Serikali ianzishe mpango wa elimu kwa watu wazima

Serikali ianzishe mpango wa elimu kwa watu wazima

ShalomP

Member
Joined
Jun 14, 2019
Posts
97
Reaction score
154
Naiomba serikali ianzishe elimu maalumu ya watu wazima ambao hawakubaatika kujifunza Kwenye mtaala rasmi. Yaani waanzishe mtaala usio rasmi kwa ajili ya watu ambao hawajui kusoma Wala kuandika.

Katika harakati zangu za kusaka maisha Kuna baadhi ya vijiji nimetembelea na kukuta Kuna baadhi watu hawajui kusoma Wala kuandika ambao baadhi yao ni vijana na wazee. Zipo sababu nyingi zilizopelekea tatizo hili baadhi yake ni migogoro ya kifamilia hasa masuala ya ndoa, Amani inapokosekana ndani ya ndoa hupelekea watoto kutangatanga na kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Pia mazungira ya vijijini Kuna changamoto nyingi sana ambazo huja kupelekea mtu kukosa kupata elimu ya mtaala rasmi.

Napendekeza hayo masomo yangekuwa yanafundishwa jioni kwa sababu wengi wao tayari wana familia muda mwingi wanakuwa Kwenye shughuli za uchumi za uzalishaji Mali.

Masomo hayo yawe manne ambayo somo la kujifunza kusoma na kuandika, somo la afya, somo la stadi za kazi au ujasiliamali na somo la hesabu. Somo la kusoma na kuandika (kiswahili) liwe la Kila siku kwa sababu ndio lengo kuu. Muda wa kusoma unaweza kuwa kuanzia saa kumi na moja jioni Hadi saa moja jioni angalau masaa mawili angalau ndani ya miezi mitatu lengo liwe limetimia. Waandaliwe walimu maalumu wapya watakaoajiliwa ambao watapelekwa vijijini moja kwa moja kwa ajili ya kazi hiyo.

Pia hata mijini kama wapo wenye tatizo la kutokujua kusoma na kuandika mpango huo ufanyike, Wizara husika zinazohusika na maswala ya elimu ninaomba walitendee kazi swala hili.

#ni mtazamo wangu tu.
 
Back
Top Bottom