Serikali iangalie upya namna ya kupambana na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya nchini!

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Kwa waliosoma magazeti leo, moja ya taarifa zilizoshtua ni jinsi wimbi la wasanii wetu wanajiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya linavyozidi kuwa kubwa.

Waliotajwa kama waliokwisha athirika vibaya ni pamoja na:-
.FEROUS
. DAZ BABA
. RAY C
. Q CHILLA
. CHID BENZ na wengineo.

Hawa ni baadhi tu, tena toka kundi la wasanii. Lakini wapo wengi wengine walio na wasio wasanii.

Nimetafakari STYLE na EFFECTIVENESS ya mikakati ya Serikali yetu ya kupambana na biashara hii nchini nimeona kuna walakini mkubwa.

Udhaifu namba moja ni kuwa vita yetu inaelekezwa kwa upande mmoja tu ambao ni kutafuta wauzaji wa madawa haya huku tukiacha kushughukia watumiaji.

Napenda kushauri sheria zetu zishughulikie wote wawili MUUZAJI na MNUNUZI/MTUMIAJI. Bila hivyo hatutaishinda vita hii.

Hata katika sheria ya Rushwa MTOAJI na MPOKEAJI wote wanashughulikiwa, iweje kwenye suala zito na la hatari kwa vizazi vya taifa letu kama hili, tushindwe?!
 
DAWA ZA KULEVYA TISHIO KWA WASANII, VIJANA.

C1TfdoJXcAAH8Vf.jpg
 
Duh!! Madawa ya kulevya ni nyoko!! Wasnii walioko juu kwa sasa ni muda muafaka wa kutafuta pesa na kuwekeza katika sehemu sahihi ili hata siku ukiishiwa mistari kwa muda uendelee kuishi katika level za juu. Vijana wapunguze starehe na wapige mahesabu ya miaka 30 mbele.
 
Tuwalee watoto wetu katika maadili mema ya kidini ktk makuzi yao na kujua mema na mabaya

Malezi bora ya DINI na elimu bora ya uraia kusaidia sana kujenga kizazi chenye maadili mema.

Vita ya madawa ya madawa ya kulevya iliyoanza miaka ya 1980 ni vita ambayo inatumia gharama kubwa sana na mataifa mengi yametunga sheria Kali sana mpaka kunyonya mfano China lakini bado shida ndiyo kwanza inaongozeka!

Kuna haja ya wadau wa vita hii kukutana pamoja na kujadili nini kifanyike ili kuwapunguzia madhara watumiaji wa madawa ya kulevya.

R.I.P wote waliokufa kwa madawa ya kulevya
 
Back
Top Bottom