mjinga asiyejielewa ndiye analiwa..... mkuu hii bashara ni world wide, wamiliki wa hizi biashara wapo kisheria na kodi wanalipa, tena wanalipa kodi kubwa sana.
wenzetu walioendelea mtu ana bet huku akiwa ana offic yake au shughuli zake nyingine zinazomwingizia kipato, sasa kibongo bongo unamkuta kijana anashinda majumba ya betting anasubiri mechi iishe ili aangalie kama mkeka unasoma achukue chake, au unakuta mtu anabet live ile michezo ya namba...cjui inaitwaje. imefika sehemu mtu anategemea betting kama ndio kipato chake, waathirika wakubwa ni sisi vijana.
sioni kama serikali inakosea kuwapa vibali hawa wawekezaji, wajinga ni hao wanashikwa masikio na kubet 24/7. pia kuna zile mashine za kichina (dubwi) ambazo ni kamari unadumbukiza mia mbili, zimesheheni sana, wajinga ndio waliwao.