Serikali ifanye AUDIT ya wafanyakazi wake wote(isipokuwa wale wa vyombo vya usalama)

moma2k

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
1,091
1,405
Serikali pamoja na taasisi zake kuna wafanyakazi wengi sana.Karibu 1/3 hawahitajiki katika zama hizi za mawasiliano ya TEHAMA na matumizi makubwa ya computer. Ukienda maofisi ni aibu tu.Ofisi nzima wamejaa wao wanapika stori/michapo tu. No effectiveness, poor work performance,hakuna tija.Pendekezo:
Wafanyakazi wasiohitajika wakafanye kozi ya mwaka moja ya kufundisha shule za msingi. Then waende kufanya kazi huko kwenye upungufu mkubwa wa walimu wa shule za msingi.Vinginevyo idadi kubwa hii isiyo na tija ni mzigo mkubwa kwa sisi walipa kodi. Kuna kipindi watu waliajiriwa hovyohovyo.
 
kwan usalama wao ni malaika au?pia kwa mtazamo wangu ni kwamba hao ndio ingebid hyo auditing(kama ulivosema ingawa nadhan hujajua maana halisi ya auditing) iwape priority maana wao ndio wanashikilia uhai wetu,ili uajiliwe katika hivo vyombo nadhan ni lazima uwe na vigezo vyao mf elimu na nk so kama mtu hana vigezo ila tukamkabidhi uhai wetu its not too late kumuondoa kwa usalama wetu
 
Serikali pamoja na taasisi zake kuna wafanyakazi wengi sana.Karibu 1/3 hawahitajiki katika zama hizi za mawasiliano ya TEHAMA na matumizi makubwa ya computer. Ukienda maofisi ni aibu tu.Ofisi nzima wamejaa wao wanapika stori/michapo tu. No effectiveness, poor work performance,hakuna tija.Pendekezo:
Wafanyakazi wasiohitajika wakafanye kozi ya mwaka moja ya kufundisha shule za msingi. Then waende kufanya kazi huko kwenye upungufu mkubwa wa walimu wa shule za msingi.Vinginevyo idadi kubwa hii isiyo na tija ni mzigo mkubwa kwa sisi walipa kodi. Kuna kipindi watu waliajiriwa hovyohovyo.
Jipange upya, kwa Tanzania wafanyakazi ndio wanaoongoza kwa kulipa kodi hivyo ni almost wanajilipa wenyewe. Na maprof waliopo gvt wakafundishe darasa la kwanza? Either ni stress au matumizi ya " prohibited substance"
 
Acha hizo hao unaoona hawafai maofisini nao wana familia na wana uzoefu mkubwa. Je wakipunguzwa familia zao utazilisha wewe?

Wasomi hawa hawa kila siku mnawalaumu hasa wale professa waliopata vyeo vikubwa wamekuletea maendeleo gani?

Umeona sekta ya elimu ni jalala kwa hao unaoona hawafai maofisin aiseee ukapimwe akili,wakienda kufundisha huko shule watazalisha taifa gani la mbelen sasa?

Mwisho Tanzania haina upungufu wa walimu bali inabania ajira za walimu. Kuna walimu wengi wenye taaluma zao wameachwa tu bila kuajiriwa kisingizio nafasi zimejaa
 
Itakuwa kazi umepata juzi hata probation hujamaliza bado... Utaanza kuachishwa wewe wakongwe utawaacha hapo hapo...

Pole sana...

Cc: mahondaw
 
Acha hizo hao unaoona hawafai maofisini nao wana familia na wana uzoefu mkubwa. Je wakipunguzwa familia zao utazilisha wewe?

Wasomi hawa hawa kila siku mnawalaumu hasa wale professa waliopata vyeo vikubwa wamekuletea maendeleo gani?

Umeona sekta ya elimu ni jalala kwa hao unaoona hawafai maofisin aiseee ukapimwe akili,wakienda kufundisha huko shule watazalisha taifa gani la mbelen sasa?

Mwisho Tanzania haina upungufu wa walimu bali inabania ajira za walimu. Kuna walimu wengi wenye taaluma zao wameachwa tu bila kuajiriwa kisingizio nafasi zimejaa

Mambo ya familia hayana uhusiano na mtu kupata ajira.Kwani sisi walipakodi hatuna familia?Mbona muda ukifika huwa wanastaafu bila kuleta agenda ya familia? Hiyo siyo hoja.
 
Back
Top Bottom