwanda cha mbolea utakuwa umwasaidia Watanzania zaidi ya 70% ambao ni wakulima kwa kuweka ruzuku kwenye hayo makampuni na wakulima kupata pembejeo kwa bei ya chini ya Kg ya mbegu kuuzwa kwa Tsh 3000na mbolea kupatikana kwa bei ya 35000-40000/=kulikoni mawakala wanasambaza pembejeo kuchukua fedha za serikali bila kuwapatia pembejeo halali.
Kuna taasisi kama Seliani na Lyamungo wamefanya utafiti mbalimbali za mbegu lakini sina hakika kama wamefanikiwa kiasi gani kwani nadhani hawana fedha za kutosha na pia baada utafiti inatakiwa makampuni ya kuzalisha mbegu hizo na kusambazwa kwa wakulima.
Kuna uzi humu kuhusu kilimo cha mahindi mbegu nyingi ni za toka mwaka 1983-2001na nyingi leo hata madukani haipo tena leo utakutana Panar ya Afrika kusini,Seedco toka Malawi,Dekalb(DK)toka Zambia nk. sina hakika kama inatoka huko au inazalishwa hapa Tanzania na vifungashio vinaagizwa huko jambo ambalo sio ajabu kwa nchi yetu kama mbolea inatengenzwa Minjingu na vifungashio vinatoka Kenya vikiwa na lebo ya kwamba mbolea imetengenezwa Kenya.
 
Umenena vyema kipaumbele kingekuwa hiki kuliko jet.
Hii ni hatari kwakweli kama kiwanda cha mbolea MINJINGU kipo Tanzania lakini kifunganishio made in Kenya..pasi na aibu mbele ya waziri mkuu mmiliki anatoa kifungashio chenye nembo ya Kenya
 
Back
Top Bottom