Waswahili wanasema "kupanga ni kuchagua", hivi tunaona jinsi vijana wsnavyohangaika kupata mikopo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu lakini kutokana na ufinyu wa bajeti ni wachache wamepata karibia nusu ya wale walioomba.
Kiwango hiki cha waliokosa ni kikubwa sana vijana zaidi ya elfu 30 wamekosa mikopo kwa ajili ya masomo yao ya juu, sasa basi ushauri wangu ni kwamba serikali iachane na mpango wa elimu bure baadala yake pesa za elimu bure zipelekwe kwenye mikopo ili wote wenye uhitaji wapate mikopo.
Kwanini nimetoa ushauri huo, elimu ya msingi na sekondari gharama zake ni ndogo ambazo mzazi anaweza kuzimudu tofauti na elimu ya chuo kikuu, kama serikali ikifanya tunaweza pata zaidi ya bilioni 200 ambazo zitakopesha vijana wengi zaidi, kuliko hivi sasa ambapo vijana hawa watakaa nyumbani na kuikosa elimu.
Kwa shule za msingi na sekondari Serikali iwajibike kulipia wale tu watakaokuwa hawana uwezo.
Nawasilisha.