Serikali ifuate ushauri wa CHADEMA

MZALAMO

JF-Expert Member
Jul 6, 2009
1,758
1,967
Kwa kuwa wapinzani wengi hasa CHADEMA wanashauri maendeleo si ya vitu ila yanatakiwa yawe ya watu, napendekeza serikali ifute ruzuku kwa vyama vya siasa ili pesa yote inayotolewa kwa ajili ya ruzuku itumike katika maendeleo ya watu vijijini, tofauti na ilivyo sasa pesa za ruzuku zinatumika kununulia vitu kama magari ambapo ni tofauti na msimamo wa wana CHADEMA walio wengi.

Kwa mfano ruzuku ya CHADEMA ni kama bilioni tatu kwa mwaka pesa hizi zisitolewe tena kama ruzuku kwa CHADEMA ila zipelekwe vijijini zikalete maendeleo kama wao wanavyoshauri pia kwa vyama vyote vinavyopata ruzuku iwe hivyohivyo.
 
vyama vya siasa ni WATU wewe mataga. vitu ni kama midege mnayoendelea kununua.
 
Ruzuku nayo ifutwe tu pesa ziende kuleta maendeleo vijijini.

..hilo halitafanyika, kwasababu watakaoumia zaidi ni ccm.

..viongozi wengi wa cdm haswa kwenye kanda na mikoani hawalipwi mishahara.

..wakati huohuo viongozi wa CCM wamezoea kuishi KIBWANYENYE wakitegemea RUZUKU kubwa na VYEO serikalini.

..CCM inapata ruzuku mara 9 au 10 kulinganisha na wanayopata CDM. Katika mazingira hayo usitegemee CCM waondoe ruzuku. Makada wao wataishi vipi?
 
Sasa kama watakaoumia ni CCM kwanini Chadema hawataki kusikia ruzuku ikifutwa?
 
..kama ruzuku ingekuwa inawafaidisha cdm kuzidi ccm, basi by this time ccm wangekuwa wameishaifuta.

..ukumbuke ccm wana wabunge wengi hivyo hawashindwi kuondoa jambo lolote lile wasilolipenda.

..Ruzuku inawafaidisha CCM kuzidi vyama vya upinzani, na ndiyo maana CCM hawaifuti.

..Hata nafasi mbalimbali za uteuzi wa Raisi ambaye ni mwenyekiti wa CCM, kwa mfano wakuu wa mikoa na wilaya, CCM wanataka ziendelee kuwepo kwani ni kichaka cha kupachika makada wao wasiokuwa na qualifications na wasiomudu ushindani ktk soko la ajira.

..Jambo lingine wasilolitaka CCM ni kutenganisha Uraisi na Uenyekiti wa chama.
 
Tusiangalie chama gani kinanufaika na ruzuku ifutwe tu kwa vyama vyote.
 
..sawa.

..lakini ccm kwasababu wana wabunge wengi, na wameunda serikali, ndiyo wenye uwezo wa kufuta ruzuku ya vyama vya siasa.

..pia itungwe sheria inayozuia Raisi kuwa Mwenyekiti wa chama cha siasa.

..Na nafasi za wakuu wa wilaya nazo zifutwe
hazina tija na mzigo kwa walipa kodi, badala yake tubakiwe na wakurugenzi wa wilaya.
 
..hilo halitafanyika, kwasababu watakaoumia zaidi ni ccm.

..viongozi wengi wa cdm haswa kwenye kanda na mikoani hawalipwi mishahara.

..wakati huohuo viongozi wa CCM wamezoea kuishi KIBWANYENYE wakitegemea RUZUKU kubwa na VYEO serikalini.

..CCM inapata ruzuku mara 9 au 10 kulinganisha na wanayopata CDM. Katika mazingira hayo usitegemee CCM waondoe ruzuku. Makada wao wataishi vipi?
Basi wabunge wa CDM, wapeleke hoja binafsi kwa Spika kwamba Ruzuku ya vyama ipeleke maji vijijini tuone
 
Wao chadema wamejishauri nini na kukifuata? Wanapokea ruzuku, kodi zetu, za mabilioni kila mwaka, umeona wamefanya nini cha maana kwa wananchi? Chadema si imegeuka kuwa kitegauchumi cha mfalme mbowe na genge lake bila kufanya chochote kwa wananchi (angalia halmashauri za miji/wilaya/vijiji wanaziongoza), wala chama chao (wameshindwa hata kujenga ofisi); then wewe unataka ushauri wao ufuatwe!
Mtu aliyeshindwa kufanya kitu chochote cha maana, na anayepinga kila kitu akikupa ushauri na ukaufuata, ni sawa na mkristo kupewa ushauri na shetani na akaufuata.
 
Sasa kama watakaoumia ni CCM kwanini Chadema hawataki kusikia ruzuku ikifutwa?

Muandikie barua rasmi rais wala usitegemee jf pekee, na umsisitizie afute hiyo ruzuku hata kesho. Wanaccm ndio wamezoea maisha ya upendeleo hivyo huwa mnadhani kila mtu anaweza kutishiwa na hiyo ruzuku. Narudia tena mwambie aifute hiyo ruzuku hata kesho.
 
Basi wabunge wa CDM, wapeleke hoja binafsi kwa Spika kwamba Ruzuku ya vyama ipeleke maji vijijini tuone

Hamna bunge bali kuna mitume wa Magufuli huko bungeni. Kwakuwa hilo bunge limejaa makondoo wanaotii kila kitu atakacho rais, msipoteze muda, muambieni rais yeye atakachosema hilo bunge dhaifu litatekeleza. Kwakuwa ameweza kupiga marufuku wapinzani kufanya siasa, anaweza futa hiyo ruzuku hata usiku huu ili maendeleo yapatikane vizuri.
 
Basi wabunge wa CDM, wapeleke hoja binafsi kwa Spika kwamba Ruzuku ya vyama ipeleke maji vijijini tuone

..ccm wataipinga.

..ccm wana tabia ya kupinga kila pendekezo la cdm.

..hakuna hoja inayoweza kupita ktk bunge la Ndugai, Tulia, na ccm, bila kuwa imependekezwa na serikali au wabunge wa ccm.
 
Kwa kuwa wapinzani wengi hasa CHADEMA wanashauri maendeleo si ya vitu ila yanatakiwa yawe ya watu, napendekeza serikali ifute ruzuku kwa vyama vya siasa ili pesa yote inayotolewa kwa ajili ya ruzuku itumike katika maendeleo ya watu vijijini, tofauti na ilivyo sasa pesa za ruzuku zinatumika kununulia vitu kama magari ambapo ni tofauti na msimamo wa wana CHADEMA walio wengi.

Kwa mfano ruzuku ya CHADEMA ni kama bilioni tatu kwa mwaka pesa hizi zisitolewe tena kama ruzuku kwa CHADEMA ila zipelekwe vijijini zikalete maendeleo kama wao wanavyoshauri pia kwa vyama vyote vinavyopata ruzuku iwe hivyohivyo.
Naunga mkono hoja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom