Serikali ieleze itakavyopata pesa mechi ya Yanga na T.P Mazembe

Yusuf Manji kasha walipia mashabiki wote shs million 600, kama wangakata tiketi zisingefika hela hizo zingefika sana million 450
Hizi pesa zote si bora wangeendelea kujenga uwanja wa kaunda kuliko kutoa bure ,mana sizan kama yanga wamefikia utajiri mkubwa sana wakudhidi virabu vya chelsea,man,real na vingine ambavyo havijawah kuruhusu washabiki waingie bure ili hali timu zina viwanja binafsi tofaut na yanga kutegemea uwanja wa taifa.Mapato ya kiingilio huifanya timu iwe strong kiuchumi tofaut na yanga wanavofanya.
 
Karibuni Taifa bana hizo ndo jeuri za watoto wa jangwani igeni kama amjauza basi la club THIMBA
 
Ushaambiwa ni Bure so Na Serikali itapata mgao wake sifuri... maana asilimia ya vat ni 18 hivyo Asilimia 18 ya Sifuri ni Sifuri shida nini? Dawa ya Jeuri ni Makusudi... Si Mmechukua coco beach yenu!
Hv mil 600 hazitoshi kuanza kusafisha eneo la uwanja na kuset msingi? Na usalama wametuhakikishiaje maana watakuja hata wasiojua idadi ya wachezaji mle ndani.
 
ukiona hivyo, ujue wanataka kuhalalisha uchotaji ela mahala fulani! Pia hii inadhihirisha klabu haina mipango ya muda mfupi ama mrefu kwa ajiri ya kujiendesha kwa faida. Tuwasikitikie tu!
 
Wakati Rais Magufuli anahimiza wananchi tulipe kodi, wengine wanajitahidi kupingana nae. Jana j2 klabu ya Yanga imetangaza wananchi wataingia bure uwanja wa Taifa (wa Serikali na sio wa Yanga) na nasikia waziri Nape kawaomba wananchi waishangilie (kiswahili cha siku hizi 'sapoti') timu ya Yanga kesho kwa nguvu zote.

Sasa najiuliza kama watu wataingia bure uwanjani serikali itapataje mapato? Au michezo hasa soka serikali huwa haipati chochote? Kama serikali inaambulia patupu basi hilo ni JIPU.
Nadhani kama ungetaka majibu ya swali hili kuna taratibu za kufwata ili upate taarifa sahihi,sasa unauliza humu jf ukitegemea majibu,serikali inafanya kazi zake kwa utaratibu taarifa ya serikali utaipata sehemu husika ila sio kwenye mitandao ya kijamii,zaidi humu utapata taarifa za kishabiki na zisizo sahihi.
 
Hv mil 600 hazitoshi kuanza kusafisha eneo la uwanja na kuset msingi? Na usalama wametuhakikishiaje maana watakuja hata wasiojua idadi ya wachezaji mle ndani.
Nasikia mtoa Offer ni Teja so ana akili za kiteja pondamali kufa kwaja... kama anawapenda Yanga awajengee uwanja na pesa hizo zingetosha sana kuanzia... sidhani wapenzi wa Yanga ni masikini kiasi hicho hadi wapende vya bure... kawatukana sana
 
Watu hatuna Pesa wengine wanazichezea... Ni Ngumu kufanya watanzania wote waishi kishetani
 
Huyu gabacholi analeta dharau, watu tunataka starehe kwa hela zetu yeye anatupa offa tudiyo muomba. Kama ana hela ya hivyo si angepeleka kwenye madawati? Au angenunua tiketi kadhaa akawatangazia wapenda bure wakafoleni kwake kuchukua tiketi za bure?
Mkuu, pana taarifa kuwa hiyo haikuwa BURE ila watu walilipa kiingilio kwa kununua jezi hizo uongozi wa Yanga ukaua ndege wawili kwa jiwe moja.
 
Back
Top Bottom