Kinachoonekana kwa sasa ni huu Utawala wa Rais Magufuli kujikita kwenye siasa za chuki dhidi ya Wapinzani. Karibu Wabunge na Viongozi wote wa Upinzani kwa sasa wana aidha kesi 1,2 au 3 hadi 8 kama Mhe. Tundu Lissu zinaendelea Mahakamani na wengine wako Mahabusu. Kesi zote zinahusu UCHOCHEZI na hakuna kesi ya UFISADI, WIZI au KUGHUSHI NYARAKA zozote...!!
Nitarejea kesi mbili muhimu zinazowahusu Wabunge machachari wa CHADEMA. Kuna Mhe Godbless Lema(MB-Jiji la Arusha) na Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu(MB-Jiji la Mbeya). Kesi zote zina dhamana kulingana na Haki,Sheria na Katibaya nchi lakini kwa maksudi Mhe. Lema alikaa mahabusu miezi 4 pamoja na juhudi zote za kumpigania atoke kwa dhamana. Jambo lilelile lilofanyika Arusha kwa sasa linajirudia Mbeya mjini kwa Mhe. Sugu na kwa mazingira yaleyale ya madai ya kumkosoa Rais Magufuli hivo kufunguliwa kesi ya Uchochezi na kunyimwa dhamana.
Tayari kuna kila dalili ya kumfanya Mhe. Sugu aendelee kusota remande kwa kesi ya Uchochezi kwa wiki, miezi au hata mwaka huku ushahidi wa upande wa Serikali ikiwa ni kanda iliyorekodiwa tarehe 30/12/2017 katika mkutano wa Mbunge wa Mbeya akiwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu ikionyesha kuwa alimkosoa Rais au kumkashfu....!!!Upande wa Serikali wanang'ang'ania kuwa Mhe. Mbilinyi na Mhe.Emmanuel Masonga-Katibu CHADEMA Nyanda za Juu Kusini kuwa hawawezi kupewa dhamana maana itahatarisha usalama wao...!!!Sijui ni kwa vipi na kwa namna gani. Kwamba watuhumiwa walitoa lugha sijui chafu au ya kumkosoa Rais iwapo wakipewa dhamana watahatarisha usalama wao..!!!Kivipi??Haingii akilini.
Kama Rais Magufuli juzi kwenye sherehe za Uhuru waJMT aliweza kuwaachia HURU watu waliokuwa wamefungwa JELA MAISHA au HUKUMU YA KIFO kwa kesi za MAUAJI na KUBAKA WATOTO WACHANGA, inakuwaje Waheshimiwa Wabunge wa UPINZANI ambao ni Viongozi wa Wananchi kwa kuchaguliwa tena kwa kura nyingi sana kwenye majimbo yao wanang'ang'aniwa kwa kesi za kutengeneza kwa kisingizio cha Uchochezi??? Naomba Mahakama Kuu ya Tanzania iingilie kati na itoe TAFSIRI au ufafanuzi wa neno UCHOCHEZI na ni wakti gani mtu au raia anaangukia kwenye makosa ya UCHOCHEZI.
Haiwezekani mtu aliyaua, aliyebaka au kulawiti, aliyeiba au kufisidi leo anapewa msamaha wa Rais Magufuli huyuhuyu ambaye hataki Mbunge wa Upinzani apewe dhamana kwa kutumia haki yake ya Kikatiba kama Raia wa Tanzania na Mbunge kuikosoa Serikali yake anawekwa Mahabusu na kufunguliwa kesi za Uchochezi na ikibidi afungwe miezi au Miaka kadhaa...!!!Tumeona kwa Mhe. Peter Lijualikali(MB)-Kilombero kwa kufungwa jela miezi 6 kwa kosa la kubambikiwa tu...kisa ni Mbunge wa Upinzani. Lakini Babu Seya na kijana wake waliobaka watoto wetu leo wako huru na walishakaribishwa Ikulu na Rais Magufuli kama Wafalme!!!Hii ni kitu haiingii akilini asilani!!!!.
Nina hakika Dunia inaposoma na kusikiliza Habari za Tanzania inajiuliza mara 2 hii nchi inaongozwa na watu wa aina gani. Si ajabu M-7 amempongeza Rais Trump wa Marekani kwa kuwapa vidonge vyao viongozi wa Afrika akiwemo na M-7 mwenyewe kwa namna wanavyo lidhalilisha Bara la AFRIKA!! Heshima ya Afrika imeondoka na kina Nyerere,Mandela, Nkrumah na Kaunda kwa kuwataja wachache...!
Wasalaam.