Serikali ichukulie kwa uzito vitisho hivi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ichukulie kwa uzito vitisho hivi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Nov 22, 2011.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kabla sijaanza kutoa maoni yangu naomba ninikuu moja ya vyombo vya habari vya hapa nchini. Japo siyo lazima tuamini kila kinacho andikwa na magazeti yetu naamini kuna badhi ya taarifa ni muhimu kuchambuliwa zaidi. Chini nanukuu taarifa kuwa raisi Jakaya Kikwete kapewa siku 100 kujiudhuru au asubirie kutolewa kwa nguvu. Kwenye nchi zilizo endelea kama Marekani, kila tishio kwa raisi, liwe dogo au kubwa huchunguzwa. Kwa maana hiyo basi hata kama vitisho hivi ni udaku au tetesi tu natumai vyombo husika vina fanya uchunguzi juu ya hili swala. Kama wazungu wananvyo sema "Better safe than sorry".

  Kwanza nianze kwa kusema kuwa naamini hali ya nchi sasa ni mbaya, na nasema hivi bila kutupa lawama yoyote ile kwa mtu yoyote ile. Hali yetu ni mbaya na tuna hitaji kutafuta suluhisho. Umeme sasa umekua adimu kuliko kipindi chochote kile, mafuta yamepanda bei, chakula kimepanda bei na hali kadhalika maisha kiujumla yamezidi kuwa magumu. Kwa maoni yangu mimi hii hali inaendelea kwa sababu viongozi wa nchi wameshindwa na wamekataa kuelewa hali wanayo pitia wananchi. Kwa vile wao hawakatiwi umeme, hawanunui mafuta na wala hawalali na njaa imekua ngumu kwao kushughulikia matatizo haya kwa haraka kwa vile hali hii haijawagusa.Ila sasa kama hali ya usalama wa nchi imekua mbaya mpaka kuna kikundi cha wanajeshi kina taka kuasi na kumuondoa raisi madarakani basi hali ni mbaya. Viongozi wetu wanaweza wasi athiriwe na mgao wa umeme wala bei ya vya kula lakini usalama ina tugusa wote sisi. Tumeona mifano mingi Afrika ambapo jeshi likichukua nchi badala ya demokrasia tuna pata udikteta au vita za wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi. Kama hii haiwatishi viongozi wetu je hawaogopi usalama wa maisha yao, familia zao na mali zao?

  Pia kikundi cha Al Shabaab kina semekana kuweka kambi nchini Tanzania. Mara zote vikundi vya kigaidi huweka kambi kwenye nchi au maeneo ambayo hakuna uongozi imara wala vyombo vya usalama vyenye uwezo wa kulinda mipaka ya nchi. Kama tumefika katika hali ambayo makundi ya kigaidi wanaweza kuweka kambi nchini kwetu basi viongozi waogope sana.Kwa hiyo ndugu zangu ninacho taka kusema kuwa mpaka sasa matatizo yetu sisi wananchi wa kawaida haija wagusa viongozi wetu ila huko tunapo elekea hawa viongozi wetu wana weka usalama wao wenyewe hatarini? Labda bado hawaamini kuwa nchi inayumba na kukaribia kudondoka. Labda mpaka maafa yawa kute ndiyo wata gundua hatari iliyopo. Nawasihi sana viongozi wachukulie vitu seriously kwa maana vitu walivyo kuwa wakidhani vina waathiri wananchi wa kawaid atu hivi karibuni vitaanza kuwa athiri na wao.

  Mwishoni niseme kwamba labda hivi vitisho kutoka kikundi cha wanajeshi na hao Al Shabaab si kubwa. Labda hawana uwezo wa kutekeleza hayo wanayo dai. Ila swali langu ni je wako tayari kuweka maisha yao rehani? Kama wananchi watakata tamaa na kuamua liwalo na liwe ni nani atawalinda viongozi hawa? Viongozi wakumbuke kuwa hawalindwi na viongozi wenzao bali na wananchi wa kawaida ambao ni polisi, wanajeshi au wafanyakazi wa usalama. Pale matatizo ya maisha yatakapo anza kuwa gusa hawa wanao walinda viongozi basi waogope sana.Mimi ni mwananchi wa kawaida tu. Sijui kiundani wa maswala haya. Naweza nikawa nimekuza swala hili. Ila natambua kabisa kwamba lisemwalo lipo na kama halipo yaja.
   
Loading...