Serikali ieleze itakavyopata pesa mechi ya Yanga na T.P Mazembe

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,700
1,721
Wakati Rais Magufuli anahimiza wananchi tulipe kodi, wengine wanajitahidi kupingana nae. Jana j2 klabu ya Yanga imetangaza wananchi wataingia bure uwanja wa Taifa (wa Serikali na sio wa Yanga) na nasikia waziri Nape kawaomba wananchi waishangilie (kiswahili cha siku hizi 'sapoti') timu ya Yanga kesho kwa nguvu zote.

Sasa najiuliza kama watu wataingia bure uwanjani serikali itapataje mapato? Au michezo hasa soka serikali huwa haipati chochote? Kama serikali inaambulia patupu basi hilo ni JIPU.
 
Wakati Rais Magufuli anahimiza wananchi tulipe kodi, wengine wanajitahidi kupingana nae. Jana j2 klabu ya Yanga imetangaza wananchi wataingia bure uwanja wa Taifa (wa Serikali na sio wa Yanga) na nasikia waziri Nape kawaomba wananchi waishangilie (kiswahili cha siku hizi 'sapoti') timu ya Yanga kesho kwa nguvu zote. Sasa najiuliza kama watu wataingia bure uwanjani serikali itapataje mapato? Au michezo hasa soka serikali huwa haipati chochote? Kama serikali inaambulia patupu basi hilo ni JIPU.

wanasema eti Yanga ni timu ya wananchi na kodi inayotokana na uwanja ni kwa ajili ya wananchi hao hao. so eti wakiingia uwanjani bure kodi itakuwa imejilipa kiaina na kutumika kiaina kwa wananchi wale wale waliokusudiwa na kodi ile ile kutoka kwa watu wale wale na kwa style ile ile kutoka Lumumba kule kule!
 
Nimeshindwa kujizuia kuchekaaa!! teheeee teh !teheeee.......
 
Yusuf Manji kasha walipia mashabiki wote shs million 600, kama wangakata tiketi zisingefika hela hizo zingefika sana million 450
Kama kafanya hivo ni vema. Navojua mie kila mtu hutakiwa kuingia uwanjani kwa kuonesha tiketi yake mlangoni sasa hilo litafanyika kwa maana ya kila mtu atapata tiketi yake iliyolipiwa?
 
Tatizo yanga wakishinda kuna jamaa anaitwa Muro! Anadharau sana.. Mbona tutakoma
 
Ushaambiwa ni Bure so Na Serikali itapata mgao wake sifuri... maana asilimia ya vat ni 18 hivyo Asilimia 18 ya Sifuri ni Sifuri shida nini? Dawa ya Jeuri ni Makusudi... Si Mmechukua coco beach yenu!
 
Wakati Rais Magufuli anahimiza wananchi tulipe kodi, wengine wanajitahidi kupingana nae. Jana j2 klabu ya Yanga imetangaza wananchi wataingia bure uwanja wa Taifa (wa Serikali na sio wa Yanga) na nasikia waziri Nape kawaomba wananchi waishangilie (kiswahili cha siku hizi 'sapoti') timu ya Yanga kesho kwa nguvu zote.

Sasa najiuliza kama watu wataingia bure uwanjani serikali itapataje mapato? Au michezo hasa soka serikali huwa haipati chochote? Kama serikali inaambulia patupu basi hilo ni JIPU.
Hivi nano kasema watu wataingia bure jamani
 
Back
Top Bottom