Serikali ifanye yafuatayo kwa haraka kulinusuru taifa

mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Posts
4,118
Reaction score
1,973
Wakati juhudi za kupambana na janga hili zikiendelea,kuna mambo ya msingi na muhimu kama nchi nahisi hayajaenda sawa. Kwa haraka haraka na bila kuchelewa nashauri serikali kufanya mambo yafuatayo:

1. Upo uhaba wa vitendea kazi kwa watumishi zikiwemo Mask aina N95 ambazo kwa mujibu wa Naibu Waziri wa afya,ni watumishi tu wanatakiwa kuzivaa, serikali itaifishe mask za aina hii kwenye maduka yote nchini ikiwemo kuzikusanya na kuzipeleka kwenye bohari za dawa.

2. Mheshimiwa Rais amezungumza wazi kuhusu baa la njaa. Hali ya hewa tuliyonayo ni uhalisia kuwa hakuna uwezekano wa kuwa na chakula cha kutosha muda mfupi ujao.Serikali ichukue hatua haraka na kuzuia kusafirisha chakula nje ya nchi. Hii itegemee na uhalisia wa uwepo wa chakula kwenye ghala la taifa walau cha miezi 10 mpaka 12.

3. Budget ya dharura wizara ya afya ipitishwe ikiwemo kununua vipimo vya COVID-19 na kila mkoa uwe nayo ili kubaini hali halisi.

4. Vifaa vikishakuwepo tuwe na mandatory testing kwa raia wote ili kuwa na takwimu sahihi na pengine kuzuia kasi ya kuendelea kuenezeana.

5.Serikali ifuate ushauri wa Spika kuepuka nchi kuwa kwenye confusion.Leo hii matamko ya ugonjwa huu ni mengi.Tuwe na one stop centre badala ya kuwaacha wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa, mawaziri,maaskari kila mtu anakuja na tamko lake.Mfano kwa sasa watu wa Dar es Salaam hawatakiwi Iringa.

7. Mpaka sasa hatuna COVID-19 Protective and Prevention Rregulations ambazo pengine ndo ungekuwa msaafu na rejea kwa viongozi na watumishi.Kanuni hizi Zitungwe upesi sana.

8. Viwanda vyetu vya ndani-SIDO vianze mara moja kuzalisha bidhaa kama barakoa zenye kiwango na kuwauzia watu kwa bei ambayo wataimudu.Hii itasaidia kuepusha kila mtu kutengeneza barakoa zisizo na kiwango.

9. Kuna haja ya kurudisha kwa muda tume ya Bei (Price Regulation Commission) ili kudhibiti upandaji holela wa vyakula na bidhaa muhimu maana kila mtu yuko kwenye taharuki na huo umekuwa mwanya kwa wafanyabiashara kupamdisha bei maradufu.

10. Kuna baadhi ya watumishi wa umma nadhani sasa watumbuliwe maana kwa matamshi yao hawatusaidii kama taifa.
 
Mambo mazuri hayo mkuu,lakini hilo la wakulima kukosa fursa za bei za masoko nje na ndani hapana.
Wakulima wanateseka sana,ikiwa kwao ni fursa acha waipate.Serikali ina facilities za kuhifadhi vyakula na Niko bodi za kununua na kuhifadhi mazao, wafanye hivo,mkulima muache apate ni faida kwa nchi pia kuliko kumnyima fursa za kukua
 
We ndugu!! This year kuna baa la njaa???

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
La msingi serikali hata kama itazuia inunue mazao hayo kwa bei ya soko
 
We ndugu!! This year kuna baa la njaa???

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature

Inawezekana mkuu maana rais alisema kutakuwa na upungufu wa chakula
 
Raisi wa Zimbabwe aliulizwa umejipangaje na Corona akasema tume jenga mortuary za kutosha.

11. Mashine za oxygen Ni changamoto
 
Back
Top Bottom