Hii ni bure inayogharimu...nikiwa kama mdau wa elimu ningemshauri raisi autathmini tena huu mpango wa elimu bure,wanaomwambia mambo yanaenda wanamdanganya,huenda wanaogopa kumpa Mh. Raisi habari isiyompendeza.
Shule hazina walimu wa masomo ya science,mwanzoni kabla ya bure walikua wakiajiriwa na shule,serikali imepiga marufuku huku kukiwa hakuna suluhisho juu ya hilo,hata kama hoja hii itatetewa na utaratibu uliowekwa ili Mkuu wa shule aweze kuchangisha michacho,utaratibu huo una milolongo mirefu ambayo mwisho wa siku wakuu wengi hupotezea na kuacha mambo yajieendee kama yalivyo,mwisho wa siku watoto wanakosa haki yao ya kusoma masomo ya science.
Pia kuna swala la hizi pesa kutofika kwa wakati au kufika katika kiwango kidogo kulingana na idadi/ukubwa wa shule na gharama za uendeshaji,hali hii hufanya wakuu kushindwa kuendesha vizuri shule kutokana na kupewa bajeti ndogo.
Kulingana na spidi ya utawala wa sasa wengi wa waliopewa madaraka ya kuongoza taasisi Fulani fulani wamekua waoga wa kuongea ukweli ya kua mambo hayaendi kwa watu wa ngazi za juu yao kwa kuhofia kuonekana hawaendani na kasi ya utawala au kutumbuliwa jipu..
Nitashangaa sana nikiona ufaulu wa mwaka huu ukiongezeka haswa kwa masomo ya sayansi tena kwa shule zetu hizi za kata,haswa hizi zilizopo vijijini...